KUANDIKISHA BIASHARA
Kabla ya kuanza biashara, sharti isajiliwe kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Jina la Biashara
Biashara sharti iwe na jina na inaweza
kuandikishwa kama ya mtu mmoja, kampuni,
ushirika au ubia.
Kama biashara yako itakuwa ya mtu mmoja
(sole proprietorship) itakupasa kufuata
utaratibu huu:-
(1)Chagua jina la biashara (2) Andika barua
kwa Mkurugenzi wa BRELA ukiomba
kuangaliziwa jina ulilochagua kama halijasajili
na mwingine (kwa sasa unaweza kuangalia
mwenyewe kutoka tovuti:
BRELA),
(3) Baada ya jina kupita jaza fomu nambari 2
na 3 ambazo unaweza kuzipata toka tovuti ya
BRELA (4) Lipia ada ya usajili ya Sh. 6,000/=
(5) wasilisha fomu na baada ya siku chache
utapatiwa hati ya usajili.
Kama unataka kusajili kampuni yenye ukomo
(Limited Liability) itakulazimu kuzingatia
yafuatayo:-
(1)Kampuni lazima iwe na watu si chini ya 2 na
wasizidi 50 (2) hakikisha jina la kampuni
utakalopendekeza liwe halijawahi kutumika
katika tovuti ya BRELA:
BRELA (3)
Andaa hati ya makubaliano (MEMARTs) (4)
Jaza fomu nambari 14a na 14b (5)hakikisha
MEMARTs na fomu 14b zimesainiwa na wakili
au mwanasheria (6)Lipia gharama za usajili
kulingana na mtaji unaoanza nao, (7) wasilisha
maombi yako na hati ya usajili itatolewa baada
ya muda mfupi.
JISAJILI KAMA MLIPA KODI (TIN
NUMBER)
Mfanyabiashara pia anapaswa kujisajili
mamlaka ya kodi TRA. Ili kujisajili unapaswa
kuzingatia yafuatayo: (1) uwe na hati ya usajili
(2) uthibitisho wa eneo la biashara.
LESENI YA BIASHARA
Biashara zote lazima ziwe na leseni na vibali
maalum ambazo hutolewa na ofisi za biashara
za halmashauri ya Manispaa au Wilaya ya eneo
la biashara yako. Baada ya kupata leseni na
vibali toka maamlaka husika unaweza sasa
kuanza biashara yako.
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums