Kusambaza nyama ya kuku

Kusambaza nyama ya kuku

Kig

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
1,076
Reaction score
458
Nafikiri kuanza biashara itakayohusisha kununua kuku toka kwa wafugaji, kuwachinja, kuhifadhi nyama kwenye freezer, na kusambaza kwa wateja hasa migahawani, kwa wachoma chips na mahotelini kama nikipata tenda. Tatizo ni kwamba sijajua changamoto kubwa za hii biashara maana kabla ya kuanza biashara lazima mtu ajue changamoto za biashara husika ili ajiandae kupambana nazo. Tafadhali naomba sana wale wenye uzoefu, na wenye ujuzi na hii shughuli wanifungue macho jamani ili nisiingie kichwakichwa. Asanteni.
 
Just kuwa na Usafiri wa uhakika kurahisisha delivery zako na kwa wakat pikipiki zinafaa zaid.
Usafi ni muhmu sana.
Hakikisha unavibali vya serikali hasa vya mazingra.
Kuwa na Packaging nzur na inayovutia.
Quality ni muhimu sana xo kuku lazma wawe na afya na wawe wametayarishwa ktk ubora wake.
Lengne maybe ni Keeping up with orders lazma uwe na flow nzur ya upatkanaj wa bidhaa zako sio leo kuku wapo kesho wameisha...
Nyongeza labda ni vizur ukawa na logo yako ambayo itatambulisha bidhaa zako na kampun yako kirahis zaid kwa wateja wako.
Na dhidi kumuomba mwenyez mungu..[emoji106]
 
Upo wapi? Kama upon arusha njoo nikupe broilers wakubwa kwa 5000
 
Nafikiri kuanza biashara itakayohusisha kununua kuku toka kwa wafugaji, kuwachinja, kuhifadhi nyama kwenye freezer, na kusambaza kwa wateja hasa migahawani, kwa wachoma chips na mahotelini kama nikipata tenda. Tatizo ni kwamba sijajua changamoto kubwa za hii biashara maana kabla ya kuanza biashara lazima mtu ajue changamoto za biashara husika ili ajiandae kupambana nazo. Tafadhali naomba sana wale wenye uzoefu, na wenye ujuzi na hii shughuli wanifungue macho jamani ili nisiingie kichwakichwa. Asanteni.
Business idea umeshaipata ifanyie kazi.Katika kuifanyia kazi utakumbana changamoto zako kipekee, usiulize watu wakupe changamoto za biashara uliyoibuni wewe.
Kwa kifupi, hongera kwa kubuni biashara ianzishe utajifunza mengi.Tayari kwenye thread yako supplier wa nyama ya kuku kajitokeza.
 
Hapo safi sana fanya hivi..nakushauli kabla ujaleta mzigo andaa ZIARA nenda kila banda la chipsi kila Mgahawa,Hotels nenda omba kuwapelekea nyama hizo tena ikiwezekana punguza na bei..atleat pata kama watu 50 watakao kubali kuwapelekea kuku..then anza kazi...
 
Back
Top Bottom