Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 458
Nafikiri kuanza biashara itakayohusisha kununua kuku toka kwa wafugaji, kuwachinja, kuhifadhi nyama kwenye freezer, na kusambaza kwa wateja hasa migahawani, kwa wachoma chips na mahotelini kama nikipata tenda. Tatizo ni kwamba sijajua changamoto kubwa za hii biashara maana kabla ya kuanza biashara lazima mtu ajue changamoto za biashara husika ili ajiandae kupambana nazo. Tafadhali naomba sana wale wenye uzoefu, na wenye ujuzi na hii shughuli wanifungue macho jamani ili nisiingie kichwakichwa. Asanteni.