Kusema hapana sio dhambi

Killing machine

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
2,052
Reaction score
2,995
Kuna wakati tunaingia kwenye ugomvi na watu kwasababu ya kushindwa kusema hapana

Na Kuna wakati tunaingia kwenye magumu ambayo hatuku paswa kuya pitia kwa kushindwa kusema hapana

Unapo shindwa kufanya Jambo na watu wakataka kukupa dhamana ya kulifanya ili Hali unajua huwezi kulifanya

basi una weza kukataa kwa kusema hapana sita weza kufanya Jambo Hilo kwasababu siwezi kulifanya

kwani kufanya hivyo sio dhambi

Dhambi mbaya nikuahidi/kujitangaza kwamba utafanya au unaweza kufanya Jambo ambalo hauwezi kufanya

kiasi kwamba hata usinge fanya hivyo usinge pungukiwa chochote hiyo ndiyo dhambi

1. Usiahidi Kama huwezi kutimiza kumbuka ahadi ni Deni na dawa ya Deni nikulipa

na usipo lipa basi utalikwepa sana lakini mwisho wa siku you have no way out utalilipa tu.

2. Usifanye Kama hauvutiwi kufanya kwa lengo la kuwa frahisha watu/mtu kwa wakati huo

kumbuka Kuna wakati unakuja lazima utimize ulicho ahidi kukifanya na hata usipo fanya ahadi yako ita kuhukumu Kila uwaonapo ulio wa ahidi

3. Ahidi kufanya kile unacho weza kufanya kinyume na hapo sio lazima kufanya hivyo Kama unajua huwezi kufanya hivyo

Mwisho

Usiahidi kufanya kitu ambacho unajua huwezi kufanya kitakughalimu baadae naghalama hiyo huanzia pale unapo shindwa kufanya

Hivyo tujifunze kusema hapana katika Yale tusiyo weza kufanya,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…