Kusema kweli Ada ya kufanyia miamala imepanda mara dufu

Kusema kweli Ada ya kufanyia miamala imepanda mara dufu

Tusilaumu sana kampuni za simu bila kuangalia chanzo ni nini!!

Nadhani mnakumbuka kipindi kile serikali ilisema kwamba inaongeza kodi kwenye miamala ya kutuma/kutoa fedha,wadau walipiga Sana kelele kwa kudai kwamba Mzigo wote ataaubeba mwananchi maana hizo kampuni za simu ni wafanyabiashara na katu mfanyabiashara hatataka apate hasara hivyo na yeye ataongeza gharama ambapo mwisho wa siku Mzigo wote anaubeba mtumiaji wa mwisho/mteja(mwananchi)

Tukija kwenye suala la kuongezeka kwa gharama za miamala hili nalo sidhani kama kuna haja ya kufikiri Sana. Ni wazi na sote tunajua kwa sasa mapato yamepungua maana watu wengi wamefunga biashara zao,misaada imepunguzea na mingine kukatwa kabisa kutokana na sababu mbalimbali hivyo ili kufidia pengo lililoachwa serikali haina budi bali kuongeza Kodi ndo hayo mnayoyaona sasa vitambulisho mpaka kwa wapika vitumbua,waokota chupa,kampuni za simu,nk. Na hii haitaishia hapo kuna mengi yanakuja.
Yajayo....

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly,,,,,,serikali inawaongezeaa makampuni hayo kodi kimya kimyaa lkn wanajua kabisa ni mzigo wa mwananchi
Ht wenyewe wanatumiaa huduma hizo zote na wanayaonaa lkn hakuna namna lazima wapate kodi,,,,,,,,huko ndio kuna urahisi wa makusanyo na watumiaji ni maelfu kwa maelfu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes, wengi hatufuatilii wizi wa hizi taasisi za kifedha. Jana ndiyo nimegundua kuwa CRDB huduma zao za kutoa fedha kwa wakala "wanatupiga sana", WAKALA ukimuuliza gharama ya muamala atakwambia haizidi hata Elfu Moja, nadhani wale wanaopendekeza wawe wanahifadhi fedha zao ndani ya nyumba wako sawa kwa kutumia kigezo cha makato makubwa.
moto,viabaka, wizi ndani ya familia hizo risks nazo zipo ila ukweli afadhali mtu ukawa na safe yako maana!! kila angle unakamuliwa tu
 
siku hizi nikitaka kutoa pesa naenda kwa wakala kusubiria wateja wanaokuja kuweka pesa, nawatumia huku nikikatwa pesa kidogo huku wao wananipa cash.
una akili kama mimi,nimekua nikifanya hivyo kwa muda mrefu lakini kwa wakala ambae nafahamiana nae vizuri
 
Back
Top Bottom