Tusilaumu sana kampuni za simu bila kuangalia chanzo ni nini!!
Nadhani mnakumbuka kipindi kile serikali ilisema kwamba inaongeza kodi kwenye miamala ya kutuma/kutoa fedha,wadau walipiga Sana kelele kwa kudai kwamba Mzigo wote ataaubeba mwananchi maana hizo kampuni za simu ni wafanyabiashara na katu mfanyabiashara hatataka apate hasara hivyo na yeye ataongeza gharama ambapo mwisho wa siku Mzigo wote anaubeba mtumiaji wa mwisho/mteja(mwananchi)
Tukija kwenye suala la kuongezeka kwa gharama za miamala hili nalo sidhani kama kuna haja ya kufikiri Sana. Ni wazi na sote tunajua kwa sasa mapato yamepungua maana watu wengi wamefunga biashara zao,misaada imepunguzea na mingine kukatwa kabisa kutokana na sababu mbalimbali hivyo ili kufidia pengo lililoachwa serikali haina budi bali kuongeza Kodi ndo hayo mnayoyaona sasa vitambulisho mpaka kwa wapika vitumbua,waokota chupa,kampuni za simu,nk. Na hii haitaishia hapo kuna mengi yanakuja.
Yajayo....
Sent using
Jamii Forums mobile app