KUSEMA KWELI CHUO NI CHUO....CHA UMUHIMU NI KUPATA AJIRA....soma wosia huu

KUSEMA KWELI CHUO NI CHUO....CHA UMUHIMU NI KUPATA AJIRA....soma wosia huu

vijana wngu,nimesha tafuta vijana wa kazi TBS,kwa njia ya interview lakini wengi ni wenye first clas lakin wanakosa nafac,sababu ni kwamba pamoja na cheti,tunakuuliza maswali mengi sana,tunaangalia uvaaji wako,vyeti vyako vya nyuma na extra experience,so unakuta ni mzuri kimasomo lakini hana ujuzi mzuri wa kazi,sasa vijana jitahidini kufaham kila kitu na msaidiane sio kusemana,usimzarau ucyemjua.
Kuna Makampuni mengine yanahitaji fresh graduate na mengine graduate ambao wana uzoefu kazini.Sasa wewe ujiangalia uko upande gani.
 
nahisi ile ligi NGUMU HUMU JF inataka anza tena...mh...
 
You do have a point zawadi machibia kasoma st john(iliyokua mazengo)lakini saii yupo bbc anakula bata kila cku jion yupo hewan,wangap wamesoma hiyo mass com kwenye vyuo vinavyotambiwa na wanavuta ndala,any way chuo chochote ni mchongo
 
Shule ni kazi au ajira? Let us change our Minds. Mimi binafsi nimesoma, nlivyomaliza nikapata ajira ya serikali lakini sasa natafuta kazi kwa maana hali ya kuajiriwa nimechoka. Twende shule na tushuriane jinsi ya kutengeneza kazi na sio ajira. Muda upo tusiangalie chuo wala mshahara maana vyote ni utumwa.
Shukrani
 
Harvard university, Yale university then University of Dar es salaam, Dodoma University na Dar Es Salaa Institute of Technology unadhani yupi atapewa kipaumbele? kuna vyuo ni lulu madogo acheni kujijaza upumbavu.........:director:
 
vijana wngu,nimesha tafuta vijana wa kazi TBS,kwa njia ya interview lakini wengi ni wenye first clas lakin wanakosa nafac,sababu ni kwamba pamoja na cheti,tunakuuliza maswali mengi sana,tunaangalia uvaaji wako,vyeti vyako vya nyuma na extra experience,so unakuta ni mzuri kimasomo lakini hana ujuzi mzuri wa kazi,sasa vijana jitahidini kufaham kila kitu na msaidiane sio kusemana,usimzarau ucyemjua.

acha kufariji watu, haya mambo ya kupata ajira kuna usanii mwingi sana nyuma yake....hapa nawaza kujiajiri tu.
 
wewe utakuwa umechaguliwa teku ndio maana halafu unajifananisha na watu wa mzumbe ,na sua au umeenda udom chuo cha kata

We acha kumeza chuo kikubwa afrika ya kati na mashariki unaxema chuo cha kata na km ndivyo cha wilaya,mkoa ni vp hvyo.
 
Binafsi huwa sipendi sana kuchangia maada kama hii maana kunawatu walibatizwa kwa majina ya vyuo vyao, yaani wao jina tu kwao faahari mi ndo nadhani vijana tunakosea sana, mtu anaenda chuoni anabweteka tu hata hakazi msuli kisa kafika kwenye chuo ambacho pengine kweke ni bora, pili hivi inamaana wote waliomaliza kwenye hivyo vyuo ambavyo tunafikiri si bora wote hawana ajira kwa sababu tu vyuo vyao si bora?Vile vile je waliosoma vyou ambavyo vinasemekama kuwa bora wote wanakazi mitaani?Na je? vipi kuhusiana na feedback kutoka kwa jamii (yaani performance yao hawa watu wawili kazini ipi ipo juu?Na mishahara yao je inatofautiana kulingana na chuo?je? nini kazi ya TCU katika hili ina maana haifanyi kazi yoyoteBinafsi nikifikiria haya huo simwelewi vizuri huyu anayesema chuo fulani ni bora sana kuliko kingine na kitukingne ni kwamba mambo yanabadilika ubora wa chuo fulani wa miaka ya 90s unaweza ukakuta sio wa leo halafu nyie mkakalili tu kwamba chuo hiki bora.
 
Sasa dudu kila mtu akianza kutambia programme anayoenda kuisoma...,sipati picha jf itakuwa na sura gani. Kama ni kujivunia allocation ni vyema uifanyie moyoni kwako tu. Binafsi na wadau wengine tunaliona hili kama sio la kiukomavu. Nawasilisha!!
 
siku ya leo nataka kuvunja mzizi wa fitina maana humu ndani yametokea mabishano na mada kuhusu
1.baadhi ya watu kusifia vyuo vyao.....
2.baadhi ya watu kuponda baadhi ya vyuo

kusema kweli chuo ni chuo....ili mradi kinatambuliwa na serikali na tcu.....kitu muhimu katika kusoma elimu ya
chuo kikuu ni baada ya kuhitimu uweze kupata ajira ambayo itakuwezesha kuendesha maisha yako...ya badae

so usije ukakariri....kwamba eti mimi nasoma chuo flani ni bola kuliko mwengine cha umuhimu ni kumuomba mungu
upate michongo wa kazi,,,,,usijidanganye eti ya kwamba kisa nimesoma maarufu eti nikimaliza chuo napata kazi hapo hapo kitu kama hichi hakuna............na huu ni wosia wangu........kwani watu wengi tukiwa vyuoni tunadanganyana sana

na mwisho nawahusia ndugu zangu.......ombeni sana mungu mpate michongo ya kazi....mtaani ni kugumu sana

hapa aisee watu wanaweza kuongea meeeengi saaana na hasa wale ambao ni kama "wamechomwa sindano" za vyuo vyao...anyway.

mbavu zangu zinazidi kuuma pale ninapoona wanajamvi waliochaguliwa kuingia kwenye vyuo flani wanavyotamba kuhusu majina ya vyuo walivyopangiwa...cha msingi Mwenyezi Mungu awafanikishe kuweza kupambana na drama za vyuoni, wasome kwa bidii na kukabiliana vyema na roho za supplementary na pepo la discontinuation likae mbali...AMEN!

Kuchaguliwa kwenye chuo ni moja, kudumu chuoni na kugraduate ni suala lingine, kufanikisha lyf after graduation ni suala lingine kabisaaaa. suala ni kwamba, hata usome "under the mango tree polytechnic college" kama kinatambulikia na taasisi zinazosimamia elimu nchini na at the end of the day maarifa uliyopata hapo yanakupa uwezo kupambana na challenge za kimaisha ikiwemo za kifedha...then good to go!
 
Daaa hapo harvard kuna mshikaji wangu wa kitaa hapa mikocheni anasoma hapo
Harvard university, Yale university then University of Dar es salaam, Dodoma University na Dar Es Salaa Institute of Technology unadhani yupi atapewa kipaumbele? kuna vyuo ni lulu madogo acheni kujijaza upumbavu.........:director:
 
wake up pipo cku hzi kupata kazi ni kwa kujuana.in short u shud have godfathers.xaxa we jitape unaxoma chuo kzur cjui kozi nzur alafu uone utakavyo hangaika na degree yako mitaani
 
Sasa dudu kila mtu akianza kutambia programme anayoenda kuisoma...,sipati picha jf itakuwa na sura gani. Kama ni kujivunia allocation ni vyema uifanyie moyoni kwako tu. Binafsi na wadau wengine tunaliona hili kama sio la kiukomavu. Nawasilisha!!

wakubwa kama nimewakosea naombeni samahani it's was just a typing error sio kama nimedharau kozi nyingne samahanini sana wakubwa !!
 
wakubwa kama nimewakosea naombeni samahani it's was just a typing error sio kama nimedharau kozi nyingne samahanini sana wakubwa !!

dogo acha uongo, typing error!! Sema thinking error.
 
Back
Top Bottom