Kiranga anakuwaga sahihi Sana kwenye nchi established..kama hizo USA na UK..zenye traditions za mda mrefu ..Sisi hata hao washauri wa Rais hatuwajui...wala vetting ipi imetumika kuwapata hatujui...Sisi ni nchi changa sana kumlaumu Rais Kwa kilakitu sio sawa let alone an accidental president
Kwanza kabisa, Samia Suluhu Hassan si accidental president.
Kama unakubali kuwa CCM ilishinda uchaguzi 2020, basi watu walichagua tiketi ya Magufuli/ Samia. Hakuchaguliwa mtu, ni tiketi ya watu wawili, mgombea urais, na mgombea mwenza anayekuja kuwa VP.
Na kuwa VP maana yake ni kwamba you are a heartbeat from the presidency. Watu walikuwa wanatakiwa wajue kwamba rais anaweza kufariki madarakani, na akifariki madarakani, tumempitisha huyu Samia kuwa rais.
Tatizo Watanzania wengi wanakwenda kwa mazoea, walifikiri rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufia madarakani, walifikiri Samia atakuwa pambo tu, afanye kazi cwremonial za kukata tepe, kuzindua majengo na kuwakilisha nchi kwenye misiba.
Sasa Magufuli alivyofariki, ndiyo wanajiona wana accidental president.
Accidental president kivipi wakati katiba imewaeleza kabisa kwamba rais akifariki, makamu wa rais anakuwa rais?
Kitu kinajulikana kabisa na kipo katika katiba, kwa nini mnakiita accident?
Kifo kinajulikana kipo, kwa nini mnakiita accident?
Samia ni rais fair and square, if at all umekubali matokeo, na hata kama hukubali matokeo that is a separate and even bigger issue.
Kuhusu nchi changa na nchi established, hoja yako haina mashiko.
We are nit talking about nuclear reactors here, we are not talking about sending people to tye moon.
Kusema huko nchi changa ni tofauti na nchi zilizoendelea katika hili la ushauri ni makosa, ni kujidogosha tu.
Kwa sababu nimekutolea mfano mzuri sana wa rais J.K Nyerere alivyopewa ushauri mbaya, na alivyoufanyia vetting, akatumia unofficial advisers, akafanya tofauti na alivyoshauriwa na washauri wake rasmi.
Kama Nyerere aliweza kufanya hivyo 1970s, kwa nini rais mwingine yeyote aliyemfuatia ashindwe kufanya hivyo?