Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Tunapitia wakati mgumu wa kuchunga kauli zetu tunapozungumza na media au tunapokuwa kwenye majukumu yetu.
Binafsi naendelea kuitafakari kauli ya CEO Kasongo kutupiga marufuku wasemaji kufanya mzaha kwenye statements rasmi za klabu. Ni kweli kuna kundi la watu hatuwatendei haki kwa kufanyia mzaha taarifa za timu zao wanazozishabikia. Lakini tukiwa serious sana mpira utaboa. Mpira ni mchezo wa kutambiana. Tambo zina raha yake.
Utani na vijembe ni culture ya mpira wetu iliyoasisiwa na Simba na Yanga. Pengine culture hii ndio inanogesha soka letu. Kwa mfano nakumbuka nilipokuwa serious sana nikaambiwa nimepooza nichangamke kidogo. Nimechangamka mambo yanaenda. CEO wa Bodi ya Ligi hataki!
Nadhani hili linahitaji mjadala zaidi au wakubwa waache tu culture iamue!