Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Si Wajerumani wala Uingereza walioiba chochote hapa kwetu, kwanza hata walipoteza zaidi kuliko walivyowekeza Wajerumani walijenga reli, barabara, mipango miji, geographical survey ya nchi yote, walifanya utafiti wa udongo na kupima matone ya mvua na kuamua wapi palimwe nini, walileta mazao ambayo hayakuwepo kama kahawa, pamba, mahindi, miwa (sukari), katani, viazi ulaya, matunda kama machungwa, mananasi, ndizi, mapeasi, n.k.

Sasa kwa nini Mwalimu Nyerere & Co. walitujaza chuki dhidi ya Ukoloni? Siongelei Afrika yote najua kuna nchi kama Kongo, Kenya au hata Uganda na Zambia Mzungu aliiba lakini kwetu aliiba nini?

Hata Madini yote tunayochimba leo ramani iko Serikalini ya tangia Mkoloni mpaka gesi ya Mtwara Mkoloni alishafanya tulichofanya ni kufukunyua makrabasha tu lakini Serikali inajua wapi kuna gesi, madini ya karibia aina zote yanayopatikana Tanzania.

Hizo highways Rais Magufuli anataka kujenga mpaka Chalinze mipango ipo, hata hilo Daraja la kuunganisha Oysterbay na Salenda ni jipya labda halikuwepo kwenye mipango ya Mkoloni lakini Mjerumani alipanga kupitisha highway baharini (ndo maana ya Ocean road leo hii Barack Obama road) hadi Bunju kuunganisha Ocean Road (RIP), Oysterbay, Msasani, kuunga na barabara ya Bagomoyo vyote vipo, na ndivyo nilivyosikia Serikali wanataka kufanya sina uhakika lakini.

Tubadilishe historia yetu, mzungu sio adui wetu, kwa Kenya ni sawa hata wana masettlers mpaka leo lakini siyo kwetu, hata utalii alitengeneza Serengeti, Ngorongoro kama hifadhi ni Mkoloni pia, Milima Kilimanjaro au Meru aliyejenga njia na miundombinu ya kupanda kufika Kileleni ni Mkoloni pia.

=====

Hoja za wachangiaji
Hamjui chochote kuhusu Ukoloni Wala wakoloni. Rudini darasani mkasome Historia. Mmesahau kuwa waliondoka na Masalia ya Mnyama mkubwa zaidi kuwahi kutokea Duniani. Waliondoka na nafsi za Mashujaa wetu wapendwa waliopigania Ardhi zao. Walitufanya watumwa kwenye mashamba yao ya mikonge na pamba. Pia umesahau kule Manda Wareno waliua kuanzia Vichanga, Mbwa wakakata mpaka minazi na awakuacha mtu hai hata mmoja.

Waliwabaka Bibi zetu, hasa mikoa ya kusini na kutumia watoto wa kiafrika katika Uwindaji wa mamba. Wakawachapa Babu zetu na kuwadhalilisha mbele ya Familia zao kisa Kodi. Kifupi walifanya mabaya mengi sanaaaa kiasi siwezi kumaliza kuorodhesha yote. Lakini kibaya zaidi walitupachika Ugonjwa mmbaya Sana na waajabu na ndo unao watafuna hata nyinyi vijana wa sahizi Kwamba Mzungu ni Super race. Maana aliwafanya mjione wajinga na msio faa dhidi yao. Kuhusu Ujenzi na Research, walifanya kwa maslahi yao Binafsi na uchumi wao!!! Lakini aminini nawaambieni. Uwekezaji wao haufiki hata Robo ya thamani kwa Roho Walizo zikatisha nnchini na Udhalilishaji walio tufanyia.
-------------
Mtazamo wako ni wa juu-juu tu, unagalia vitu unavyoviona leo. Lakini nikuulize, fedha za zao la mkonge walikuwa wanazileta hapa Tanganyika? fedha za almasi nazo walizileta au hata mazao mengine waliokiwa wanapora wananchi walizileta. Reli unayoisema wewe ilijengwa kwaajili ya kumsaidia muafrika au mkoloni. Asilimia 20% ya watu wetu walipoteza maisha kutokana na njaa na magonjwa, hivi vitu viliweza kuepukika kama sio wakoloni kusomba mazao yao yote na kupeleka kulisha ndugu zao Ulaya.

Hapa hapa Tanzania ya leo, kuna maeneo (sitaki kuyataja) ambayo wewe unapita kila siku chini kuna makaburi ya pamoja ya watanzania waliokufa kwenye vita vya mkoloni na wengine kwa magonjwa na njaa. Mnatupwa kama mzoga bila alama yoyote.
--------------
Nani huyu asiyekumbuka matendo maovu ya Karl Peters(mkono wa chuma), biashara ya watumwa iliyochagizwa na wazungu, wizi wa mali mf: ngozi za wanyama, pembe za ndovu, madini mbalimbali, kutujengea miundo mbinu ambayo haikuwa na lengo la kimnufaisha mtu mweusi, elimu yenye ubaguzi na utabaka, kutuhubiria dini zenye kutusahaulisha asili yetu, utitiri wa kodi, ukiukwaji wa haki za mtu mweusi kama vile kuchukua ardhi kwa mabavu, kutumikisha watu bila malipo au kwa ujira kiduchu na kwa muda mrefu bila kupumzika, kuibwa kwa masalia ya mifupa yaani skeleton ya mijusi wakubwa yaani (dinosaurs), kuharibu viwanda vyetu asili vya kipindi kile ambavyo ndio ungekua msingi wa ubunifu wa leo, kutujengea viwanda vidogo visivyo na tija yaani (processing industries) siyo heavy industries, kuwafanya baadhi ya makabila kuwa vibarua wa kidumu hadi leo.

Kiujumla nakishangaa kutetea wakoloni, yaani hata kina Kinjekitile Ngwale na Mkwawa walipambana na huu udhalimu bado wewe msomi wa Leo unatetea! Dah

Wakoloni ni wabaya zaidi ya wabaya hasa kupitia matendo yao makuu matatu yaani Creation, Destruction & Preservation.
Si kwamba nawatetea waarabu la hasha! Naongelea upande wa wazungu kuanzia kwa wareno, wajerumani na waingereza. Waarabu nao wana shida zao pia
--------------
Mkoloni hasa Mjerumani aliondoka Tanganyika akiwa ameijenga vizuri mzizima (Baadae ilikuja kuwa Dar es Salaam). Majengo yote mazuri ikiwemo Ikulu na majengo ya serikali yote alijenga. Alipanga miji karibia yote na kutengeneza master plan akielekeza watu wajenge na kuishi kwa ustaarabu.

Alijenga pia reli na kuhamasisha kilimo cha Mazao ya biashara. Alijenga viwanda vya kuprocess law materials kwa ajili ya usafirishaji.

Kulikuwa na shule za wamissionary aliowaruhusu kuja kujenga. Kulikuwa na wafanyabiashara sliowaruhusu kuja kuwekeza na kufanya biashara.

Ufike muda tuseme ukweli. Mkoloni alikuwa anafanya maendeleo makubwa sana Tanganyika na Tanganyika ingekuwa nzuri, iliyojengeka vizuri na tena kimpangilio chini ya mkoloni.

Tanganyika ilikuja kuharibika baada ya Mzee Nyerere kuanza kuweka vitu vyake hasa ujamaa n.k.

Mengi anayoyafanya Mh Magufuli leo na tunamsifia sana Mkoloni aliyafanya kwa kiwango kikubwa sana hasa ujenzi wa miundombinu
-------------
Tutafakari kwa hoja. Je, hali ya mwafrika kabla ya wazungu kuja afrika na baada ya kututawala akaondoka, ilizidi kuwa mbaya au iliboreka?

Je kama wazungu wasingewahi kukanyaga Afrika kabisa mpaka leo hii 2019, Afrika tungekuwa wapi? Tungekuwa na maendeleo ya teknolojia kiasi gani? Tungepiga hatua kiasi gani kupambana na magonjwa na maradhi, tungekuwa na mataifa?

Hata China, Singapore, Malaysia walikuwa makoloni. Ukoloni ulitunyonya ndio lakin kupitia maumivu hayo tulipiga hatua nyingi tu za kimaendeleo kama binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waasisi wa tanu na ccm ni watu wa mwambao ambao wengi walipokea dini ya mwarabu hawa ndiyo waliochangia kujaza propaganda kuwa wazungu wa ile dini ya magharibi kuwa ni wabaya sana. watu hawa wa mwambao wameshiriki sana katika kuandika vitabu vya kufundishia shule zetu, vitabu vyenye kujaa historia ya upotoshaji.

Jiulize jambo moja: ni wapi waarabu walijenga japo mita moja ya reli? ukinitajia nidai buku.
 
hawakuiba sawa, lakini walitutawala bila ridhaa yetu, ubaguzi wa elimu, dini, kabila, walitugawa sana ili watutawale vizuri
 
waasisi wa tanu na ccm ni watu wa mwambao ambao wengi walipokea dini ya mwarabu hawa ndiyo waliochangia kujaza propaganda kuwa wazungu wa ile dini ya magharibi kuwa ni wabaya sana. watu hawa wa mwambao wameshiriki sana katika kuandika vitabu vya kufundishia shule zetu, vitabu vyenye kujaa historia ya upotoshaji.

jiulize jambo moja: ni wapi waarabu walijenga japo mita moja ya reli? ukinitajia nidai buku.

Sijui kwa watu wa mwambao unamaanisha nini, lkn kama ni Waarabu walijenga pia tena sana tu mfano Stone town Zanzibar, Miji mashuhuri na ya kihistoria kama Kilwa, Bandari Mikindani, hata ramani ya reli treni kutoka Kigoma - Dar ilifuata Karavani, Wajerumani hawakubadilisha kitu waliweka mataruma tu kwa ramani ambayo tayari ilikuwepo.

Lkn Mada haihusu Waarabu vs Muzungu.
 
hawakuiba sawa, lakini walitutawala bila ridhaa yetu, ubaguzi wa elimu, dini, kabila, walitugawa sana ili watutawale vizuri

Haya hayo ulioyataja hayakufanywa kwetu, kwingine sawa waligawanywa Ukabila au Dini lkn kwetu hilo halikufanyika na ndo maana tunaishi pamoja Dini zote.
 
Sasa hivi wakoloni wanajuta kuja africa kipindi kile, kama wangejua basi wangebakia huko kwao na kujenga mataifa yao. Sisi africa kiukweli hatuna "FADHILA WALA SHUKRANI".

Dunia hata itusaidie vipi, iwe kwa misaada ya dawa na fedha au wataalamu, malipo tunayowapa ni matusi na kejeli.
 
Kuna vyama vya siasa vinaiba na ni vibaya na vina ukatili kuliko mkoloni nakuambia. Kwani wakati wa ukoloni kulikuwa na rushwa nchini? Ufisadi?

Kwa mfano, ubaya wa mkoloni Mreno kule Msumbiji ulikuwa nini? Maana weusi waliruhusiwa kila kitu hata kuoa wazungu na kuwa raia wa Ureno na kwenda kuishi Ureno, hata kuwa kwenye timu ya taifa ya soka ya Ureno kununua nyumba Ureno popote walipotaka nk, isipokuwa kuwa viongozi wa Msumbiji. Hata baa walikunywa pamoja weusi kwa wazungu.

Leo hii Brazil ni koloni? Maana weusi wa Brazil wameamua kwamba mambo ya uongozi wa nchi watawaachia wazungu kwa sababu waswahili wana mambo ya ajabu sana. Tofauti ni nini na ilivyokuwa Angola na Msumbiji?
 
Back
Top Bottom