RWEGOSHORA FROLIAN,
Nani asiekumbuka matendo maovu ya Karl peters(mkono wa chuma),nakukumbusha wapo viongozi wengi waafrika wenzetu walitawala nchi zao kwa Mkono wa Chuma na hata leo wapo wanaoendelea kufanya hivyo,umezungumzia kutujengea miundombinu ambayo haikuwa na lengo la kumfurahisha mtu mweusi lakini ukiangalia mpaka leo ipo miundombinu mingi iliyofanywa na hao wakoloni ambayo bado inatunufaisha kuliko iliyoanzishwa na waafrika wenzetu baada ya kujitawala.
umezungumzia suala la kuchukua ardhi kwa mabavu nataka nikukukumbushe hata kabla wakoloni hawajaja zilikuwepo WATEMI,WAFALME na viongozi wa koo waliokuwa wanaenda kuvamia koo zingine na kuteka ardhi na watuwake na kuwa chini ya himaya yao na wanakuwa kama watumwa tu kwenye himaya mpya.
kuhusu utitiri wa kodi hata sasa bado tunalalamikia utitiri wa kodi,sidhani kama ingekuwa ni hiyari kulipa kodi unadhani watu wangelipa kodi?
kutumikisha watu bila malipo hata sasa wapo watu wengi wanatumikishwa bila malipo au kwa malipo kiduchu.
mifupa ya mijusi mikubwa hata wangetuachia tungeifanyia nini kwa kipindi hicho?hata sasa inatusaidia nini zaidi ya kuiweka tukitegemea hao hao wakoloni waje kuitizama kwa kulipia pesa kuna faida yoyote nyingine tunaweza kuipata?
Hii mada aliyoileta mtoa mada ni ya kufikirisha sana,Tujiulize tu Je?kama wakoloni wasingekuja kututawala waafrika tungekuwa tunaishi maisha ya namna gani leo hii?maendeleo yetu tungeyapimaje?maana mpaka leo yapo maeneo hapa hapa Afrika watu wake wanaishi maisha yaleyale waliokuwa wanaishi waafrika kabla ya kuja mkoloni je?hizo madini pembe za ndovu na ngozi za wanyama zingekusaidiaje?
kwa mfano tuchukue kabila kama WAMANG'ATI,tungekuwa tunaishi hivyo maana wao wanaishi maisha waliyoishi kabla wakoloni hawajaja je?hayo madini yangewasaidiaje?
yapo maendeleo ambayo tungekuwa nayo kama waafrika lakini usifananishe na maendeleo haya tunayoyaishi ambayo yametokea kwa wakoloni.