kilama
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 2,745
- 1,989
Ningepata mtu angeelezea vizuri kuhusu ukoloni mamboleo, nafikiri hoja za mtoa mada zingejibiwa vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilibidi wawe wawekezaji sio kuwafukuza
Acha kupotosha. Kwani machief tuliokuwa nao hawakuua watu? Serikali zilizoundwa baada ya uhuru hazikuua watu?? Kwenye ukweli tuseme ukweli. Hao IMF na World Bank unaowasema ndo wanaofadhili miradi mingi nchini kwako ikiwamo ya utafiti wa madawa , ujenzi wa miundombinu Mf barabara unazoona zinajengwa kwenye miji na majiji mbalimbali sasaivi.Nimesikitika sana na watu wanaomuunga mkono mleta mada. Ama kweli kutokujua ulipotoka ni hatari. Mkoloni alifanya mambo yote kwa manufaa yake na aliua wengi sana. Hatuna cha kumshukuru mkoloni zaidi ya kumtupia lawama kwa uovu wake. Na kwa nyakati hizi mkoloni bado yupo akiwa kavaa koti la IMF na WB. Ni unyonyaji mtupu.
hawakuiba sawa, lakini walitutawala bila ridhaa yetu, ubaguzi wa elimu, dini, kabila, walitugawa sana ili watutawale vizuri
[/QU
Mkoloni hasa Mjerumani aliondoka Tanganyika akiwa ameijenga vizuri mzizima (Baadae ilikuja kuwa Dar es Salaam). Majengo yote mazuri ikiwemo Ikulu na majengo ya serikali yote alijenga. Alipanga miji karibia yote na kutengeneza master plan akielekeza watu wajenge na kuishi kwa ustaarabu.
Alijenga pia reli na kuhamasisha kilimo cha Mazao ya biashara. Alijenga viwanda vya kuprocess law materials kwa ajili ya usafirishaji.
Kulikuwa na shule za wamissionary aliowaruhusu kuja kujenga. Kulikuwa na wafanyabiashara sliowaruhusu kuja kuwekeza na kufanya biashara.
Ufike muda tuseme ukweli. Mkoloni alikuwa anafanya maendeleo makubwa sana Tanganyika na Tanganyika ingekuwa nzuri, iliyojengeka vizuri na tena kimpangilio chini ya mkoloni.
Tanganyika ilikuja kuharibika baada ya Mzee Nyerere kuanza kuweka vitu vyake hasa ujamaa n.k.
Mengi anayoyafanya Mh Magufuli leo na tunamsifia sana Mkoloni aliyafanya kwa kiwango kikubwa sana hasa ujenzi wa miundombinu
Ni ujinga kuaminishwa kuwa wakoloni ‘wazungu’ walikuja kunyonya malighafi Africa kwa sababu kwao hakukuwa na nazo za kutosha, eti walitulimisha mfano mahindi na mkonge kisha wakasomba vyote kupelekea ndugu zao huku sisi tukifa njaa.... kama hilo ni kweli je siku hizi mashamba yameongezeka huko Ulaya kiasi kwamba hawahitaji tena kuja kulima huku..?
Chaguo la Lubuva na Jecha litakuwa vipi chaguo la weng?Serikali iliyochaguliwa na watu zaidi ya Millioni 8, demokrasia ya kweli ni kuheshimu maamuzi wa watu wengi.
Nyerere alitaka sifa za kipuuzi, sasa amepelekea taifa kuwa na umaskini.
Kila siku nalisema hili na nitazidi kusema. Hakukuwa na maana ya kutufukuza wazungu. Labda kwa nchi nyingine lakini Tanzania hapana.
Nilishindwa kuelewa mantiki yake, ni mtu wa ajabu sana.Unawafukuza wakoloni kisha unaanza kusafiri kwenda kwao kila wakati ili kujipatia mahitaji yako, hapo ni kujiongezea gharama zisizo na tija.... Canada hadi leo bado ni koloni je wanakosa nini..?
Wewe unayejua tueleze tuelewe na tutoe hoja zetu, hii ni JF of GT si ukumbi wa kuunga mkono hoja.Kama hujui ubaya wa wakoloni mpaka umri huo basi bora unyamaze
Kwa tuliosoma shule za serikali enzi za mwingereza chini ya silabasi ya Cambridge hatuwezi kukubaliana na kiwango duni cha elimu iliyopo hivi sasa. Shule za kati (middle school) zilifundisha stadi za maisha zikiwemo ufundi na kilimo jambo ambalo hivi sasa halipo na elimu ni duni sana sana.Chochote walichokifanya wakoloni, walifanya kwa manufaa yao mapana.
Hata sasa bado sie ndio soko la bidhaa zao, chanzo cha mali ghafi za viwanda vyao n.k.
Tukiwa na dunia yenye amani na utulivu, watauza wapi silaha zao ikiwa wao ndio wazalishaji wa silaha?
Walijenga reli na barabara wakati uke zirahisishe usafirishaji wa bidhaa ziende kwao, hapo bidhaa inajumuisha watumwa, mafini, mazao n.k.
Tafiti walizofanya kuhusu maeneo yenye madini na miundo mbinu nayo ilikua kwa kusudi lilelile, kuwanufaisha wao.
Kusingekua ni kwa ajili ya maslahi yao kwanini waligombania maeneo ya Afika hadi kufikia kufanya mkutano wa kugawana bara letu?
Maovu na uzembe wa viongozi wetu baada ya uhuru umekithiri kiasi cha kufanya tuwakumbuke wakoloni, lakini haiondoi ukweli kwamba mkoloni hakufanya chochote kisicho na faida kwake.
Barbarosa pole sana, mbaya zaidi umesahau kusema kuna jamaa sasa hivi ametuletea lugha ya kuwaita wazungu mabeberu huku akiendelea kuwaomba watusaidie na kuwasifia kila wanapofanya hivyo.
Wakoloni hawa kama kweli wana kusudi na nia njema, UN wapo kuhakikisha dunia inakua salama na hatuna migogoro kati ya nchi na nchi huku haki za binadam zikipewa kipaumbele, lakini hilo halijawahi kufikiwa.
Mashirika yake ya maendeleo yamekuwepo zaidi ya miaka 70 wakijinasib kusaidia nchi kupambana na umaskini, kuimarisha utawala bora, kueneza demokrasia n.k lakini hakuna nchi hata moja wanaweza kuitolea mfano kwamba waliikuta na hali mbaya, wameisaidia na sasa imefikia pazuri wanaweza kuiacha ikajiendesha yenyewe, haipo.
Nabaki na msimamo wangu kwamba mkoloni alifanya yote kwa maslahi yake binafsi.