Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Wajerumani walikwapua dinosaur skeleton..liko pale Dinosaur hall Berlin
 
Tulitaka uhuru Kwasababu tulitaka tujitawale

Kongole kwa Rais Magufuli anatufanya tujivunie Uhuru wetu
 
RWEGOSHORA FROLIAN,
Nani asiekumbuka matendo maovu ya Karl peters(mkono wa chuma),nakukumbusha wapo viongozi wengi waafrika wenzetu walitawala nchi zao kwa Mkono wa Chuma na hata leo wapo wanaoendelea kufanya hivyo,umezungumzia kutujengea miundombinu ambayo haikuwa na lengo la kumfurahisha mtu mweusi lakini ukiangalia mpaka leo ipo miundombinu mingi iliyofanywa na hao wakoloni ambayo bado inatunufaisha kuliko iliyoanzishwa na waafrika wenzetu baada ya kujitawala.

umezungumzia suala la kuchukua ardhi kwa mabavu nataka nikukukumbushe hata kabla wakoloni hawajaja zilikuwepo WATEMI,WAFALME na viongozi wa koo waliokuwa wanaenda kuvamia koo zingine na kuteka ardhi na watuwake na kuwa chini ya himaya yao na wanakuwa kama watumwa tu kwenye himaya mpya.

kuhusu utitiri wa kodi hata sasa bado tunalalamikia utitiri wa kodi,sidhani kama ingekuwa ni hiyari kulipa kodi unadhani watu wangelipa kodi?
kutumikisha watu bila malipo hata sasa wapo watu wengi wanatumikishwa bila malipo au kwa malipo kiduchu.

mifupa ya mijusi mikubwa hata wangetuachia tungeifanyia nini kwa kipindi hicho?hata sasa inatusaidia nini zaidi ya kuiweka tukitegemea hao hao wakoloni waje kuitizama kwa kulipia pesa kuna faida yoyote nyingine tunaweza kuipata?

Hii mada aliyoileta mtoa mada ni ya kufikirisha sana,Tujiulize tu Je?kama wakoloni wasingekuja kututawala waafrika tungekuwa tunaishi maisha ya namna gani leo hii?maendeleo yetu tungeyapimaje?maana mpaka leo yapo maeneo hapa hapa Afrika watu wake wanaishi maisha yaleyale waliokuwa wanaishi waafrika kabla ya kuja mkoloni je?hizo madini pembe za ndovu na ngozi za wanyama zingekusaidiaje?

kwa mfano tuchukue kabila kama WAMANG'ATI,tungekuwa tunaishi hivyo maana wao wanaishi maisha waliyoishi kabla wakoloni hawajaja je?hayo madini yangewasaidiaje?
yapo maendeleo ambayo tungekuwa nayo kama waafrika lakini usifananishe na maendeleo haya tunayoyaishi ambayo yametokea kwa wakoloni.
 
infinix,
huko zanzibari umeenda mbali.mkumbushe tu hata kabla ya kuja wakoloni kulikuwa na vita zinapiganwa za kuvamia na kuteka ardhi,watu,mifugo na kilakitu cha himaya za makabila,koo zingine na kuwa chini ya koo zilizoshinda vita,na watu walikufa pia tofauti ipo wapi?
 
Mwanzi1, Hahahaha we jamaa upo mwepesi sana kichwani,kwani sasa watu hawafi na njaa?au hawauliwi na hao viongozi weusi wanao watawala?Kweli wazungu walikuwa na mabaya lakini mengi mazuri,kuliko tulio waamini sasa tukijua ni wenzetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wametufanya tuwe tegemezi kwao, mpaka leo tumekua dormant hatuwezi fanya kitu tunasubiri kuletewa na Wazungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
miaka 50 iliyopita,bado tu hatujaweza kufanya vitu bila wao?na si mpaka leo kuna makabila yanaishi kama vile tulivyoishi kabla ya wakoloni?vipi maendeleo yao sasahivi yanazuiliwa na kina nani?au bado wakoloni wanawazuia?wapo wamang'ati,wamasai,na wengine wengi vipi maendeleo yao?
 
Mnafananisha ukoloni na kujitawala wenyewe kiasi kwamba hata wewe leo unaweza kuamua kugombea nafasi ya uongozi na ukaleta maendeleo kwa hiyo nafasi uliyonayo halafu mtu anafananisha hili na ukoloni,hao ccm tunaolalamikia na kuona.ndiyo kikwazo tukumbuke ccm watu wanatoka kwenye jamii zetu hizi hizi ndugu zetu marafiki zetu ndio hao hao na si watu kutoka sehemu zengine hata wewe leo unaweza kuwa ccm halafu et tusime hao ni sawa wakoloni?
 
Dunia ya tatu ndio yetu hii ya watu masikini.
Dunia ya pili ni vile vinchi kama India, Brazil, Nchi za mongolizi, N.k

Dunia ya kwanza ni zile nchi babalao. G8
Yes! wakatugawana na kututawala.
 
Uongo ubaguzi ndiyo unaletwa sasa na washamba
Jambo baya likifanywa na Mzungu tutalipia kelele sana lakini lifanywe mweusi mwenzetu tutajitahidi sana kuonyesha sio baya awamu ya tano umejitahidi sana kuturudisha nyuma kwa maana ukabila,upendeleo,kutugawa nk
 
[QUOTE="Dreamlinerz, ukipata muda jaribu kusoma Historia ya Bara la ulaya halafu uone haya unayosema yalitokea kwetu kama kwao hayakutokea. Hayo unayozungumzia ni mifumo tu ya maisha ambayo ni lazima itokee kwenye jamii fulani ili iweze kuendelea na hayo hayapingiki kwa sababu ni LAW OF NATURE. Sawa tulipambana wenyewe kwa wenyewe Lakini mfumo ulitaka hivyo. Ili tuingie kwenye Feudalism ni lazima tungepigana ili ukoo au kiongozi mwenye nguvu apate eneo kubwa na watu wengi ili kuunda Empire Kama alivyo fanya Askia Mohamed wa Soghai kingdom au Shaka wa Zulu land Pia mutota wa Buganda.

Mkuu tulipigana lakini mwishowe Vita hiyo vilikuwa na manufaa kwetu....Tuliunganishwa kwa Damu na machozi na tukaishia kuwa ndani ya utawala mmoja na kufanya kazi pamoja na kushirikiana....Ilibidi iwe hivyo.....Lakini angalia Mzungu alipofika ...Kwanza aliua Viwanda vyetu vya ndani na kuwakata mikono walio kaidi....Akaharibu mifumo yetu ya kibiashara kama East African na TranSaharan Trade.

Kibaya zaidi wakaaribu mfumo mzima wa Maisha yetu na kutupachika mtindo wao wa Maisha unao tutesa mpaka sasa.....Na Kama wangetuacha na mfumo wetu Maisha yaani kuanzia shughuli za kiuchumi na kiteknolojia,Kijamii na kisiasa, Nina uhakika Sasa waafrika tungekuwa tumeendelea mbali kwa njia zetu wenyewe..na tungekuwa na mfumo wetu mzuri tu wa Maisha yetu.....Kinacho tutesa sisi ni kuishi kwenye mfumo ambao hatujauunda sisi na sio kwaajiri yetu yaani sawa na Gari kupita kwenye njia ya Garimoshi

NB:Ukipata muda Soma kitabu Cha Walter Rodney kiitwacho "HOW EUROPE UNDERDEVELOP AFRICA".
 
Leo hii ma DC na RC unawapigia kura?

Halafu ninyi wa digrii 4 majanga kweli kweli.
We unajua ni utaratibu upi ulitumika ili Nyerere waziri mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana lakini kuna uchaguzi wa ngazi zote, kuanzia kijiji, mtaa, kata, ubunge hadi urais. Wakati wa mkoloni kulikuwa na uteuzi tu tena hakuna uteuzi wa ngazi ya kijiji kata au jimbo huko mtajijuwa wenyewe.
 
Hahahaha we jamaa upo mwepesi sana kichwani,kwani sasa watu hawafi na njaa?au hawauliwi na hao viongozi weusi wanao watawala?Kweli wazungu walikuwa na mabaya lakini mengi mazuri,kuliko tulio waamini sasa tukijua ni wenzetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba unipe mfano mmoja kwamba serikali ilivamia nyumba ya mtu na kubeba chakula chote cha akiba.

Kuna tofauti kubwa Kati ya njaa iliyotokana na kukosekana mvua au mazao kushidwa kukuwa, na njaa ambayo chakula chako kinanyagaywa kwa nguvu bila ridhaa yako mwenywe.
 
Back
Top Bottom