Chochote walichokifanya wakoloni, walifanya kwa manufaa yao mapana.
Hata sasa bado sie ndio soko la bidhaa zao, chanzo cha mali ghafi za viwanda vyao n.k.
Tukiwa na dunia yenye amani na utulivu, watauza wapi silaha zao ikiwa wao ndio wazalishaji wa silaha?
Walijenga reli na barabara wakati uke zirahisishe usafirishaji wa bidhaa ziende kwao, hapo bidhaa inajumuisha watumwa, mafini, mazao n.k.
Tafiti walizofanya kuhusu maeneo yenye madini na miundo mbinu nayo ilikua kwa kusudi lilelile, kuwanufaisha wao.
Kusingekua ni kwa ajili ya maslahi yao kwanini waligombania maeneo ya Afika hadi kufikia kufanya mkutano wa kugawana bara letu?
Maovu na uzembe wa viongozi wetu baada ya uhuru umekithiri kiasi cha kufanya tuwakumbuke wakoloni, lakini haiondoi ukweli kwamba mkoloni hakufanya chochote kisicho na faida kwake.
Barbarosa pole sana, mbaya zaidi umesahau kusema kuna jamaa sasa hivi ametuletea lugha ya kuwaita wazungu mabeberu huku akiendelea kuwaomba watusaidie na kuwasifia kila wanapofanya hivyo.
Wakoloni hawa kama kweli wana kusudi na nia njema, UN wapo kuhakikisha dunia inakua salama na hatuna migogoro kati ya nchi na nchi huku haki za binadam zikipewa kipaumbele, lakini hilo halijawahi kufikiwa.
Mashirika yake ya maendeleo yamekuwepo zaidi ya miaka 70 wakijinasib kusaidia nchi kupambana na umaskini, kuimarisha utawala bora, kueneza demokrasia n.k lakini hakuna nchi hata moja wanaweza kuitolea mfano kwamba waliikuta na hali mbaya, wameisaidia na sasa imefikia pazuri wanaweza kuiacha ikajiendesha yenyewe, haipo.
Nabaki na msimamo wangu kwamba mkoloni alifanya yote kwa maslahi yake binafsi.