Nani huyu asiyekumbuka matendo maovu ya Karl Peters(mkono wa chuma), biashara ya watumwa iliyochagizwa na wazungu, wizi wa mali mf: ngozi za wanyama, pembe za ndovu, madini mbalimbali, kutujengea miundo mbinu ambayo haikuwa na lengo la kimnufaisha mtu mweusi, elimu yenye ubaguzi na utabaka, kutuhubiria dini zenye kutusahaulisha asili yetu, utitiri wa kodi, ukiukwaji wa haki za mtu mweusi kama vile kuchukua ardhi kwa mabavu, kutumikisha watu bila malipo au kwa ujira kiduchu na kwa muda mrefu bila kupumzika, kuibwa kwa masalia ya mifupa yaani skeleton ya mijusi wakubwa yaani (dinosaurs), kuharibu viwanda vyetu asili vya kipindi kile ambavyo ndio ungekua msingi wa ubunifu wa leo, kutujengea viwanda vidogo visivyo na tija yaani (processing industries) siyo heavy industries, kuwafanya baadhi ya makabila kuwa vibarua wa kidumu hadi leo.
Kiujumla nakishangaa kutetea wakoloni, yaani hata kina Kinjekitile Ngwale na Mkwawa walipambana na huu udhalimu bado wewe msomi wa Leo unatetea! Dah
Wakoloni ni wabaya zaidi ya wabaya hasa kupitia matendo yao makuu matatu yaani Creation, Destruction & Preservation.
Si kwamba nawatetea waarabu la hasha! Naongelea upande wa wazungu kuanzia kwa wareno, wajerumani na waingereza. Waarabu nao wana shida zao pia