Kusherehekea siku ya kuzaliwa hali ya kuwa wananchi wanateseka na umasikini

We hater...lazima utambue kila jambo lina nafasi yake na muda wake.

Hayo ya kusimamia miradi ya kiuchumi ni majukumu ya serikali yake na wapo watendaji wa kushughulika hilo, hata birthday ni haki yake kusherehekea maana hata yeye ni binadamu kama kwako haina umuhimu hilo ni juu yake.

Kila jambo lina muda wake, umuhimu wake na wakati sahihi wa kufanya usichanganye majukumu ya lazima ya Rais (taasisi) na majukumu yake ya kila siku kama binadamu wa kawaida (ikiwemo kusherehekea birthday party).
 
Hizo nchi ulizotaja kama mifano labda utujuze na chumi zao + changamoto nyingine za uchumi kwa watu wake wa chini zikoje labda.
 
Brother P, huwa natamani sana TABIA yako ya kutojali, hata utolewapo maneno makali!
 
Queen (Monarchy) huo ni utamaduni wa Kifalme na wanaenzi culture yao...., Mtendaji ni Prime Minister, Queen ni just symbolically (Na ni hapo juzi tu Bwana Boris kaingia kwenye misukosuko kwa mambo ambayo huenda ungeweza kuyaona kwamba ni petty)

Kumuelewa mleta uzi sio kwamba mtu asisherekee, hata akiamua kusherekea mwaka mzima its okay so long as (he / she is eating matunda yake)..., ila mpaka mleta uzi kalalamika inaonekana anaona kile alichotumwa huyu mwajiliwa wetu hajakitekeleza kwahio kuonekana anakula Bata huenda ni Kejeli fulani (thus kama ningekuwa mshauri wake ningemwambia hizo Bata ale kwa siri) Yaani ajue kula na vipofu.....
 
Hizo nchi ulizotaja kama mifano labda utujuze na chumi zao + changamoto nyingine za uchumi kwa watu wake wa chini zikoje labda.
No matter how bad ones economic situation is, hakuna ubaya wowote mtu kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa with whatever s/he has, hata kama hana kitu, just a glass of water is enough. Na akiwa hana hayo maji, then hata kuambiwa tuu happy birthday is just enough.
Hata akikosa chakula anakula hewa kama wafanyavyo breatharians .
P
 
Nipo Shinyanga. Mwishoni mwa Novemba mwaka jana, nilinunua mtungi wa gesi wa kilo 30 kwa 54,000/=. Leo, nashangaa naambiwa 59,000/=.
Upandaji wa vitu, sisikii Serikali ikikemea!
Gesi ni biashara binafsi kama huwezi kununua pikia kuni.
 
Lini walikuwa matajiri? Je sherehe zilikuwa hazifanyiki? Rais ndio huwa anatafutia watu maisha mazuri?
 
Kawaida tu mkuu.....mwache afurahie hii siku muhimu kwake.....nna chojua hakuna kiongoz anayeweza kumaliza matatizo yote



Hiv legendary MAGU alikuwa anasherekea hivi vitu

Binafsi sjawahi kusikia bday yake
Manyang"au yote duniani huwa yanafanya sherehe za kunywa damu za watu na hufanya Kwa Siri sana.
 
Aseeeh! Kwani kila kitu lazima mkiseme vbaya tu
Rais ata asipokuwa na hiyo party unafikri wewe itakuongezea nini kwa mfuko wako,,majungu lawama malalamiko haya kila Siku ya nini,shida haziwezi isha kamwe ata wewe mleta Uzi upewe nchi hii...

Tufanye Kazi tu Dudes...Rais hawezi kuja kwako kukupa hela ...Au huwa mnaandika kujifurahisha Jf....
 
Hapa issue sio birthday ya mama,hapa ni kwann asherehekee Ikulu? Kumbuka Ile ni Ofisi/Ikulu ya taifa,na sio sehemu ya mtu binafsi. Pascal Mayalla Acha kujipendekeza kaka,ww kama mwandishi ni mwandishi wa waheshima Sana,unapaswa kukemea hili swala Kwa kalamu. Huu no mfano mbaya Sana Rais anaonesha,tuendako tutaanza kuwa na viongizi wanaoenda kunywa chai London na Lunch Dubai huku wananchi wakiteseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…