Kusherehekea siku ya kuzaliwa hali ya kuwa wananchi wanateseka na umasikini

Hii inaitwa roho ya kwanini, sio kitu kizuri!. Mtu amelitumikia taifa kwa siku 364, hiyo siku moja tuu ya 365 ndio inakuuma?.

Tena sisi Tanzania tuna bahati, siku ya birthday ya mkuu wa nchi ni siku ya kawaida...
Sasa mwenzio mtawala wa dunia na hela anazo yeye utajilinganishaje
 
PM wa UK sio head of state. President of URT is the head of state.
Hakuna ubaya wowote rais kusherekea siku yake ya kuzaliwa. Kama ingefanyika dhifa ya kitaifa Ikulu, kusherekea birthday ya rais, hapo ndio labda angekuwa na hoja.
P
Kaka yote iyo choyo tu
 
Wakuu nina mengi moyoni ila hasira zimenikaba kwenye koo mpaka nashindwa kuendelea. Naomba niishie hapa kwa Leo .
Bwashee, kimbia haraka ukajinyonge kabla hujapasuka. Kama birthday party binafsi inakuuma kiasi cha kutaka kufa, ni afadhali tupunguze watu wenye akili za kiuwendawazimu kama nyie.
 
Wakuu nisipende kuwachosha
Ila inasikitisha sana kuona ikulu ambapo Nyerere aliwahi kusema kuwa ni mahala patakatifu imebadilika na kuwa pango la walanguzi...
Yeye anafanya kazi ya ku- print pesa siyo?Unataka aje akutupie pesa mlangoni kwako? Nenda fanya kazi hata kulima utapata pesa!
 
Hizo ni tabia za KICHACHAWA na tabia za nyinyi CHAWA ni kuwahadaa maboss wenu kuwa mnawapenda kwa kuwaandalia sherehe kama hizi!!!
Mkuu Bulesi, nimesema wazi kabisa kuwa sherehe za birthday ni sherehe za kizungu sisi watu wa bushi tulikuwa hatuzifanyi, lakini sasa kutokana na maendeleo nasi sasa tunazifanya. Kumfanyia bosi, wife, wazazi, watoto a surprise party, ni ishara ya upendo na sio uchawa, ila pia naomba kukiri, the dividing line between upendo wa dhati na uchawa is very thin, kama ilivyo mwanaume kumtokea demu bomba mwenye sura nzuri na bonge la shape na kumwambia "I love You," kuwa unampenda na umemzimikia kwake umekufa umeoza, the dividing line between hiyo I love you yako yako kama ni love kweli na umempenda kwa dhati au ni lust tuu unamtamani umduu tuu, is very thin, with naked eyes you just can't tell, ila sisi wa jicho la tatu can!. Najitolea mfano mimi mwenyewe, ikitokea nikamsifia Samia kwa lolote very genuine, halafu ukaniita chawa utakuwa ni unanionea kwasababu kumsifu sikuanza leo!.

Angalia tarehe za mabandiko haya...
Hivyo kwa mtu kama mimi kumtakia Rais Samia Happy Birthday, ni bonafide Happy Birthday na sio uchawa!.
Happy Birthday Rais Mama Samia!.
Paskali.
 
Hii inaitwa roho ya kwanini, sio kitu kizuri!. Mtu amelitumikia taifa kwa siku 364, hiyo siku moja tuu ya 365 ndio inakuuma?...
Umesahau The Netherlands siku ya kuzaliwa ya king kila bidhaa ina uzwa bei chini na free day nenda haraka nunua unacho taka, tena tuna amka mapema sana kuwahi soko. Na ishi hapa miaka 25 sasa ni mtanzania mke Mholanzi watoto mchanganyiko.
 
Umesahau The Netherlands siku ya kuzaliwa ya king kila bidhaa ina uzwa bei chini na free day nenda haraka nunua unacho taka, tena tuna amka mapema sana kuwahi soko. Na ishi hapa miaka 25 sasa ni mtanzania mke Mholanzi watoto mchanganyiko.
Mkuu tilburg1 kwanza asante kujitokeza, na hongera to mix blood maana... Brain ya point five is something else, namuona Maria Sarungi anavyosaidia taifa. Nyinyi Watanzania wenzetu wenye bahati ya kupata exposure kwenye nchi za wenzetu, mnawajibu wa kuileta experience yenu kulidaidia taifa letu kwa kuishauri nchi yetu I copy some good practices za wenzetu, na mfano nzuri ni huu ili kutuondoa ushamba sisi Watanzania, tena makao makuu ya Tanzania Diaspora yako hapo Uholanzi, Diaspora wetu wengi wamefanyiwa brain drain mkitumika ughaibuni, sio lazima mrudi nyumbani maana hii dhiki hamtaiweza but bring back the brain, through exposure yenu mlidaidie taifa.
P
 
mmh!!! najua JNHP inaendelea kujengwa, SGR inaendelea na majuzi tu mh.rais kasaini mkataba wa SGR PHASE3,DARAJA KIGONGO BUSISI linaendelea, kasaini mkataba wa TEMBO NICKLE fursa mbalimbali zipo pale zikiwemo ajira kibao, madarasa yamejengwa,zahanati zimejengwa, mishahara ya wafanyakazi sekta ya umma inalipwa kama kawaida n.k. NINI kimekwama?!!!??!!. naomba wewe binafsi utoe takwimu yako hapa umeifanyia nini TANZANIA!!??!!
 
HAIHUSIANI KWA LOLOTE!!!!
Mleta mada huwa husherehekei siku yako ya kuzaliwa kwakuwa jirani zako hawajavaa nguo mpya na hawajala wali mwaka mzima????
 
Nipo Shinyanga. Mwishoni mwa Novemba mwaka jana, nilinunua mtungi wa gesi wa kilo 30 kwa 54,000/=. Leo, nashangaa naambiwa 59,000/=.
Upandaji wa vitu, sisikii Serikali ikikemea!
Njoo Iringa ni sh. 38,000/= complete.
 

Ni haki yake kusherehekea siku yake, ila pia lazima akutane na mawazo kinzani kulingana na hali ya watu wa chini waliyo nayo,
Huku kitaa hali ya kifedha ni mbaya sana, watu wanakatika mitaji kwa kukosa wateja na ghalamaza vitu zilivyo juu na faida kidogo kwa sasa huku matumizi yakipanda juu.
Kwa hiyo mtu wa aina hiyo akiona mkuu anafanya party inamhuzunisha sana.

Jambo dogo linaweza kuzua jambo kama ilivyotokea kwa Borris Johnson nadhani aliona ni jambo la kawaida tu lakini kwa ssa linamtoa jasho.

Raisi anatakiwa kufurahi baada ya kuona watu wa china nao wana furaha, tofauti na watu wa kipato cha juu ambao hawaathiriki kama hawa wa chini na istoshe bado ana msiba wa mtangulizi wake,
Ni furaha gani hiyo anayo hadi asisubili mwaka ushe afanye mwaka wa pili?
Au kuna fulaha yenye maslahi?
 
Nipo Shinyanga. Mwishoni mwa Novemba mwaka jana, nilinunua mtungi wa gesi wa kilo 30 kwa 54,000/=. Leo, nashangaa naambiwa 59,000/=.
Upandaji wa vitu, sisikii Serikali ikikemea!
Dawa ya meno ile ya 1200 saivi inauzwa 1500, vifaa vya ujenzi ndio havishikiki mkuu. Yule bibi anaongea anarembua macho eti ' nafungua nchi'.
 
Mwafrika na nongwa zake zinazomjazia umaskini kila kukicha. Sherehe ya kuzaliwa ni siku moja tu, leo hii imeshakuwa historia.

Asiifurahie eti kisa shule zinataka kubomoka!!. Ungejua kuwa SSH ameweza kusafiri kuonana na mabeberu ili kupata pesa za kukarabati shule usingeandika huu upuuzi.

Ungejua kuna fedha za uviko19 zinazotumika huko kwenye halmashauri zote nchini, usingekuja na habari ya malalamiko kama hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…