Kusherehekea siku ya kuzaliwa hali ya kuwa wananchi wanateseka na umasikini


Tena hii hata sio ya Rais ni mke wa Rais. Tuache ushamba jamani. Hao wananchi unaosema hawafanyi sherehe za birthday, harusi na kipaimara? Tena unakuta nacheza ngoma.
 
Nakubaliana na wewe kwamba hiki ni kitu kidogo.
Lakini nafikiri angetumia siku hii kufanya jambo moja unique kwa ajili ya Taifa ukiacha routine zake.
Lakini nikuambie usijaribu kujilinganisha na wazungu hata wakifanya hiyo siku ni public holiday wana haki.
Acha kulinganisha usingizi na kifo.
 
Siku mkiniambia siku ya kuzaliwa ya Boris Johnson ni Sikukuu ya kitaifa nitaanza kuwaamini. Au mkisema baada ya Mama Samia kuwa Chifu basi ana hadhi ya Kifalme.
 
Yule bibi anaongea anarembua macho eti ' nafungua nchi'.
Kwanza kitaifa jina lake ni Mama na sio Bibi, pili ukome kusema anaongea huku anarembua macho!, ukweli ni kuwa, harembui macho, bali hivyo ndio macho yake yalivyo, yaliumbwa hivyo hivyo marembo na Mungu mwenyewe, hivyo yanaonekana kama yameregea...lakini yanaona hayo!.
And by the way, kuna watu ni wagonjwa wa macho, wao wanayependa hivyo hivyo yalivyo!
P
 
Kawaida tu mkuu.....mwache afurahie hii siku muhimu kwake.....nna chojua hakuna kiongoz anayeweza kumaliza matatizo yote

Hiv legendary MAGU alikuwa anasherekea hivi vitu

Binafsi sjawahi kusikia bday yake

 
Mkuu Paschal nikiri wazi uwezo wako wa kufikiri umeshuka sn kama siyo kuisha, hivi wewe unajilinganisha na Uingereza na mataifa mengine makubwa serious? wanashinda ya barabara, madawati, madarasa, nyumba za tembe, maji, huduma za afya, mishahara ya watumishi kutopandishwa miaka 7, mifugo kufa na ukame kwa kukosa maji n.k? ndiyo maana siku hizi unadharaulika sn na vijana wanakutukana
 
Ukiwa na waandishi wajinga kama hawa nchi kupata maendeleo ni ndoto za mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…