Kushindwa kubeba ujauzito na kukosa hedhi kwa muda mrefu

Maulid mussa15

New Member
Joined
Aug 1, 2017
Posts
3
Reaction score
1
Habari zenu wadau,

Naomba kushea hii kitu, kuna mtu nimekutana naye ana shida ya uzazi lakini mwanzo aliweza kubeba ujauzito na kujifungua mtoto mmoja. Baada ya hapo hakuweza tena kubeba ujauzito wala kupata hedhi kwa muda wa miaka 4 hadi sasa.

Mwenza wake alijuzwa na madaktari kuwa mkewe hatoweza kubeba ujauzito na baada ya muda ndoa ikavunjika, lakini muhusika akajaribu kwenda kupima kwenye moja ya hospital aliambiwa uwezo wa kubeba ujauzito anao.

Shida aliyonayo ni kubeba ujauzito, hapati hedhi na huwa anapata maumivu ya tumbo mara kwa mara. Je, hilo tatizo linaweza tibika?
 
Kama hapati hedhi inamaana mayai yake hayapevuki na amepata pcos (vimbe ndogo kwenye kizazi) au ana homoni nyingi ya kiume ya testorene,kama anapata ndevu hii ni dalili moja wapo.
ndio anaweza kuzaa ,kama anahitaji mtoto kuna dawa zipo za kutumia ili mayai yapevuke ,wanapewa kwanza dawa ya kuleta period inaitwa duphaston alaf wakiona ndio wanatumia hizo zingine za kupevusha mayai,namshauri akaonane na mtaalam wa afya ya wanawake.

Pia zipo supplements za kutibu hil hali.
 
Habari zenu wadau,

Naomba kushea hii kitu, kuna mtu nimekutana naye ana shida ya uzazi lakini mwanzo aliweza kubeba ujauzito na kujifungua mtoto mmoja. Baada ya hapo hakuweza tena kubeba ujauzito wala kupata hedhi kwa muda wa miaka 4 hadi sasa.

Mwenza wake alijuzwa na madaktari kuwa mkewe hatoweza kubeba ujauzito na baada ya muda ndoa ikavunjika, lakini muhusika akajaribu kwenda kupima kwenye moja ya hospital aliambiwa uwezo wa kubeba ujauzito anao.

Shida aliyonayo ni kubeba ujauzito, hapati hedhi na huwa anapata maumivu ya tumbo mara kwa mara. Je, hilo tatizo linaweza tibika?
Kuna gonjwa linamtafna kwenye kizazi kama alikuwa danga haya ndo malipo yake kama sio danga bas ni tatizo tu limempata
 
Back
Top Bottom