Uchaguzi 2020 Kushindwa kwa maandamano ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ni ushahidi wa wazi kuwa ushindi wa CCM hauna dosari zozote

Uchaguzi 2020 Kushindwa kwa maandamano ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ni ushahidi wa wazi kuwa ushindi wa CCM hauna dosari zozote

Wameweka Polisi kila mahali na baadhi ya maeneo hadi wanajeshi , lakini ninachoona haya maendeleo hayana kikomo hivyo siku yeyote yanaweza kuibuka ......sio busara sana kukebehi kuwa hawakutokea wakati viongozi karibu wote wakuu wamekamatwa ...na baadhi ya waliogombea ubunge
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Watu hawashiriki kwenye maandamano kwa kushawishiwa. Maandamano ni utashi wa mtu na hushiriki tu kwa kuwa ameguswa. Maandamano ya kushawishiwa kwenye mikutano na waandishi wa habari ama kwenye mitandao ya kijamii siku zote hayafanikiwi.

Wananchi wakiguswa hata utumie vifaru huwezi kuwanyamazisha. Maandamano ya CHADEMA na ACT Wazalendo hayakuwa na hisia za wananchi bali yaliitishwa na watu waliokosa ulaji kupitia sanduku la kura.

Wananchi wanajua wazi kuwa Ushindi wa CCM ni wa halali hivyo wameamua kuwapuuza waandaaji wa maandamano hayo. Maandamano ya CHADEMA na ACT Wazalendo hayakuwa na hisia za wananchi bali yalisukumwa na genge la watu lililokuwa linapigania maslahi binafsi.

Hivyo tunahitimisha kuwa Ushindi wa CCM ni halali kabisa na wananchi wameamua kuwaadhibu CHADEMA na ACT Wazalendo kupitia sanduku la kura na kupitia maandamano feki.

Hongereni sana Waheshimiwa Wananchi. Ninyi ni zaidi ya Wale Wajumbe wa CCM. Mmetuheshimisha Watanzania. Mmewatia adabu CHADEMA na ACT Wazalendo kupitia sanduku la kura na kukataa maandamano yao
Maandamano yasio na KIKOMO na ya amani ujua maana yke mkuu kwani barabarani watu hawatembei je unajua siri ya Kila mmoja moyoni mwake ,hata mfanyakazi wa ofisin kwako anaandamana akuleteapo mafaili , hili neno pana Sana mpaka pale litakapotenguliwa na waliolitoa mkuu
 
Tatizo siyo maandamo ya amani kuwepo au kutokuwepo...

Issue ni nguvu ambayo ingetumika kuyazuia maandamo kutoka kwenye kuwa ya amani kwenda kwenye kua ya machafuko...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom