Kushiriki usafi Jumamosi ya kwanza ya mwezi ni lazima kisheria?

africansongs

Member
Joined
Jan 5, 2018
Posts
83
Reaction score
225
Hivi jamani wadau huu usafi wa jumamosi umekuwaje? Ni kila jumamosi ama?
Leo naelekea kazini nasimamishwa kwanini huendi kwenye usafi na kweli watu wengi walikuwa wanafyeka.

Nikazozana nao kidogo ndo wakaniachia maana niliwaambia nina funguo za ofisi hivyo nitawaweka watu nje muda mrefu.

Hivi hizi sheria huwa zinapitishwa na chombo gani au mkuu wa wilaya au mkoa akijiskia tu basi anatoa tamko.

Hivi kodi zetu zinafanya nini? Asubuhi kweli nikafyeke? Sasa shule nilienda kufanya nini? Hizo kodi zetu kwanini zisilipie watu watakaofanya kazi hizo tena sasa hivi ni kila wiki.
 
Makonda alikurupuka na hili tamko kwa hofu ya ukuta,Leo hii ni mradi wa watu kuchukulia rushwa.
Nilifanya tafiti hamna usafi unafanyika zaidi ya watu kuchelewa kufungua biashara na ofisi kujiingizia kipato
 
Hilo Tamko Ni la Uchochezi Kuingilia Uhuru Wa Kuabudu Wa Dhehebu la Wasabato na wengine Siku hii Kwa Wengine Ni Siku ya Kurelax Na Familia zao

Mfano Sisi wa Siku Jumapili Ingekuwa Kila Jumapili ya Mwisho wa Mwezi Ni ya Kufanya Usafi Au IJUMAA ya Mwisho wa Mwezi Kwa Ndugu Zetu waislamu ingependeza Na Ingekuwa Mwisho wa Hilo Tamko
 
Acha kulalamika bhana, kwani ukifanya huo usafi kama wenzako ulowakuta wanafyeka unapungukiwa nini
 
Naona mods wamebadirisha heading ya uzi. Si jumamosi ya kwanza, sasa ni kila jumamosi na kuna sungu sungu kabisa na majina yanarrkodiwa.
Hivi sheria si zinatungwa na bunge au hamna bunge siku hizi. Sheria hutokana na matamko, haya mambo ni uonevu wa hali ya juu.
Kodi tulipe bado tena tulazimishwe kufanya usafi, sometimes kufyeka vichaka, nikiumia au kung'atwa na nyoka, inakuwaje?
Hii nchi kwakweli inapoelekea si kuzuri.
 
Acha kulalamika bhana, kwani ukifanya huo usafi kama wenzako ulowakuta wanafyeka unapungukiwa nini
Hiyo sheria imepitishwa lini na bunge? Kuna watu tunafanya kazi jumamosi na wengine ni siku ya kurelax, kodi wanatoza na kazi tulazimishwe, ni uonevu wa hali ya juu.
Kwanini kodi zetu zisitumikekuajiri watu na iwe kazi yao hiyo, yaani niache shughuli zangu eti usafi. Haya matamko haya ni uonevu wa hali ya juu.
 
Hili jambo la usafi kila jmosi linaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa...maduka yote yanafungwa mpaka saa nne ....bado serikali inataka kodi haraka....wananchi wamewekeza ili wapate returns tena jmosi ndio siku nzuri coz familia nyingi ziko pamoja kwa ajili ya chai...mikate wala maandazi wala.maini huwezi kupata mpaka saa 4.
Usafi ufanyike jmosi moja kwa mwezi...period
 
Hiyo sheria imepitishwa lini na bunge? Kuna watu tunafanya kazi jumamosi na wengine ni siku ya kurelax, kodi wanatoza na kazi tulazimishwe, ni uonevu wa hali ya juu.
Kwanini kodi zetu zisitumikekuajiri watu na iwe kazi yao hiyo, yaani niache shughuli zangu eti usafi. Haya matamko haya ni uonevu wa hali ya juu.
We unadhani sheria zote lazima zipitishwe na Bunge! Pitia kidogo hata google uone 'Sources of Laws in Tanzania' utaelewa kidogo. Narudia tena acha kulalamika lalamika hovyo
 
Ccm ni shida sana. Yaani kukombatia ujinga tu
 
Hiyo sheria imepitishwa lini na bunge? Kuna watu tunafanya kazi jumamosi na wengine ni siku ya kurelax, kodi wanatoza na kazi tulazimishwe, ni uonevu wa hali ya juu.
Kwanini kodi zetu zisitumikekuajiri watu na iwe kazi yao hiyo, yaani niache shughuli zangu eti usafi. Haya matamko haya ni uonevu wa hali ya juu.
sio sheria zote zinatungwa na bunge kuna By laws zinazotungwa na serikali za mitaa.
 
Makonda alikurupuka na hili tamko kwa hofu ya ukuta,Leo hii ni mradi wa watu kuchukulia rushwa.
Nilifanya tafiti hamna usafi unafanyika zaidi ya watu kuchelewa kufungua biashara na ofisi kujiingizia kipato
Hii ni GN no.139 of 2016 iliyotolewa na waziri ofisi ya makamu wa rais mazingira na muungano kuifanya kila jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya usafi sasa sijajua Makonda kaingiaje katiak mjadala huu ??
 
Hilo Tamko Ni la Uchochezi Kuingilia Uhuru Wa Kuabudu Wa Dhehebu la Wasabato na wengine Siku hii Kwa Wengine Ni Siku ya Kurelax Na Familia zao

Mfano Sisi wa Siku Jumapili Ingekuwa Kila Jumapili ya Mwisho wa Mwezi Ni ya Kufanya Usafi Au IJUMAA ya Mwisho wa Mwezi Kwa Ndugu Zetu waislamu ingependeza Na Ingekuwa Mwisho wa Hilo Tamko
Kama kuna infringment ya haki zako unaruhusiwa kwenda kuichallenge hii sheria kama ambazo alifanya Ezekiah Oluoch katika kesi yake dhidi ya Waziri wa mazingira kuhusu siku hii ambapo alishinda kesi.
 
Hivi jamani wadau huu usafi wa jumamosi umekuwaje? Ni kila jumamosi ama?
Leo naelekea kazini nasimamishwa kwanini huendi kwenye usafi na kweli watu wengi walikuwa wanafyeka.

Nikazozana nao kidogo ndo wakaniachia maana niliwaambia nina funguo za ofisi hivyo nitawaweka watu nje muda mrefu.

Hivi hizi sheria huwa zinapitishwa na chombo gani au mkuu wa wilaya au mkoa akijiskia tu basi anatoa tamko.

Hivi kodi zetu zinafanya nini? Asubuhi kweli nikafyeke? Sasa shule nilienda kufanya nini? Hizo kodi zetu kwanini zisilipie watu watakaofanya kazi hizo tena sasa hivi ni kila wiki.
The Environmental Management (Designation of National Cleanliness Day) Guidelines, 2016, G.N. No. 139 of 2016 exerts an irresistible dint upon you to occasion the required.

Kwa hiyo fanya usafi mkuu usije ukatenguliwa kiuno wakakuambia ulikiuka amri halali ya mamlaka.
 
huku kwetu ni jumamosi ya mwisho ya mwisho wa mwezi, inakuwa balaa na watendaji wa mitaa faini njenje
 
Hiyo sheria imepitishwa lini na bunge? Kuna watu tunafanya kazi jumamosi na wengine ni siku ya kurelax, kodi wanatoza na kazi tulazimishwe, ni uonevu wa hali ya juu.
Kwanini kodi zetu zisitumikekuajiri watu na iwe kazi yao hiyo, yaani niache shughuli zangu eti usafi. Haya matamko haya ni uonevu wa hali ya juu.
Kuna baadhi ya sheria zinafanya kazi baada ya sheria za bunge kutoa mamlaka kwa chombo/taasisi/kiongozi kutunga/kupitisha kanuni/taratibu/sheria/amri ambazo lazima ziwe ndani ya mamlaka waliyopewa na sheria hizo za bunge ..

Hivyo huyo mkuu wa mkoa/halmashauri wanaweza wakatoa amri ya watu kufanya usafi ambayo ipo chini ya mamlaka yao kisheria mkuu.

Sio kila agizo au amri utakayoisikia mpaka bunge likae, maagizo mengine yanatokana na nguvu walizopewa hao maRC na sheria kwa hiyo ni suala kujiuliza je maagizo hayo wanayotoa yapo kwenye mipaka ys nguvu walizopewa kisheria?
 
Kasome Case ya Ezekiah olouch v. Vice presidentoffice and enviroment & A.G
 
Acha kulalamika bhana, kwani ukifanya huo usafi kama wenzako ulowakuta wanafyeka unapungukiwa nini
Kila mtu afanye usafi kwa wakati wake bwana kwani serikali imekupangia muda wa kuoga?

Siyo kusupport kila jambo la viongozi wanaloleta au kuanzisha.
 
Back
Top Bottom