Kushuka kwa kiwango cha elimu tanzania

Kushuka kwa kiwango cha elimu tanzania

karani

New Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Elimu ya Tanzania haimwezeshi mwanafunzi kuweza kujitegemea bali ni ya kukaririsha zaidi. Serikali iwaandae na kuwaendeleza walimu kupitia Mpango wa Mafunzo Kazini ili kuinua kiwango cha Elimu nchini.
 
Nini kifanyike? Lawama pekee haitoshi. Changia lau kidogo kuliko kujaza lawama kapu.
 
Tatizo kubwa ni mfumo wa elimu na miundo mbinu suni. Umenikumbusha lile tangazo mwalimu anafundisha, kipisi cha chaki kinaanguka. Hana kingine, nahisi wanafunzi wamekaa sakafuni hadi mbele ya darasa, na inabidi wanafunzi wa-imagine the rest of the lecture. Kweli ukitoka hapo utakuwa una lolote la kuchangia kwenye labour market? Ukikutana na graduate ni aibuuuu, hajui lugha wala content ya somo lake. Hata kama waalimu wakiendelezwa bila kubadili mfumo wa elimu kuwa competency based, bado tutakuwa pale pale.
 
mitaala ibadilishwe, mifumo ya mitihani iwe ile ya kujieleza zaidi, ufaulu yaani maksi zipandishwe mpaka 80%, uteuzi uwe wa haki na kweli, walimu pia waboreshwe na tuheshimu na kusaidia watoto wenye vipaji.
 
Kuna baadhi ya shule (chache mno) zinaivisha wanafunzi wake vizuri sana, kielimu na kimaadili. Warekebisha mambo waangalie kinachofanyika kwenye shule hizo ili yaliyo mema wayasambaze kwenye shule zote. Najua kunahitajika resources - lakini hakuwezi kuwa na elimu nzuri bila kuigharimia.
 
Nini kifanyike? Lawama pekee haitoshi. Changia lau kidogo kuliko kujaza lawama kapu.


Father mbona umekuwa mkali leo.

Taifa linawataalamu wengi

Taifa linaraslimali za kutosha

Taifa lina watu wakutosha

Kinachokosekana ni usimamizi mzuri wa raslimali zetu kuka kwa wanasiasa, tuliowapa jukumu la kukaa, kupanga, kukusanya, kuzigawa na kuzisimamia raslimali hizi wamepoteza kumbukumbu na vichwa vyao vimeishiwa ubunifu.

Hatakama tutatoa mapendekezo je serikali itayasikiliza maana hata wataalamu hawafui dafu mbele ya ccm? mbona kila siku bungeni wanaacha mambo ya msingi kujadili wanajadili simple issues.

Tatizo ni serikali mbovu kuwa naviongozi wabovu walokalia kuiba wala hawatambui vipaumbele katika taifa lolote ni Elimu, afya na manufacturing.

kama serikali na chama tawala wamelala sisi raia tufanyaJe? maana ya Misri na Tunisia hatuyawezi japokuwa hayawi hayawi mwishowe hutoke.
 
Tunalilia mifumo, viongozi na kila siku ngonjera ni hizihizi......nani wa kufanya km watendaji hawataki kusimia? Leo hii nikiuliza ni nini tafsiri halisi ya neno ELIMU BORA utajibu nini? Je, wewe binafsi umepata elimu bora?
 
Tunalilia mifumo, viongozi na kila siku ngonjera ni hizihizi......nani wa kufanya km watendaji hawataki kusimia? Leo hii nikiuliza ni nini tafsiri halisi ya neno ELIMU BORA utajibu nini? Je, wewe binafsi umepata elimu bora?


Mkuu umeongea nini hebu weka sawa, wewe hujui elimu bora nini?

Kujuwa kitu bora nilazima uwe na uwezo wa kukimiliki?

Kama mfumo bovu sijakuelewa nini kifanyike? au unamaanisha nini?
 
mitaala ibadilishwe, mifumo ya mitihani iwe ile ya kujieleza zaidi, ufaulu yaani maksi zipandishwe mpaka 80%, uteuzi uwe wa haki na kweli, walimu pia waboreshwe na tuheshimu na kusaidia watoto wenye vipaji.

na tusichukue waliofeli kwenda ualimu!
 
Hivi tunaposema kiwango cha elimu ya Tanzania kimeshuka tunalinganisha na ya wapi? Tunakutana kwenye conferences za kitaaluma na wanataaluma kutoka sehemu mbalimbali za Africa na bado mahali pengi wasomi wa Tanzania wanaonekana kuwa ni tishio despite kiingereza chao kibovu. Sasa tunasema kiwango kimeshuka kivipi?

Labda ninachoweza kusema ni kwamba Tanzania tuna tatizo kubwa la lugha. Hilo kwa kweli ni eneo ambalo inatakiwa ifanyike kazi ya ziada kuwawezesha watoto wetu waweza kuongea kiingereza vizuri mara tu wanapomaliza elimu ya msingi. Kuna nchi mbalimbali ambazo zinafundisha kiingereza kama somo, lakini mtoto akimaliza shule ya msingi anaongea kiingereza kizuri sana, lakini huku kwetu imekuwa ngumu sana.

Lakini tukija kwenye uwezo wa jumla ya kitaaluma Tanzania hailinganishwi na yeyote Africa masharika na kati. Sijajua kwa nchi nyingine kama Africa kaskazini, magharibi na kusini.
 
Hiki ndicho nilichotaka niliposema watu wasilaumu tu bali kutoa mchango. Mchango wako naukubali mwanangu.
Father mbona umekuwa mkali leo.

Taifa linawataalamu wengi

Taifa linaraslimali za kutosha

Taifa lina watu wakutosha

Kinachokosekana ni usimamizi mzuri wa raslimali zetu kuka kwa wanasiasa, tuliowapa jukumu la kukaa, kupanga, kukusanya, kuzigawa na kuzisimamia raslimali hizi wamepoteza kumbukumbu na vichwa vyao vimeishiwa ubunifu.

Hatakama tutatoa mapendekezo je serikali itayasikiliza maana hata wataalamu hawafui dafu mbele ya ccm? mbona kila siku bungeni wanaacha mambo ya msingi kujadili wanajadili simple issues.

Tatizo ni serikali mbovu kuwa naviongozi wabovu walokalia kuiba wala hawatambui vipaumbele katika taifa lolote ni Elimu, afya na manufacturing.

kama serikali na chama tawala wamelala sisi raia tufanyaJe? maana ya Misri na Tunisia hatuyawezi japokuwa hayawi hayawi mwishowe hutoke.
 
Hili umenena vema hasa.

Githeri tunashida ndugu yagu bora umeliona hilo ccm hawalioni

Hao jamaa huko juu hawana la kuboresha katika elimu, ilikuwa na walimu bora, vifaa na mazingira bora ya elimu

Wanauchungu gani? iwapo fedha ya ufisadi inawasomesha watoto wao shule za viwango kama Fedha, Soni, Kifungiro nk ada ipo juu.

Lengo kubwa lakuwa na elimu duni na kupigia upatu shule za kata ni kuendeleza ya wakoloni, watoto wa wakulima kubakia wapiga kura siku zote kuwachaguwa akina kawawa, makamba, kikwete, mkapa, mwinyi, akina mnauye,kingunge ilikuendeleza utawala wa kifalme.

Haaingii akilini watu kupuuza elimu, unamchukuwa form four Div iv akafundeshe!!!! pumbaf, anafundisha nini huyu hata what is

chemistry hajuwi? wala ya mwenemutapa kindom na akina zwangendaba au mfekane war hajui?????? Utaona waziri anaongea na

kusifia ujinga bungeni, huwa natamani kulia kwa jinsi elimu inavokuwa mishandled.

Tunasema education is a key for success how? kwa hawa failure teachers????? na sio kwamba hawana akili lakini walipata

elimu ovyo kwa misingi hii hii ya kisiasa. The reason behind our poverty - poor education cannot be a key for success.
 
Unaongozwa na rais mwenye ufaulu mdogo afu utegemee elemu iwe juu thubutuu
 
Kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika kuimarisha elimu Tanzania.

Kwanza ni kuimairisha nidhamu ya walimu na wanafunzi. Wanafunzi wamekosa nidhamu hadi wanawabaka walimu wao. Hili sijalisikia katika nchi nyingine lakini kwa Tanzania limesikika mara mbili mwaka huu - Bagamoyo na Ruaruke huko Rufiji. Wamasai nao waliamua kuwachapa viboko walimu. Zamani mwalimu alikuwa ni mtu wa kuheshimika sana katika jamii, lakini si leo.

Walimu wengi pia wameamua kunywa au kufanya biashara wakati wa kazi. Hawajali tena kufanya kazi waliyoiomba wao wenyewe bila kulazimishwa.

Serikali ni lazima ihakikishe kuwa inawapandisha vyeo walimu kwa kuzingatia uwezo wao katika kufundisha masomo fulani katika ngazi fulani na siyo miaka aliyofundisha. Serikali kwa mfano ingeweza kujenga vyuo maalumu vya kutahini walimu wanaotaka kupanda vyeo. Hawa wangeweza kuwekwa huko kwa miezi mitatu halafu wapewe mtihani wa masomo wanayofundisha. Wanaofaulu wapandishwe daraja na wanaoshindwa wabaki palepale. Mwalimu asifundishe somo ambalo ameshindwa katika ngazi ile. Katika nchi kama Botswana kwa sasa wameamua kuwa walimu wote wa sekondari ni lazima wawe na degree. Kwa shule za msingi walimu lazima wawe na degree au Diploma.

Tatizo la wanafunzi kukaa chini mimi naona kwa kiasi fulani linachangiwa na utamaduni wa mahali shule ilipo. Kijijini kwetu hatukai chini majumbani kwetu kwa sabau ya ubaridi na vumbi jingi. Kwa hiyo ni rahisi kwa wananchi kuona ni umuhimu wa kuweka madawati shuleni. Shule zetu zina madawati mengi sana kuliko mahitaji!
 
Kinachotakiwa kifanyike, ni kubadilisha kabisa mfumo wa elimu, kuanzia kwenye utawala, mitaala na uwezeshwaji kimaslahi na mazingira. Mfumo wenyewe bado haumkomboi (bado ni wa kikoloni) mtanzania ili aweze kujitegemea bali unamfanya awe na mawazo ya kitumwa ya kuajiliwa (white colar job) na sio kujiajiri mwenyewe, hapa tatizo ni watawala waliong'ang'ania mfumo huu bila kujali unatupeleka wapi; Pia wanajinufaisha kipesa kwa kula dili na wauzaji wa vifaa, vitabu na wafadhili wa elimu; utunzi wa mitihani unaoendana na vitabu fulani vya watu fulani: nini kifanyike kutokana na hili, ni kufanya mabadiliko ya kiutawala hasa uliopo madarakani kwani utendaji wake ni wa kisiasa zaidi kuliko maslahi ya taifa, 2015 chagua viongozi wenye kulitakia mema taifa hili katika maendeleo ya elimu, Kwa sasa unatakiwa kutoa maoni yako ya katiba juu ya suala la uangalizi na usimamizi wa Elimu pamoja na kuwawajibisha viongozi husika pale wanapoenda ndivyo sivyo. Sisi watanzania twende kwa mipango, baada ya hapo ndio tunaweza kushughulikia maslahi na mazingira bora ya shughuli nzima ya uendeshaji wa Elimu.
 
Back
Top Bottom