Kushuka kwa thamani ya shilingi, zigo lililomshinda Mwigulu kulielezea kiuchumi

Kushuka kwa thamani ya shilingi, zigo lililomshinda Mwigulu kulielezea kiuchumi

Jidu,
Tanzania ni shamba la bibi, mimi nishakaa na mkuu mmoja nikamwambia kuhusu jinsi uchumi unavyoharibiwa na hawa watu uliowataja, lakini nilichoshangaa hawa waliopewa madaraka kuongoza nchi hasa Bank Kuu na Wizara ya fedha including taasisi nyingi za fedha na biashara ni kama vile hawajui lolote kuhusu uchumi na wengi wamesomea uchumi. Kwanza unamuuliza waziri hizi mashine za bahati ambazo zipo hadi kijijini kwa nini zinaruhusiwa? Jibu lao anakwambia ati zinapunguza unemployment; unamuuliza hebu aelezee madhara yake yeye hajui. Kwanza zile mashine anayepata siyo mwananchi yaani hizo machine zinakusanya pesa kutoka kwa wananchi, yaani wanazoa pesa, wanakusanya hizi pesa wanaenda Dar na makao makuu ya mikoa wananunua dollar wanapelela kwao. Waziri anabisha hadi ishipa ya shingo inamtoka kama vile yeye anatumikia hao wezi.

Laana nyingine ya nchi yetu kwa hawa watawala, kila kazi sasa hivi anapata Mchina au muarabu; na wahindi, kwa sababu hawa wanakubali kutoa rushwa na kupandisha gharama za miradi. Na hawa wakuu waipewa cha juu nafikiri hata mkuu kule juu anapata direct au indirect; unashangaa kampuni inajenga barabara inapata faida ya equivalent ya dollar 62 million kama faida, sasa hizo barabara zina gharama ya bei ya chini kulinganisha na hiyo faida. Hizo kampanu haziweki pesa Tanzania pesa, wana network zote kwenye casinos, bank kuu, bank za biashara hata black market kununua hizo dollar; sasa hizo dollar mtatunza wapi? Wamekuja kukusanya na watendaji wetu wanawaangalia tu.
Ni kweli, waziri wa fedha ni mmoja wa watu wabaopwaya katika nafasi yake. Ni kama mtu wa bora liende.
Suala hili la fedha yetu kuporomoka ndani ya hasa mwaka huu mmoja lazima aweze kujibu kwa nini linatokea na jinsi ya kuchukua hatua kudhibiti tatizo holi!
 
Kwa mujibu wa Dokta mwenyewe, uchumi wetu unakua vizuri, na nchi yetu deni la taifa linahimilika, na bado tunakopesheka.😂😂😂
Hilo neno “tunakopesheka” nalichukia Sana Kila linapotajwa…sijui ni Kwa nini …
Ila likitajwa tu, hata hamu ya chakula basi…
 
Nchi ina rasilimali zote za kutengeneza pesa bila kua omba omba Mungu katupatia, lakini walivyo kua hawana akili timamu wanaziacha nyuma Kila siku kiguu na njia kuomba misaada na kukopa alafu wanagawa na kuweka rehani rasilimali zile zile, wameshindwa kujenga viwanda vya kuzalisha na kuuza nje hakuna juhudi zozote wanazo fanya ili kuinua kilimo wananchi tukalima kwa ukubwa na huko ndiko ambako hasa midola inapatikana tunakwenda tuu ilimradi, alafu bado wanapata nguvu ya kusema wapinzani hawafai 🤔 hua nawaombea mabaya tuu siku wakiwa kikao Cha chama litokee hata tetemeko liwamalize wote labda nchi itapumua
 
Defaluation ya local currency pia ni mbinu ya uchumu ku-promote export na ku-discurrage import, huenda hilo linafanywa kwakusudia na BOT.
If true This the worst idea, hii mbinu itafeli watafute nyingine, we all know mazingira ya uwekezaji nchini yakoje yet tuna import zaid, export hatuwekez kwbisa
 
Tuna import mno. Inatakiwe tuzalishe wenyewe na vingine tuanze kuexport nje ndio tutabalance trade. Utalii impact yake ni ndogo kwenye uchumi kwa kuwa mahoteli mengi na sekta nzima ya utalii imeshikwa na makampuni toka nje. Kwa hiyo hela ya utalii inarudi hukohuko nje.



Kwa hali ilivyo dola itafika 3000. Na wakiendelea kusifiasifa dola itakuja kuwa 10,000.
2025-$1=Tsh 3,000/= +

2028-$1=Tsh 10,000/=+



Anaupiga mwingi mno 🤣
🤔🤔🤔🤔
Point well noted
 
Utaumiza kichwa wenzako hawajali, haumii kabisa kuona tanzania ikiyumba na mtanzania wa chini kabisa akiteseka.
 
Mkuu kuna nchi kama Morocco Egypt sheli sheli zina depend katika utalii kwa 70% wakati sie tuna vivutio utalii vingi kuwapita kinacho takiwa ni kufufua huo utalii pesa yetu ita paa
One of the reasons tupo hapa ni kuwa utalii wetu tuna charge gharama kubwa but services si nzuri. is why statusticaly wageni wengi wakija hawarudi. Kuna sababu nyingi pia serikali itabidi iamke kwenye hili
 
Utaumiza kichwa wenzako hawajali, haumii kabisa kuona tanzania ikiyumba na mtanzania wa chini kabisa akiteseka.
Wao hawaumii lakini wananchi tunaumia. Ukweli ni kwamba kama ulikuwa unaagiza dawa fulani kwa Dollar 100 mwaka jana kwa Tshs 230,000 leo dawa ile ile ya Dollar 100 unailipia kwa Tshs 285,000. Ongezeko la shs 55,000 kutokana na kuporomoka hela yetu.
Natamani kumtukana mtu. 😲😨😨😨
 
Kulingana na data zilizopo hata mtandaoni, shillingi yetu imeshuka kwa kiwango cha kutisha.

REKODI ZIPO HIVI:
Mwaka 2020. 1 Dollar -Tshs 2,314.8
Mwaka 2021. 1Dollar -Tshs 2,314.3
Mwaka 2022. 1Dollar- Tshs 2,326.1
Mwaka 2023 1Dollar- Tshs 2,419.6
Mwaka 2024 1Dollar- Tshs 2,463.5(Jan -June)
Sasa hivi June 2024 1Dollar -Tshs 2,627.5

Hizi ni data unaweza kuzipata hata Bank of Tanzania(Benki Kuu)

Lakini blck Market rate kwa sasa hivi mitaanai 1Dollar-Tshs 2,850, na dollar haipatikani hata benki zetu.

KWA NINI?

Dollar ZOTE ZINANUNULIWA NA MAKAMPUNI YA KI CHINA, kwa bei ya Tshs 2,850 tena bila kupepesa macho.

Nashangaa wabunge hawambani Waziri wa Fedha kuwa hili ni janga la kitaifa. Na janga hili limeanza baada ya mwaka 2022.

Dr wa uchumi, Dr Mwigulu Nchemba hapa inabidi awajibike na madhara ya kuwapa wachina kazi zote za ujenzi na wao wachina wanakausha Dollar katika uchumi wetu.
Mnamuonea bure "Dr" wa uchimi, Mwigulu. Zaidi ya sifa kwa Dr Samia zilizosheheni , kichwani ni mtupu kiuchumi.
 
Na tunatarajia kuwa na deni la trillion 120 bye Oct 2025.. yaani Samia kwa miaka minne atakuwa amekopa trillion63.Lakini ni huyuhuyu mwiguru chemba na January na kinana na ndugu nape nauye walisimama bungeni nakusema serikali ya maguru ilikopa pesa nyingi sana abazo zilikuwa trillon 7 kwa miaka 5.Nashangaa wao ndani ya muaka 5 watakiwa wamekopa trillion 63..Hivi Hawa kwanini tuwaamini
Majizi hayo
 
Back
Top Bottom