Kushusha Sukari Kienyeji

Kushusha Sukari Kienyeji

Ulipojaribu tiba lishe ya mchicha kudhibiti kisukari

  • Ndio ilishusha sukari

    Votes: 3 21.4%
  • Hapana sukari ilibaki vilevile

    Votes: 2 14.3%
  • Sukari ilizidi badala ya kupungua

    Votes: 0 0.0%
  • Sielewi

    Votes: 7 50.0%
  • Sikujaribu

    Votes: 2 14.3%

  • Total voters
    14
MziziMkavu,

Sukari ikishuka, kwa njia ya tibalishe kama hii ya juisi ya mchicha mbichi, kwa mgonjwa ambaye ilikuwa haishuki kwa baadhi ya watu, itakuwa ni jambo la manufaa. Kushusha wingi wa sukari kwenye damu kwa kutumia juisi ya mchicha mbichi, ndiyo mada iliyoko; usipotoshe kwa kudai mada ni kushusha ugonjwa wa kisukari.

MziziMkavu umesajiliwa na mamlaka husika? Mitishamba unayodai kuitumia inatambuliwa na mamlaka? Usihatarishe afya ya jamii kwa matibabu mangungu.
 
Dawa hamna mkuu utaliwa hela zako tu cha msingi diet iwe fresh tu, achana na vyakula vya wanga, sukari na punguza ulaji wa matunda yenye sukari. Hapo sukari itashuka yenyewe na uta enjoy maisha, kula sana nyama zote, mbogamboga za majani na matunda(Ila yenye sukari kula kwa wastani)
Mimi nahitaji dawa ya sukari kwa anayejua
 
Huyu jamaa hatibu chochote, nilimuulizia dawa akaniambia ni milioni kadhaa na lazima nitoe cash. Huu si ni uhuni wa waziwazi
Sukari ikishuka, kwa njia ya tibalishe kama hii ya juisi ya mchicha mbichi, kwa mgonjwa ambaye ilikuwa haishuki kwa baadhi ya watu, itakuwa ni jambo la manufaa...
 
Dawa hamna mkuu utaliwa hela zako tu cha msingi diet iwe fresh tu, achana na vyakula vya wanga, sukari na punguza ulaji wa matunda yenye sukari. Hapo sukari itashuka yenyewe na uta enjoy maisha, kula sana nyama zote, mbogamboga za majani na matunda(Ila yenye sukari kula kwa wastani)
Shukraniiii
 
Mlenge kikombe kimoja mara ngapi kwa siku kwa muda gani?

kabugira ,

Inategemea. Wapo wanaokunywa lita moja kwa siku. Wapo wanaokunywa pungufu. Kitu muhimu ni kuangalia iwapo kwa mtu binafsi inaleta ahueni kwenye wingi wa sukari kwenye damu. Ndio maana ni muhimu kuwa na kipimo cha kujiangalia wingi wa sukari kwenye damu, na hata shinikizo la damu, na kurejea kwa watoa huduma rasmi za afya kwa ushauri na vipimo. Mtu asiache kutumia dawa alizoandikiwa hospitali.
 
Changamoto ya Kula chakula cha usiku kwa wenye sugar ni ipi na tunawezaje kusaidiana wkt wa tendo?? Msaada
 
Mrejesho walio tumia juisi ya mchicha je hakuna walio jaribu?
 
Dawa hamna mkuu utaliwa hela zako tu cha msingi diet iwe fresh tu, achana na vyakula vya wanga, sukari na punguza ulaji wa matunda yenye sukari. Hapo sukari itashuka yenyewe na uta enjoy maisha, kula sana nyama zote, mbogamboga za majani na matunda(Ila yenye sukari kula kwa wastani)
Sukari usiile kabisaaa
 
Mrejesho walio tumia juisi ya mchicha je hakuna walio jaribu?
Unataka kupata mrejesho wakati aliye toa hiyo dawa ya asili ya kutibu Ugonjwa wa kisukari hivi sasa amekuwa ni Marehemu aka (RIP) Huwezi kujuwa labda yeye Marehemu pia alikuwa anao huo ugonjwa wa kisukari na akawa anatumia hiyo dawa ya jusi ya mchicha na haikomsaidia kitu. Utawezaje kupata mrejesho? Dawa ya Kutibu ugonjwa wa kisukari mimi ninayo ukihitaji nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako.
 
😂😂😂😂😂😂mkuu mzizi mkavu umenichekesha sana .Ahsante sikuwa nimecheka toka asubuhi
 
B
Yes, bado anaumwa japo anaendelea vizuri kwa kutumia vyakula na dawa za hospitali ambazo kwa hakika haziponyeshi kisukari bali zinasaidi tu kushusha kiwango cha sukari kwenye damu

Tumejitahidi sana kumtafutia tiba za asili lakini tatizo ni kwamba kila anayesema ana dawa anakuhakikishia kua hiyo ndio yenyewe, watu wengi wamepona na kwamba lazima muilipie, tena bei zao sio ndogo. Mwisho wa siku mnagundua kua nayo hiyo ni dawa ya kupunguza tu kiasi cha sukari kwenye damu na muda wowote akiacha masharti ya vyakula au akiacha dawa za hospitali inapanda tena!
dawa za hospital zinasaidia kushusha tu na pia mgonjwa akishashusha basi aachane nazo abaki tu kubalansi na vyakula.mm mama yangu siku hiz imekaa vzr ana mwaka wa tatu huu ipo normal sema tu presha ndio inamsumbua.
zingatieni vyakula vya protini wanga uwe kdg sana na vitu vya sukari asipewe kbsa ht chumvi ktk chakula isiwe nyingi. pia jitahidi awe anatoka jasho afanye mazoezi simple km ni mzee.
 
Back
Top Bottom