Kusikiliza ni sehemu ya kujisaidia wewe na watu wengine pia

Kusikiliza ni sehemu ya kujisaidia wewe na watu wengine pia

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kama ilivyo kuongea ni tiba kwa muongeaji basi hata kusikiliza nako ni muhimu kwa kusaidia wengine na kujisaidia wewe pia

Kuongea na kusikiliza ni mambo ambayo yote yana uzito wake na yana umuhimu wake,kwahiyo asitokee mtu akasema kuongea ni bora kuliko kusikiliza laa! Anafeli bali yote mawili yana uzito sawa

Kumbuka ili kujifunza maarifa mbali mbali inabidi usikilize zaidi kuliko kuongea,na kwa kusikiliza pekee ndio ufahamu wako utapanuka na kupata maarifa zaidi

Bahati mbaya sana watu wengi huwa hatupendi kusikiliza na matokeo yake tunashindwa kutatua changamoto mbali mbali ambazo zinaikumba jamii yetu na watu wa karibu,mfano wenye mamlaka hawana mda kusikiliza changamoto za wananchi wao na hivyo inakuwa vigumu kutatua shida zao

Mfano hivi karibuni katika nchi ya mlima kilimanjaro,kumetokea majanga ya watu kutekwa na kuuwawa na jamii nyingi ya nchi hiyo imepoteza wapendwa wao,lakini pamoja na wananchi wa nchi ya kilimanjaro kuongea bado viongozi wa jamhuri ya kilimanjaro wameziba masikio yao,matokeo yake mamlaka imeshindwa kutatua kero ya wananchi wake

Lau mamlaka ingesikiliza na kuelewa hitaji la watu wa jamhuri ya kilimanjaro basi hakika leo hii tusingekuwa tunalalamika kuhusu utekaji huu na madhila haya ambayo wananchi wanapitia

Kama kila mtu kwa nafasi yake akijifunza kusikiliza vizuri hakika tuta tatua changamoto nyingi sana ambazo zipo katika jamii yetu,ikiwa wanandoa watasikilizana hakika migogoro ya ndoa itapungua,jamii ikisikilizana ndugu watapatana na kushirikiana

Kwahiyo kusikiliza ni kipaji kama vipaji vingine hivyo tujifunze kusikiliza na mwisho wa siku tutakuja kuwa wasikilizaji wazuri

Na ukiwa na mtu msikilize bila kuharibu mazungumzo kwa kupokea simu au kujibu meseji,maana siku hizi tumekuwa na huu ugonjwa wa smart phonization yaani simu zimetuathiri kiasi kwamba hatutaki kuziacha hata dakika moja,itafika kipindi tusipokuwa makini upo na mwenza wako unafanya ibada ya tendo la ndoa na wakati huo huo unataka kuchezea simu,huu ni wehu wa wazi wazi kabisa

Tujifunze kusikiliza mara mbili zaidi ya kuongea hata nature/God alitupa masikio mawili ili tusikilize zaidi kuliko kuongea,na cha kufurahisha zaidi organi ya kwanza kuumbwa tukiwa tumboni ni masikio ili tuanze kusikiliza kabla ya kuongea

Ni hayo tu!
 
Kusikiliza ni bora kuliko kuzungumza na ndio maana tuna masikio mawili na mdomo mmoja
 
Back
Top Bottom