Kusimama na Catherine Ruge ni Wajibu

Huyu Catherine Ruge anaonekana ni Kamanda kweli kweli. Anaonekana siyo mtu wa kucheka na kima.
Huyu Shangazi amepigwa, akaumizwa mpaka kulazwa na anatibiwa mpaka leo. Shangazi Fatma ofisi yake ilipigwa bomu bila majibu, kaondolewa kwenye kampuni aliyoianzisha, kafungiwa leseni inayompa kula na bado wamesimama. Kuna uzi humu niliona wanaume wazima, tena wenye magari na wasomi, mmoja hakosekani kwenye nyuzi za diamond kumpambania, wakilia lia kwamba hawawaoni akina shangazi wakiwapigania tena. Vilio hivyo vilitokana na kupanda Kwa bei ya mafuta ya gari.

Ukifikiria mtu kama huyu, pengine ana watoto wanamuita Baba, utavionea huruma vizazi vijavyo.
 
Wacha upumbavu wewe,kwa hiyo hao wamwela walikuwa wanatembea na hukumu ya kumpiga risasi huyo mshukiwa? Kwa sababu waliondoka naye akiwa mzima kabisa.
 
Wacha upumbavu wewe,kwa hiyo hao wamwela walikuwa wanatembea na hukumu ya kumpiga risasi huyo mshukiwa? Kwa sababu waliondoka naye akiwa mzima kabisa.
Narudia tena na ninakazia siku nikiwa Rais wa nchi hii wezi na majambazi hawatasau jina langu maana watapata show hawajapata kuona
 

Kuna mambo yanasikitisha sana.

Hatukupaswa kuwatelekeza mashangazi hawa hivi, katika nyakati zao za kutuhitaji kama hizi.

Nawaelewa wenye maoni hasi kumhusu mama Tanzania. Mama TZ ni nani kulinganisha na mpambanaji Catherine Ruge?

Full force tunaweza kusimama na Catherine Ruge kwa vitendo na meza ikapinduka.
 
Ni muendelezo wa matendo yanayovunja sheria toka kwa jeshi la polisi, na hii yote inasababishwa na kukosekana consistence kwenye madai yetu, hasa kuhusu haki.

Matukio kama haya yanapotokea, huwa hatuhakikishi mwisho wake umejulikana, ili kama watuhumiwa wakikutwa na hatia wapelekwe mahakamani, mfano Akwilina na mauaji kule Mtwara.

Huu ukimya wetu ndio unasababisha polisi waendeleze hii tabia yao, msukumo toka kwa raia kuhusu haki huwa kuna wakati unayeyuka mithili ya barafu kwenye jua kali, na hili jukumu sio la wanasiasa peke yao, ni letu sote, kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo, ahakikishe analaani huu ukatili kwa namna yake.
 

Kupiga kelele sawa. Kila mmoja? Ndiyo. Lakini cha kujiuliza vyama vya siasa viko wapi?

Vyama vya Siasa havijui au vimesahau wajibu wao?
 
Kupiga kelele sawa. Kila mmoja? Ndiyo. Lakini cha kujiuliza vyama vya siasa viko wapi?

Vyama vya Siasa havijui au vimesahau wajibu wao?
Hawa tuungane nao, tusiwaache peke yao, tabia ya kuwaacha peke yao ndio hutufanya tuanze kulalamika pale wanapoonekana kukaa kimya, kumbe kama tungejijengea mazoea ya mapambano ndani yetu, wao wakikaa kimya, sisi naturally tungeendelea na mapambano tu.
 
Polisi ni genge la kihalifu lililoundwa na Serikali na kubarikiwa na wananchi👇

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Unasimamaje na kahaba? Yule amechoka a anatafuta Kiki akijaribu kuwalinda wahalifu apate umaarufu. Anashirikiana ns wezi, anafaifika na uwizi w mjombake. Naye akamatwe atoe ushirikiano. RPC wa Mara mdebweto kweli arudishwe makao makuu
Bila kuathiri mchango wako, kwanini umemuita huyu Dada "kahaba"?
 
Hakuna Mwanadamu yoyote aliyeruhusiwa KUUA - kufanya hivyo ni kumkosea Mungu. Na ndiyo maana kuna sheria na Mahakama kama mmoja wetu amekengeuka.

Police hili kwenu ni doa jipya jekundu !! Mtuhumiwa Jambazi sugu uliyemkamata kumwekea mazingira ya kukimbia then unamtwaga risasi... hapa pana maswali mengi kuliko majibu.
 
Nakazia nakazia.
Tupinge uhuni wa mauaji ya kukusudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…