Kusimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara

Kusimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara

JamboJema

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
1,143
Reaction score
209
Wajuvi wa sheria imekaaje hii kwamba mumishi anasimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara? Nimeisoma sheria ya kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 inasema mtu atasimama kazi na kulipwa mshahara full. Kumbe eti Public Service's Standing Orders ya 2009 inasema utaendelea kulipwa nusu mshahara kipindi umesimama kazi.

Wadau hii ya sheria kusigana inawaweka wapi watumishi wa umma.

Where could one seek for redress on this?
 
Mie napita tu. Wasubili wenyewe waje wakupe maelezo.
 
heri huo nusu mshahara, ile sheria mpya inataka ulipwe 1/3 ya mshahara
 
mkuu me napita tu lakini according to wizara ya kazi walipopita kutoa elimu ya haki ya mfanyakazi walisema sheria mpya inamlazimisha mwajiri kumlipa mwajiriwa mshahara kamili pindi amsimamishapo kazi...wataalamu watujuze zaidi
 
mkuu me napita tu lakini according to wizara ya kazi walipopita kutoa elimu ya haki ya mfanyakazi walisema sheria mpya inamlazimisha mwajiri kumlipa mwajiriwa mshahara kamili pindi amsimamishapo kazi...wataalamu watujuze zaidi

Na mm najua kuwa aliyesimamishwa hulipwa full salary. Kabla ya 2004 alikuwa analipwa half salary ambapo akirudishwa kazini baada ya kuonekana hana hatia hurudishiwa ile nusu. Sheria hii ilibadilishwa baada ya kuona waajiri wengi huwasimamisha kazi waajiriwa kwa uonve tu, kama kuwakomoa vile.
 
Kweli kabisa, mwajiriwa anapaswa kulipwa mshahara kamili pindi akiwa amesimamishwa hii imeelezwa kwenye Rule 27 (1) ya Tangalo la Serikali Namba 42. Pia kama nakumbuka vizuri kuna Judge wa High Court alikubaliana na hili katika kesi kati ya Salivatory Kundi Vs Precision Air (Hii nitathibitisha nikirudi Bongo kwani mikoba yangu sipo nayo huku nilipo) Nikumbushe siku yoyote kuanzia Saturday nipitie documents zangu ili nikupe kesi ya uhakika. Kisha umpatie huyo Afisa Utawala ajiupdate kwani kupitia yeye ndio wanaweza kufanya marekebisho wa hiyo Standing Order.
 
Na mm najua kuwa aliyesimamishwa hulipwa full salary. Kabla ya 2004 alikuwa analipwa half salary ambapo akirudishwa kazini baada ya kuonekana hana hatia hurudishiwa ile nusu. Sheria hii ilibadilishwa baada ya kuona waajiri wengi huwasimamisha kazi waajiriwa kwa uonve tu, kama kuwakomoa vile.
Standing Orders za 2009 bado zinatambua nusu mshahara!
 
Ni kweli sheria namba 6 ya mwaka 2004 Empolyment and Labour Relations Act 2004 haitambua nusu mshahara na wala haina kufukuza kazi ,lakini ukija kwenye sheria namba 8 2002 na kanuni zake 2003 ya Public service Act 2002 INATAMBUA NUSU MSHAHARA NA PIA BADO INA KUFUKUZWA KAZI.

hizi sheria mbili zinatupa shida sana katika matumizi yake na pia zinaleta ubaguzi. Kwani utakuta sheria namba 8 /2002 inatumika sana kwa watumishi wa vyeo vikubwa na sheria namba 6 /2004 inatumika kwa watumishi wa vyeo vya chini,wakati sheria zenyewe hazibagui vyeo. Ukiuliza maasifa utumishi hawana jibu ila wanafanya kazi kwa mazoea tu.ELIMU NI MHIMU KWA HAWA MAAFISA UTUMISHI KUHUSU MGONGANO WA SHERIA HIZI
 
Mloko dip kwenye sheria mtudadanulie kwa kina
 
Kweli kabisa, mwajiriwa anapaswa kulipwa mshahara kamili pindi akiwa amesimamishwa hii imeelezwa kwenye Rule 27 (1) ya Tangalo la Serikali Namba 42. Pia kama nakumbuka vizuri kuna Judge wa High Court alikubaliana na hili katika kesi kati ya Salivatory Kundi Vs Precision Air (Hii nitathibitisha nikirudi Bongo kwani mikoba yangu sipo nayo huku nilipo) Nikumbushe siku yoyote kuanzia Saturday nipitie documents zangu ili nikupe kesi ya uhakika. Kisha umpatie huyo Afisa Utawala ajiupdate kwani kupitia yeye ndio wanaweza kufanya marekebisho wa hiyo Standing Order.

NIMETUMIWA HII KUHUSIANA NA MADA TAJWA. WAJUVI WA SHERIA ENDELEENI KUTUPATIA 'DOZI': "Ni kweli kwa mujibu wa ELRA 2004 mtumishi anapaswa kulipwa full salary. ELRA 2004 ni general law ambayo inabeba watumishi wa umma na wengine wa mashirika ya binafsi ndiyo maana utaona kuwa kesi uliyo-site inahusu precission air.

Kwa case ya Serikali mara nyingi wanaohudumiwa na ELRA 2004 ni Operational Workers tofauti na maofisa wengine ambao wanahudumiwa na Public Service Act 2002 ambayo inatamka kuwa Mtumishi alipwe nusu mshahara. Kwa maneno mengine Public Service Act ni Specific law kwa Watumishi wa Umma ambao si operational. Inahitajika harmonization ya hizi sheria hata hivyo."
 
NIMETUMIWA HII KUHUSIANA NA MADA TAJWA. WAJUVI WA SHERIA ENDELEENI KUTUPATIA 'DOZI': "Ni kweli kwa mujibu wa ELRA 2004 mtumishi anapaswa kulipwa full salary. ELRA 2004 ni general law ambayo inabeba watumishi wa umma na wengine wa mashirika ya binafsi ndiyo maana utaona kuwa kesi uliyo-site inahusu precission air. Kwa case ya Serikali mara nyingi wanaohudumiwa na ELRA 2004 ni Operational Workers tofauti na maofisa wengine ambao wanahudumiwa na Public Service Act 2002 ambayo inatamka kuwa Mtumishi alipwe nusu mshahara. Kwa maneno mengine Public Service Act ni Specific law kwa Watumishi wa Umma ambao si operational. Inahitajika harmonization ya hizi sheria hata hivyo."

Wadau hebu tuache kutafsiri sheria kwa mazoea.

Act No 6 of 2004 (ELRA) kwenye scope of coverage haijasema kama ina cover watumishi walio kwenye operation service serikalini na wala haijagusa amma kutafsiri neno operation services na wala hilo neno halipo.

Maafisa utumishi wengi na wadau bado wana ile dhana na minajili iliyokuwamo kwenye Security of Employment Act.

USHAURI
uKIWA NATATIZO ANGALIA NI SHERIA IPI KWAKO UNAKUPA AHUENI KATI YA ELRA AU PUBLIC SERVICE ACT then itumie inayokufavor. Hata unapokata rufaa angalia ni wapi more favourable kwako kati ya CMA au Tume ya Utumishi wa Umma.

ANGALIZO
Hiszo sheria zinagongana ni muhimu kuutumia huo udhaifu kushinda kesi yako
 
Wadau hebu tuache kutafsiri sheria kwa mazoea.

Act No 6 of 2004 (ELRA) kwenye scope of coverage haijasema kama ina cover watumishi walio kwenye operation service serikalini na wala haijagusa amma kutafsiri neno operation services na wala hilo neno halipo...

You make good point, I do concur with you. Lakini naona as long tumeona kuwa kuna sheria mbili ambazo zinakinzani nazani tukiwa kama watu ambao tunapenda haki basi ni bora kuliweka hili wazi ili mabadiliko yaweze kufanyika.

Kitu ambacho nilikua naomba nisaidiwe ni Kifungu (Section) ipi kwenye The Public Service Act of 2002 imezungumzia maswala ya half pay kwa mtu aliye suspension. Nitafurahi sana kama mtanisaidia katika hilo.

Pia nimejaribu kuambatanisha kesi ya Precision Air Services v. Salvatory Kundy ingawa the last two weeks ilikua inanisumbua sana.
 
You make good point, I do concur with you. Lakini naona as long tumeona kuwa kuna sheria mbili ambazo zinakinzani nazani tukiwa kama watu ambao tunapenda haki basi ni bora kuliweka hili wazi ili mabadiliko yaweze kufanyika...
JamhuriHuru nazidi kukushukuru. Hata hivo kesi hii kwangu imezidi kugoma kufunguka! Nasubiri kwenye email ndugu yangu.
 
Hello JamboJema nimeshakutumia kwenye email yako, jamani naombeni minisaidie Kipengele (Section) kwenye The Public Service Act ambavyo vinakinzana na Employment and Labour Relation Act kama ambavyo ilielezwa na wenzetu hapo chini. Binafsi nataka nifanyie kazi zeni tutapeana taarifa kamili.
 
You make good point, I do concur with you. Lakini naona as long tumeona kuwa kuna sheria mbili ambazo zinakinzani nazani tukiwa kama watu ambao tunapenda haki basi ni bora kuliweka hili wazi ili mabadiliko yaweze kufanyika...
Mr Jamhuri huru, kifungu cha sheria ya public service Act kinachosema half Salary kiko kwenye public service regulation ya 2003 kifungu cha 34(4)hii ni regulation ya PSA number 8 ya 2002(public service act) na pia kifungu kinachofukuza kiko kwenye ACT yenyewe ya PSA 2002 kifungu cha 23 pia Rais anaweza kumwondoa mtumishi wa umma katika ajira kwa mjibu wa kifungu cha 24 cha PSA 2002
 
Mr Jamhuri huru, kifungu cha sheria ya public service Act kinachosema half Salary kiko kwenye public service regulation ya 2003 kifungu cha 34(4)hii ni regulation ya PSA number 8 ya 2002(public service act) na pia kifungu kinachofukuza kiko kwenye ACT yenyewe ya PSA 2002 kifungu cha 23 pia Rais anaweza kumwondoa mtumishi wa umma katika ajira kwa mjibu wa kifungu cha 24 cha PSA 2002

Thanks a million ndugu yangu, Section 24 ya PSA 2002 nimeiona na nimejiridhisha nashukuru sana, ila sababu yakuuliza ilikuwa ni kupata kujua kuhusu NUSU MSHAHARA ambapo nimeona kuwa kumbe imewekwa kwenye Kanuni ya 34 (4) ya Regulation ambayo nakili bado sijaipata. Naomba sana ukiipata soft copy unitumie kwenye jumuhurihuru@rocketmail.com.

Katika pekua pekua yangu kuna kitu nimegundua hasa ukizingatia kuwa hoja ya msingi ilikua ni kukinzana katika maswala ya mshahara wakati mtumishi wa serikali yupo suspension. Pia hoja zingine zilikua kuhusu mambo mbali mbali yanayotofautiana kati ya Publice Service Act na Employment and Lobour Relation Act (ELRA).

Regulation ya Public Service Act (Kanuni ya 34 (4)) kama ilivyowekwa na Mjaumbute hapo juu inasema nusu mshahara wakati G.N. No 42 Rule 27 (1) ya ELR Act inasema full remuneration. Hapa sitaki kusema sheria ipi ina nguvu kuliko nyingine ila swala nalotaka kusema ni Sheria ipi itatumika wakati Mtumishi wa Serikali yupo suspension. Tukilijua hilo ndio wote tutakubalia kuwa Mtumishi wa serikali aliye suspension anatakiwa kulipwa nusu mshahara au mshahara kamili.
  1. Kwanza wote tunakubaliana kuwa Mahakama ndio chombo kilichopewa dhamana yakutafsiri sheria, na pia huwa kinatunga sheria (Precedent/Case Law). Hivyo basi kwa mujibu ya Ruling ya kesi kati ya The Attorney General vs. Maria Mselemu, nyingine kati ya Attorney General vs. Allan Mulla (Revision No 270 and 271 respectively) . Ambapo kati ya disputing issue zilizosababisha preliminary objection (PO) moja wapo ilikua ni "Jurisdiction of CMA to entertain the dispute where the government is part" Maauzi ya CMA yaliungwa mkono na Rweyemamu, J katika revision aliposema "…CMA had acted properly and dismissed PO number 1 the court emphasized that, under Section 2 of ELRA No.6/2004 the CMA has jurisdiction to labour disputes defined by Section 4 of ELRA No.6/2004 and those reversed for the decision of the Labour Court under Section 94(1)(a) to (f) of of ELRA No.6/2004"
Katika hizo Sections hapo juu kwanza utaona wigo ambao ELR Act of 2004 imepewa, pili utapata tafsiri ambapo serikali nayo inatambuliwa kama ni Mwajiri , tatu ni uwezo/nguvu iliyopewa Labour Court. So hapa kwanza tutakubaliana kuwa kumbe Public Servant nao wanalindwa na sheria hii (ELRA No.6/2004) inapotokea kuna dispute. Hivyo nachelea kusema kuwa mfanyakazi wa serikali anapokua suspension anapaswa kulipwa mshahara kamili kama G.N No 42, Rule 27 (1) inavyosema. Ambapo kwenye the same (G.N No 42) Rule 2 inasema itatumika hata kwa Government Officials.

  1. Pili kama ambavyo sheria yenyewe inavyojiita kwenye Section 1 "The Public Service Act" hii inamaanisha ni sheria ya wafanyakazi wa Serikali ambapo Serikali yenywe ni Mwajiri. Hapa tunaona kwamba, na ni ukweli usiofichika kuwa Serikali ni Mwajiri kama alivyo Mwajiri mwingine inapokuja kwenye maswala ya kazi au mahusiano kazini. Achilia mbali kazi zingine za serikali ikiwa pamoja na kulinda mipaka ya nchi. Lakini hapa tunamwangalia Serikali kama mwajiri na si vinginevyo. Ambapo kihistoria ndio alikua mwajiri mkubwa alishajitengenezea Sheria na Kanuni zake mbalimbali kabla hata hii ELRA No.6/2004 haijatungwa.
Hivyo basi Mwajiri Serikali anapata advantage ya kihistoria kuwa na "employment policy or practice" kabla ya Waajiri wenzake kama ambavyo imetafsiriwa kwenye Section 7(9)(c ) ya ELRA No.6/2004. Mbali na hivyo pia alishawahi kuwa na policies and procedures that establish standard of conduct required of her employee. Kama ilivyo kwenye Rule 11 (1) to (6) of G.N. No 42. Kwa mantiki hii The Public Service Act, Regulation na Standing Orders zote pamoja na mambo mengine yanayoendesha mahusiano kati ya Serikali kama Mwajiri na Wafanyakazi wake yapo subject to ELR Act of 2004. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo;

(i)Article 36 (4) ya Katibu ya Tanzania inampa Rais nguvu yakuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali. Hapa inamaanisha, kwa namna moja ama nyingine Rais ndio Kiongozi mkubwa wa mwisho katika Serikali ambayo ni Mwajiri.Ndio maana hata appeal za maswala ya kinidhamu za wafanyakazi wa Serikali zingine anapelekewa yeye kwa mujibu wa Section 25 (1) to (2) ya Public Service Act. Mfano Section 25(1)(d) inasema "where a public servant or the disciplinary authority is aggrieved with the decision in………… shall appeal to the President whose decision shall be final". Hapa ukomo wa maamuzi ya Rais ni Final katika maswala ya kinidhamu kwa Public Servant ambao ni wafanyakazi wake na yeye akiwa kama boss wao wa mwisho. Kama ilivyo kwenye makampuni binafsi ambapo Wamiliki/ Directors/ Managers wanavyotoa maamuzi ya mwisho ndani ya kampuni.

(ii)Nikilejea kwenye Section 25(1) (d) niliyoitaja hapo juu kwamba Rais decision yake ni final only katika maswala ya mahusiano ya kikazi kati ya Mwajiri (Serikali) na Mwajiriwa (Public Servant). Endapo Public Servant atakua hajalidhishwa na maamuzi ya Rais ambaye kwa mujibu wa taratibu zao ni final basi mtu huyo anayohaki ya kwenda kwenye vyombo vya sheria ambavyo ndio vina jukumu lakutoa haki. Hii ni kwa mujibu wa Article 107A ya Katiba ya Tanzania ambayo inasema "Mamlaka ya utoaji haki ktk Jamuhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama…..". Kwa hiyo sio Rais wa Tanzania ndio atatoa haki, so hapa tutakubaliana kuwa Rais ambaye ni Kiongozi wa Serikali ni Mwajiri kama walivyo Waajiri wengine. Hivyo basi Publice Service Act na Regulation zote zipo subject to ELR Act of 2004.

(ii) Kwa kumalizia ni kwamba hata Section 24 (1) ya Public Service Act inayompa Rais nguvu yakumtoa Public Servant kazini if in the interest of public. Hakifanya hivyo bila kufwata taratibu zilizowekwa kwenye Rule 13 of G.N No 42 halafu hiyo kesi ikaenda CMA itakula kwa Mwajiri ambaye ni Serikali na Kiongozi wake ni Rais. Swala la Public Interest haliwezi likafanya mtu akose haki yake na wakati tumeona kuwa mtoa haki kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ni Idara ya Mahakama.

Wanajamii vipi hapo mmenielewa?
 
Mkuu Hamhuri Huru wewe unaonekana ni mzuri sana kwenye labour laws and legal aurguments.

Plz ni pm email yako ili tuunganishe nguvu kutetea wafanyakazi wafanyakazi wanaonewa na waajiri wao. tutaongea zaidi
 
Back
Top Bottom