Kusingiziwa kunauma jamani asikwambie mtu

Kusingiziwa kunauma jamani asikwambie mtu

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Habari ya weekend wana Jf,.
Waswahili huwa tuna msemo mmoja eti 'ukweli unauma'... Kwamba ukiongea jambo ukaona mhusika amekasirika basi hilo jambo ni la kweli. Mimi nakataa jamani jambo la kusingiziwa linauma sana, mimi binafsi mtu akikomaa kuning'ang'aniza nimefanya kitu ambacho sijafanya naweza kumchapa makofi na kama ni mtu ambae siwezi kumpiga wala kugombezana nae huwa najikuta nalia tu.
Mimi binafsi katika kukua kwangu nimesingiziwa mengi sana ila yapo mengine hadi leo hayafutiki. Nikiwa darasa la saba kuna mtu alipeleka taarifa kwa walimu kwamba natoka na wakaka fulani hivi wawili (msishangae enzi zetu tulikuwa tunamaliza la saba tukiwa wakubwa sio kama siku hizi watoto form three ndo anavunja ungo). Ni stori ndefu ilikuwa ila habari ilikuwa ndio hiyo, tulitajwa wengi tuliokuwa tunatuhumiwa kujihusisha na mapenzi tukaitwa kwa mwalimu mkuu akawa anatupatia nasaha eti 'kuweni makini siku hizi magonjwa mengi ikibidi basi mtumie kondom' lahaulaa mimi hakuna siku nililia kama siku ile nilijiapiza aliyefanya hivyo lazima nimkomeshe japo mwisho wa siku sikumfanya chochote. Ninachomshukuru Mungu mzazi wangu alinielewa na hakuwa na nongwa na hiyo ilitosha sana kunipa amani. Cha ajabu yule mwendawazimu baada ya kuingia sekondari form one tu kafukuzwa shule kwa kashfa ileile aliyonizushia mimi nikasema malipo hapahapa duniani pambaf.
Jambo lingine ninalokumbuka nikiwa form four kuna mtu alimpelekea maneno rafiki yangu wa karibu kuwa mimi nilikaa nilisema eti yeye anatembea na mkaka mwenye UKIMWI, Nilishangaa tu yule rafiki yangu anajiweka mbali na mimi hanichangamkii wako busy tu na rafiki yetu mwingine, siku anakuja kuniambia hayo nilishangaa sana maana kwanza sikuwahi kusema, pili sinaga tabia ya kumsema mtu wangu yeyote wa karibu iwe rafiki,ndugu,mpenzi or whatever kwa watu baki, lakini baadae nilikuja kuhisi labda ametunga tu mwenyewe kwa lengo la kukata urafiki.
Lingine nikiwa mdogo kuna dada yangu mmoja alinisingizia nimemuibia mia yake aliweka mezani na mimi ni mtu pekee nilikuwepo humo ndani, alinikomalia kuwa nimeichukua akaanza kunipiga kadri ninavyokataa sijachukua ndivyo kipigo kinazidi, baadae nilipoona kipigo kimenielemea ikabidi nikubali kuwa nilichukua ila mimi pia nimeipoteza nilikokuwa ninacheza ndio kuniacha. Kesho yake asubuhi akiwa anapiga deki akaiona uvunguni mwa kitanda. Akaniita tena nikasema si unaona, mimi sikuchukua akataka kunishushia tena kipigo kwa kuogopa kipigo na fimbo za jana yake hata hazijapona nikasema niliidondosha mwenyewe baada ya kuchukua sikujua imedondokea hapo. Hili tukio huwa linaniumiza na kila nikikumbuka machozi yanadondoka ila nimepanga ipo siku nitamkumbusha mhusika najua ye kasahau.
Kama umewahi kusingiziwa tupatie kisa na wengine wajifunze.
 
Kumbe wewe ndiwe uliyenisingizia kuwa mimi ni mlevi wa gongo, mvuta bangi, mbinafsi, msengenyaji, mlafi, mchawi, kibaka, mzinzi, jambazi, mchoyo, mchafu, mkorofi/mkatili, kiherehere, muuaji na sitaweza kukuoa kwa hizo sababu?

Niko hapa nnje mlangoni kwako toka ndani uje nje nikukung'ute vizuri ili uwe na adabu.
 
Hahaha walaaa sijawahi kumsingizia mtu mimi
Kumbe wewe ndiwe uliyenisingizia kuwa mimi ni mlevi wa gongo, mvuta bangi, mbinafsi, msengenyaji, mlafi, mchawi, kibaka, mzinzi, jambazi, mchoyo, mchafu, mkorofi/mkatili, kiherehere, muuaji na sitaweza kukuoa kwa hizo sababu?

Niko hapa nnje mlangoni kwako toka ndani uje nje nikukung'ute vizuri ili uwe na adabu.
 
Kuna mtu humu ananisingizia ananijua, ni jirani yake Dar, tena nipo chuo, Tanzania Insitute of Accountancy. Inauma sana. 😟😖
 
Pole sana aisee, Iyo ya primary imenikumbusha kuna jamaa yangu alikuwa na mdogo wake wa kike, Sasa yule mdogo wake tulikuwa tunasikia tu uvumi kama anatembea na mwl wa Hisabati tukawa tunamtania kumbe ilikuwa inamuumiza moyoni,Akaenda kusema nyumbani kwao yule binti akachapwa sana. Baadae kama siku 2 hivi, mwl alitoa zoezi gumu sana bila kutoa mda wa kukusanya akaondoka na tulishazoea kukusanya ni mda wowote tu aisee alirudi zimebaki dakika 10 kipindi chake kuisha akaomba kazi yake. Cha kushangaza wadada wengi akiwepo yeye walikuwa wamefanya na vidume wachache. Ikaja ikaniangukia nami sijafanya kwenye kundi moja na huyo kaka yake. Ndo siku niliochapwa bakola 5 utadhani anaua nyoka siwezi sahau hadi sasa ila bahati nzuri mwl mkuu alikuwa rafki yake mzee nlienda kumweleza wakamkanya.
 
Kwa hiyo mwalimu alihusisha uvumi ndio akalipiza au..

Back
Top Bottom