Kusinyaa kwa Nafasi ya Kiraia (Civic Space) Tanzania: Si salama kuendelea kuishi chini ya Sheria kandamizi

Kusinyaa kwa Nafasi ya Kiraia (Civic Space) Tanzania: Si salama kuendelea kuishi chini ya Sheria kandamizi

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Nafasi ya kiraia (2).png


Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kusinyaa kwa Nafasi ya Kiraia (civic space), yaani ushiriki huru katika masuala ya kidemokrasia nchini Tanzania kabla na baada ya uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba, 2020. Serikali sio tu ilijionesha wazi kukandamiza vyombo vya habari, lakini pia kudhoofisha uwezo wa vyama vya siasa kufanya kampeni.

Vyombo vya habari ni muhimu katika uchaguzi. Wananchi hutumia vyombo vya habari kutafuta habari kuhusu ajenda za kisiasa za wagombea na kujadili masuala mbalimbali ya umma. Vyombo vya habari hufanya kama mlinzi wa usimamizi wa uchaguzi. Lakini ukandamizaji dhidi ya waandishi wa habari na sauti pinzani umesababisha vyombo vya habari kujidhibiti wenyewe, hivyo kujikuta wakiwa wamebakiwa na uchochoro mdogo tu wa kutamba katika shughuli zao.

Tangu 2019, serikali ilifanyia marekebisho Sheria mbalimbali ili kuzuia haki ya kukusanyika na uhuru wa kutoa maoni binafsi.

Serikali iliweka vizingiti dhidi ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari bila uhalali. Zaidi ya hayo, wananchi walizidi kukosa fursa ya kupata habari na vyama vya siasa kuwekewa vikwazo katika uhuru wao wa kujumuika. Hii ni hatari hasa kwa vile Tanzania itaendelea kufanya chaguzi zake kila baada ya miaka mitano.

Hata hivyo, namna za kuzima sauti za watu hufanyika kwa mitindo mingi – vitisho, Sheria kandamizi n.k. Nadhani sote tunakumbuka suala la changamoto ya kutumia mitandao ya kijamii kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2020. Sina taarifa rasmi lakini nachelea kusema haikuwa coincidence eti kwamba, ghafla tu, tukiwa kwenye kipindi cha uchaguzi tunakumbana na changamoto ya huduma za mitandao ya kijamii.

Kabla ya vimbwenga hivyo, tarehe 10 Agosti 2020, kwa mfano, Radio Free Africa iliwekwa chini ya uangalizi kwa muda na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kurusha hewani mahojiano ya BBC na mgombea urais wa upinzani kwa sababu mahojiano hayo hayana uwiano.

Marekebisho ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) yamezidisha ukandamizaji wa vyombo vya habari kwani inaharamisha uhuru wa kujieleza, inakataza uchapishaji wa masuala mbalimbali na kumpa Mdhibiti mamlaka makubwa ya kusimamisha vyombo vya habari na waandishi wa habari.

Mnamo Januari 2019, Bunge lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo inaweka mazingira magumu sana ya kufanya kazi kwa vyama vya siasa, na kukandamiza uhuru wa kujumuika:

Sheria hiyo inampa mamlaka makubwa sana Msajili wa vyama vya siasa, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kudai taarifa zozote kutoka kwa vyama vya siasa bila kibali, na hivyo kutengeneza mwanya wa ufuatiliaji wa uendeshaji wa vyama vya siasa.

Yapo maeneo mengi yanayohitaji kushughulikiwa ili umma wa Watanzania uendelee kuwa na uwanja mpana wa kufurahia Utanzania wao pasi na kuwa na hofu ya “kushughulikiwa” na “wenye mabavu”.

Katika Ripoti ya Uhuru wa Kujieleza iliyotolewa na taasisi ya Article 19 Mwaka 2021, inaonesha kuwa katika mwaka wa Uchaguzi 2020 Tanzania ilishika nafasi ya 103 kati ya nchi 161 zilizoorodheshwa. Nafasi hii ya 58 kutoka mkiani si sehemu sahihi ingawa ina ahueni kulinganisha na nchi kama Rwanda na Burundi ambazo zipo katika hali tete (in crisis) katika namba 138 na 147 – yaani nafasi ya 23 na 14 kutoka mkiani.

Katika nchi 8 zinazoizunguka Tanzania, ni nchi mbili tu – Malawi na Kenya – ambazo zinadondokea katika category ya “Less Restricted” (Vizuizi Vidogo). Ni anguko kubwa la nafasi 25 kwa Tanzania tangu mwaka 2010.
Info-Graphics.png

Kielelezo 1: Nafasi ya Uhuru wa Kujieleza ya Tanzania kidunia ikilinganishwa na nchi 8 inazopakana nazo.

Ni sawa kuwa inawezekana kiongozi aliye madarakani akaonekana kuwa si “mtata”, lakini hii haitoshi kuendelea kuishi na Sheria kandamizi – hususan zile zinazowaziba Wananchi wake mdomo. Ni vema kufuta sheria zinazokinzana na uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika pamoja na kukomesha unyanyasaji wa wanahabari na vyombo vya habari ili kuendeleza utiririshaji wa habari huru kabla, wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.

Civic space ndio msingi wa jamii yoyote iliyo wazi na ya kidemokrasia. Nafasi hii ya raia kushiriki shughuli za kidemokrasia bila woga na vikwazo ikipewa kipaumbele, raia na taasisi za dola wanaweza kupanga, kushiriki na kuwasiliana bila vikwazo.
 
Hivi ulimaa Isha asasi za kiraia au ndio ulimaanisha hiyohiyo nafasi za kiraia?
 
Ukweli usemwe: hapa ndipo alipokosea zaidi marehemu. Katika kipindi chake ndiyo mambo yaliharibika zaidi. Hadi mwisho wa kipindi cha JK nadhani tulikuwa 'less restricted'.

Aliyemrithi amerithi hali iliyokuwepo na hakuna dalili za kubadili, zaidi ya maneno.
 
Back
Top Bottom