Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wana CCM wengi sana wanatamani kwa mtizamo wao ghushi na uliojaa ugoto katika kufikiri, kuwa John Magufuli asipingwe na mgombea toka CHADEMA. Wao wanadai kwa aliyoyafanya Magufuli kama Rais wa Tanzania hakuna haja ya kupingwa.
Lakini najiuliza kama Magufuli wanataka apite bila ya kupingwa, je kutakuwa na haja ya kufanya uchaguzi kuwachagua wabunge na madiwani? Kama kuna ulazima wa kuwepo kwa uchaguzi huo kigezo kitakuwa ni nini? Je, Madiwani na Wabunge hakuna cha kutukuka walichofanya kuwafanya wasipingwe kwenye uchaguzi ujao?
Na kama itakuwa na wabunge na madiwani nao wasipingwe kigezo kitakuwa ni nini na je na wabunge na madiwani toka vyama vingine mbali na CCM nao hawatapingwa?