Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Una uelewa wowote kweli kwenye investments za namna hiyo au ni akili matope tu zimekujaa kichwani? Kama kitu hukielewi heri kukaa kimya maana kukaa kimya pia ni hekima!
 
Naona mheshimiwa Zitto hawajui vizuri wachina ila sijajua kama anafanya makusudi kwa ajili ya kujiimarisha kisiasa au wachina walishafanya yao tayari. Kwa kumsaidia tu angeangalia kwanza mkataba mdogo tu wa Star times walioingia wachina na TBC aone jinsi hawa viumbe walivyo hatari ndio sasa aje atoe ushauri kuhusu huu mkataba wa ujenzi wa bandari Bagamoyo kama utakuwa na manufaa. Mchina akikupa milioni moja ujue yeye anategemea kupata zaidi ya bilioni moja hawa viumbe ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa letu. Wako tayari kutoa hongo kwa gharama yoyote kwa wanasiasa ili mradi tu wafanikishe wanachokitaka, ndiyo maana sishangai kuona wanapata watetezi wa huo mradi.
 
Waimba kwaya hata kukusoma hawataki, hilo ndilo tatizo kubwa sana nchi yetu ililonalo sasa hivi.

Kila kitu kinatazamwa kwa mlengo wa sisi au wao, sio kwa taifa letu. Inasikitisha sana.

Mada kama hii haistahiri kuwekwa uCCM au upinzani hata kama imeletwa na mtu kama Zitto.
 
Hongo kama "u-Profesa"?

Tatizo lililopo sote humu ndani tunajadili tu bila ya kujua masharti yaliyoambatana na ujenzi na uendeshaji huo.


Hoja ya kusema tu 'waChina ni hatari' haituongezei ufahamu wowote juu ya nini kilichotokea hadi serikali ikaghairi kuruhusu.

Mimi nadhani tuwe ni watu wa kujiamini sasa, tuache hizi tabia za kujiona sisi ni watu tunaoyumbishwa tu kirahisi. Hatuwezi kila mara kuingia kwenye mikataba tukiwa na hofu kwamba tunapigwa, tunaibiwa. Kwa nini tuibiwe, kwani hatuna akili za kufikiri, kutambua na kujua maslahi yetu ni nini?

Mpaka hapo itakapojulikana ni sababu zipi hasa zimefanya mradi usifanyike, sio busara kurukia tu kwamba ni kwa sababu ya 'wachina kuwa hatari'.
 


Hivi ulishatoa mchango wa mafuta ya mwenge ??
 
Nyinyi ndio wale watz wachache mnaotegemea akili za mtu kuishi.

Yaani kila mtu unataka akubaliane na huyo zitto, kwanini una imani naye kiasi hicho!!!

Kwenye hili swala mnaonyesha upumbavu kiwango sana bila kusita.

Huo mradi aliuanzisha Zito ??
 


Umesoma vizuri au tumbaku ya Chato imekuzidi ?? Bandari ni sehemu tu ndogo ya mradi , soma tena baada ya nishai kukutoka
 
Ngoja nikasome kwanza ile habari ya speaker kushangaa mradi huu kusitishwa ndio nirudi hapa
 
Waambie hayo masharti magumu watu watoe maoni yao, waambie ukweli mda wa wachina katika uwekezaji wa huo mradi ni mpaka miaka 99, tena ukiwa na conditions za kukataza bandari zingine kuendelezwa. Wape na mifano ya miradi kama hii iliyofanyika nchini Eritrea na baadhi ya nchi za Asia ni jinsi gani walifaidika?? Weka wazi masharti hayo ya mikataba..

Wachina wa leo ni hatari kuliko hata mabepari wa kizungu, ukiona mpaka trump anawawekea vikwazo kwa kupandisha kodi kwenye bidhaa zao ujue kuna kitu, hakuna sehemu ambayo serikali inapata pesa nyingi kama bandarini, ikijengwa bandari ya b moyo automatically utaua bandari ya dar. Yaani utacha mapato ya uhakika utaenda kuchukua kodi kwenye biashara ambayo mpaka ipate faida ndo walipe kodi.

Hakuna asiyejua makampuni makubwa yanavojua kucheza na mahesabu kukwepa kodi, kwenye hili naipongeza serikali. Hakuna haja ya haraka kwenye mradi huu. Wasomi wauchambue, usalama wa taifa wauchambue, wabunge na wadau waupitie.... then serikal ifanye maamuz
 
Kuna mtu anataka kuwafanya watz wajinga na serikali yote, ila yeye tu ndiye anafikiri sawa sawa.
 
Tatizo sio mradi tatizo ni aina ya mkataba ambao haukuonyesha matunda kwa Taifa, pili ni akna zitto hawahawa waliupinga huu mradi na kusema ni wa kinyonyaji na kushauri ufanyike upanuzi wa bandari tu.
 
Huu ni ulimwengu wa biashara ya kutengeneza faida,awe Mchina Mmarekani Mwarabu Mwafrika popote anapoingia ni kwa ajili ya maslahi yake sio yako.
Kwa hiyo Mchina asibebeshwe lawama waliobuni mradi ni sisi wenyewe si ajabu na wanaoukataa mradi huu wana maslahi kwenye miradi wanayotaka kuianzisha.
 
Hatuwezi kujua yote yaliyojificha kwenye mradi huu.
Haya yanaweza kuwa moja ya sababu ya Serikali ya sasa kusitisha mradi huu.
1. Gharama za mradi kutokuwa halisi (inflated costs).
2. Maamuzi ya kuujenga mradi huu Bagamoyo una personal goals/ uzawa kwa sababu Rais aliyekuwa madarakani kwao ni Bagamoyo.
3. Harufu ya ufisadi.
4. Kuvunja miiko ya kiuchumi hata ile ya Inchi za Kibepari kwa kuruhusu Inchi nyingine kumiliki Ardhi na Bandari ya Taifa lingine.
Kwa namna yoyote ile Rais aliyeko madarakani ana washauri makini sana katika mambo makubwa kama haya ya uwekezaji kwa hiyo hawezi kutelekeza mradi mkubwa ambao una maslahi kitaifa ndani ya muda mfupi.
 
kuna vitu ndugu zito umezungumza kwa kutumia hisia na sio utaalam...swala mahusiao mema haliwapi mamlaka wachina kututawala.
 
Inchi za Africa zitaendelea kupata matatizo ya uwekezaji katika miradi mikubwa kwa sababu kila Rais anyeingia madarakani anakuja na vipao mbele vya kwake.
Ifike mahali Tanzania tuwe wa kwanza kuwaondolea Marais kubuni miradi mikubwa kadri ya matakwa yao.
Kuwe na chombo maalumu cha kikatiba cha kuandaa miradi na mipango mingine ya maendeleo ya Inchi ya muda mrefu na mfupi ambayo itakuwa inapitishwa na Bunge na kuwa kama sheria ili Rais anayeingia madarakani awe na jukumu la kutekeleza tu badala ya kuacha miradi ya aliyemridhi na kuanzisha ya kwake.
Jambo linguine muhimu la kitaaluma ni kuwa miradi mikubwa ikifanywa kisiasa inaweza kuyumbisha mzunguko wa pesa na kuharibu uchumi wa Inchi. Pesa ikizidi sana ndani ya mzunguko ni mbaya pia pesa ikupungua kwenye mzunguko inaharibu uchumi wa Inchi na kufanya wafanyabiashara na Mabenki mengi kufilisika.
Ni lazima uwekwe uwiaano wa kitaalamu kuhusu money circulation ambao Benki kuu itahakikisha hauyumbi.
 
Zitto, mradi huu kweli ulikuwa na faida kubwa - kasoro yake ni kuwa ulipaswa kuwepo na ubia wa nchi tatu (Tanzania, Oman, na China) vinginevyo kama ungetekelezwa sisi faida yetu ingetoka kwenye eneo la Multiplier effects na si direct benefits ya kodi, na ajira
 

Mkuu umesahau kuw ahii ni GRANTS!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…