Waambie hayo masharti magumu watu watoe maoni yao, waambie ukweli mda wa wachina katika uwekezaji wa huo mradi ni mpaka miaka 99, tena ukiwa na conditions za kukataza bandari zingine kuendelezwa. Wape na mifano ya miradi kama hii iliyofanyika nchini Eritrea na baadhi ya nchi za Asia ni jinsi gani walifaidika?? Weka wazi masharti hayo ya mikataba..
Wachina wa leo ni hatari kuliko hata mabepari wa kizungu, ukiona mpaka trump anawawekea vikwazo kwa kupandisha kodi kwenye bidhaa zao ujue kuna kitu, hakuna sehemu ambayo serikali inapata pesa nyingi kama bandarini, ikijengwa bandari ya b moyo automatically utaua bandari ya dar. Yaani utacha mapato ya uhakika utaenda kuchukua kodi kwenye biashara ambayo mpaka ipate faida ndo walipe kodi.
Hakuna asiyejua makampuni makubwa yanavojua kucheza na mahesabu kukwepa kodi, kwenye hili naipongeza serikali. Hakuna haja ya haraka kwenye mradi huu. Wasomi wauchambue, usalama wa taifa wauchambue, wabunge na wadau waupitie.... then serikal ifanye maamuz