Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

So sad kwamba pamoja na uchambuzi wa kina uliofanywa kwenye uzi huu hujaelewa chochote, na bado umefanya kosa lile lile la kudhani huo mradi ni bandari tuu. Kwa nini hamsomi mada mkaelewa kwanza? Mnajidhalilisha sanaa...
 
kichwa maji kweli wewe unasoma kwa kuruka ruka kukimbilia dirashani kupanga foleni kwa ajili ya buku saba. Huo mradi wa bagamoyo ni uwekezaji sio kwamba nchi inatoa kila kitu toka mfukoni mwake zaid ni hao wachina ndo wanahusika kurun hiyo project
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kudeal na.china kunahitaji watu makini na kama huyu muonyesha njia angekuwa makini angeluona na hilo akajua pesa nyingi za china zinazokuja adrika zina madhara makubwa kuliko faida sijaisoma yote ila pia achambue faida itakayopata nchi ikilinganishwa na faida wanayovuna wawekezaji. Zama.za awamu.hii ni win win
 
Braza kuna bandari tatu kubwa nchini, na uzuri zote zipo kwenye kanda na location kimkakati kabisa.

Leo hii zitto angekuja kuandika kuzihusu hizi bandari ningeona maono chanya juu yake, lakini kama kawaida, vile hayana faida kwake kisiasa, hana muda nayo.

Dar port, iko kwenye upanuzi, mtwara hivyo hivyo, tanga nayo iko kwenye hatua, na katika hizo hakuna yenye kufanya kazi kwa uwezo wake hata 70%.
 
Nimekuelewa sana kuweka mpira kwapani haikuwa njia sahihi.
 
Nyinyi ndio wale watz wachache mnaotegemea akili za mtu kuishi.

Yaani kila mtu unataka akubaliane na huyo zitto, kwanini una imani naye kiasi hicho!!!

Kwenye hili swala mnaonyesha upumbavu kiwango sana bila kusita.
Mtu yeyote akiwa na hoja zenye mashiko anakubalika... Mtu hapendwi au kuaminika kwa uzuri wake au kuongea sana bali kwa kuleta hoja zenye mashiko.
 
Kama mna eneo lenu mnaweza wapa hao wachina wajenge, wapeni.

Hizi siasa uchwara zinazokwenda na matukio, zinahitaji backup za wasio na misimamo kama wewe.

Zitto hawezi kuwa mshauri mzuri wakati wote.
Ndipo uwezo wenu wa kufikiri unapokomea... hebu soma kilichoandikwa na ZK kisha ucomment tena... mbona la koroshow umeliruka?
Wazee wa "ndiyooo..." kila jambo mna msimamo sana 😆😅😅
 
Wewe jamaa hujaelewa kitu bora ukae kimya
 
So sad kwamba pamoja na uchambuzi wa kina uliofanywa kwenye uzi huu hujaelewa chochote, na bado umefanya kosa lile lile la kudhani huo mradi ni bandari tuu. Kwa nini hamsomi mada mkaelewa kwanza? Mnajidhalilisha sanaa...
Kuna mtu katoa uchambuzi mzuri kasome uelewe kwa kifupi huo mradi Ni Kama ambao tunasikia yanayotokea Kenya, Zambia na nchi nyingine duniani ambako wachina wamewekeza kwa stail hiyo
 
Unadhani hajui braza, huyu jamaa ni opportunist tu kama wengine tunao wakataa humo kwenye system.

Mchina ni wa kujiaminisha utashindana naye kibiashara[emoji23][emoji23], aulize kenya na sgr yao.
 
Financer wa mradi 100% ndio hafai.

Umesoma uchumi wapi nyumbu wewe!!!

Maana yake hiyo bandari ni mali ya hao wachina 100%, unajua madhara yake, au mauno tu kama kawaida yenu!!
Unaonekana ni so layman kwenye haya mambo...
 
Wewe ni useless ! Elimu za kukariri !
Unaambiwa Uwekezaji wa Bagamoyo si Bandari pekee in pamoja na viwanda!
Lakini ita create link na SGR na italeta tija zaidi.
 
Mkuu embu soma tena hiyo article kama hutojali.
 
Sina haja ya kwenda kusoma coz nina uelewa wa kutosha... Narudia kama hukielewi kitu bora kunyamaza ni busara zaidi...
Kuna mtu katoa uchambuzi mzuri kasome uelewe kwa kifupi huo mradi Ni Kama ambao tunasikia yanayotokea Kenya, Zambia na nchi nyingine duniani ambako wachina wamewekeza kwa stail hiyo
 
Kuna mtu katoa uchambuzi mzuri kasome uelewe kwa kifupi huo mradi Ni Kama ambao tunasikia yanayotokea Kenya, Zambia na nchi nyingine duniani ambako wachina wamewekeza kwa stail hiyo
Achana na vilaza hao wafuasi watiifu.
 
Nadhani mjadala huu ni mkubwa sana kuushinda uwezo wako, tafuta mada nyingine ya uwezo wako "uirukie".
Unadhani tu!!!

Kawaida ya nyumbu hufuata aliyetangulia, hata akipita walipo mamba, wengine watafuata, kama wewe mkuu.
 
Pamoja na maelezo mareefu ya Bw. Zitto ameshindwa kutueleza baada ya kukamilika kwa huo mradi Tanzania itamiliki asilimia ngapi, China asilimia ngapi na Oman nao watakua na asilimia ngapi. Hizo faida nyingine za kiuchumi kama ajira n.k haziwezi kuwa na manufaa zaidi kuliko umiliki wa bandari unaoingiza faida kubwa.

Viwanda vyote vitakavyojengwa ni vya kwao, ina maana uchumi wote utakaondeshwa hapo ni wa kwao. Kama nchi ilibidi kujipanga kwanza kwa kuchangia gharama za mradi, let's say katika trilioni 23 angalau sisi tuwe na mtaji wa trilioni 13 then hizo 10 tuwaache wao wachangie kila mmoja atoe trilioni 5. Then tuwe na mtaji mwingine wa ardhi yetu tutakayotoa kwa ajili ya huo uwekezaji. Hayo yakifanyika tutakua na uhakika wa kusecure asilimia kubwa zaidi ya kumiliki bandari na hivyo kupata faida kubwa kama nchi kutokana na shughuli za bandari.

Kwenye Viwanda watavyoanzisha, hatutokua na shida hata wakichukua vyote. sisi tutahitaji tu ajira kwa watu wetu pamoja na kupewa kodi yetu stahili kutokana na bidhaa zitakazozalishwa. Kinyume na utaratibu huu, kuiacha bandari imilikiwe na wageni ni sawa na kurudi kwenye ukoloni. Huwezi kuacha nyanja kuu za kiuchumi za nchi yako zimilikiwe na wageni hata siku moja. Dunia nzima itatucheka hata kama kuna faida kiasi gani.

Wachina wasasa sio wale wa enzi za mwalimu nyerere (communist) hawa wasasa ni mabeberu kama mabeberu wengine. Yaani Ujamaa china umebaki kwenye masuala ya kisiasa tu lakini kwenye uchumi hawana ujamaa ndo maana nchi kama Sri Lanka na Kenya zinalia kutokana na mikopo yenye riba kubwa kutoka China tena yenye masharti magumu. China sasa hivi anafight kuwa Super Power against marekani na target yao kubwa ni Africa kwenye mabongo lala na Viongozi wenye tamaa kama Zitto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…