Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Huyu mh ni tabu sana. Jambo dogo kama hili pia hajachunguza.
 
Ingependeza mjadala huu kuwa kwenye thread ya mtoa hoja (ZZK) ili kama kuna material facts ambazo mtu anazo azitoe ili watu wazifahamu na mjadala uendelee. Ila ni vizuri watu wajadili hoja na si kuwajadili au kubeza watoa hoja.

Lakini ni vizuri pia tujipime pia jinsi tunavyo handle wawekezaji wetu. Isije ikawa kuna mambo pia ya uadilifu kama alivyo sema waziri wa uwekezaji kule Kigoma. Watu wanaweza kuangalia hizo Trillion 23 na wakajiwazia kama wao wana achajwe??!! as waliojadili mwanzo ni wengine 😂? just Kidding!!!
 
Nyinyi ndio wale watz wachache mnaotegemea akili za mtu kuishi.

Yaani kila mtu unataka akubaliane na huyo zitto, kwanini una imani naye kiasi hicho!!!

Kwenye hili swala mnaonyesha upumbavu kiwango sana bila kusita.
Zitto ni opportunist anayedakia jambo kwa maslahi yake binsfsi, ila anajificha kwenye hoja ambayo inasisimua ili kuvuta watu hasa wasioelewa kwa kina. Hakuna mweke
 
Serikal haitoi hata senti kwenye huo mradi.
 
Perfect. Tatizo ni nn? Kwanini tunasitisha? Hizo sababu ni sahihi? Wanaotaka uendelee wana maslahi binafsi na si ya kitaifa? Haya majibu yote yanapatikana tukiona content.
 
Makala ndefu iliyojaa pumba. Mkataba ulisainiwa na CCM, iwe Kikwete au Magufuli wote ni viongozi na wanachama wa chama chenu cha majambazi. Badala ya kukosoana wenyewe, mmepata pa kulaumu kwa kumnyooshea kidole Zitto
 
Mh Zitto. Anamatatizo ya kulaani kila kitu kinachoanzishwa na serekali hii. 1,Bombardier Q400 akisema ni mtumba ulikuwa ya Kaz...... 2, Boieng 787 - Dre. ... Eti ulikuwa ni mtumba iliyokataliwa. Bombardier CS300 kwa sasa Airbus 220-300 akisema ni ndege ambazo azijulikani duniani.. Atakaruditena na Bwawa la Rufiji na mazingira. Tukumbuke wakati walipoazisha huo mradi wa bagomoyo alilipinga sana akitaka upelekwe kigoma. Sasa anaupenda. Walipiga kelele kuhusu ATCL sasa wanasemaje eti tungejenga mahospatali nk
 
Financer wa mradi 100% ndio hafai.

Umesoma uchumi wapi nyumbu wewe!!!

Maana yake hiyo bandari ni mali ya hao wachina 100%, unajua madhara yake, au mauno tu kama kawaida yenu!!
Kwani mwekezaji anapokuja kuwekeza hela si zake serikali yenyewe huchukua kodi yake kikamilifu
 
 
Watasema unatumika na mabeberu,sasa hapa ni china na oman
 
Mbona uwanja wa ndege hankukutaaa,zito anasema faida ambazo nchi ingezipata na sio kua mradi unakwenda bagamoyo.Na pesa hizo anazosema za kukamilisha mradi huo ni za mwekezaji mwenyewe ambae angewekaza kwa muda maalum ila kodi,ajira zingebaki kuwa za kwetu.ameeleza vema sana,sema kasema Zito angesema wa kutoka ccm angeungwa mkono
 
Weka audio bwana! Alafu mimi napenda uhusiano wetu na China uharibike ili jiwe ajali haki za binadamu maana China ndio wanampa kiburi
 
Mkuu original poster ahsante sana kwa kuchukua muda wako na kujibu hawa wanasiasa vijana ambao wananifanya nidoubt sana our next leaders, God forbid.
Huyu zito hafai kabisa aise, sijui ni anahongwa au ni ujinga.
 
Twende Mbele turudi Nyuma, hili ni kosa kubwa serikali ya awamu hii ya tano imefanya, Tanzania ambayo inataka kukua kiuchumi Zaidi haiwezi kuwa inaogopa ushindani, hoja ya kusema china itataifisha bandari tukishindwa kulipa ni hoja totally mfu, mfu kabisa,mawazo ya kimasikini kabisa, sisi tumetoa eneo la uwekezaji tu, mtaji unatoka china/Oman,hata kama china/oman wataendesha hiyo bandari kwa muda ya miaka kadhaa ni sawa, serikali wao watakuwa wanapata mapato, ajira zitaongezeka kwa vijana, bagamoyo ingekuwa na kuwa center ya usafirishaji wa bidhaa katika ukanda huu wa EAC nad nchi nyingi za kusini,ukisimamisha mradi huu kwa woga wako kuwa eti bandati yetu ya Dar itakufa au kukosa mizigo huwakomoi wachina, unakomoa wananchi wako, unajikomoa wewe mweyewe na serikali yako kwa kukosa mapato, unajirudisha nyuma wewe mwenyewe katika dhamira ya Tanzania ya viwanda,tuacheni kuogopa kwa kila jambo, nature ya Zambia na srilanka ni tofauti na Tanzania, kwa hili Zitto Kabwe yuko sahihi Zaidi 100%, Magufuli aangalia upya maamuzi yake, ni bora aangalie jinsi ya kukutana na Rais mwenzake wa china kwa majadiliano Zaidi.
 
Hata mimi najua details za majadiliano haya,

Ulichokosea ni kutumia muda mwingi kumjadili Zitto badala ya kujadili hoja zake.

Lingine ambalo tumeshindwa kwenye diplomasia. Ilishajulikana tofauti kati yetu na Wachina na watu wengi walishauri hizi tofauti zote zitaisha kwa rais Magufuli kwa kukutana na rais wa China.

Lakini sisi tumeshindwa kufanya hivyo na matokeo yake tumeshindwa kutumia ukaribu wetu na China kuhakikisha kama nchi tunafaidika bila ya kuathiri Uhuru na usalama wetu.
Majadiliano yetu na China yameishia ngazi za civil servants na hilo ni kosa la kidiplomasia.
 
We jamaa huwa huna akili. Sijui ulikuaje usalama wa taifa kilaza hivyo? Mi nadhani ungejibu hoja tu lakini kuandika ulichoandika ni uthibitisho wa kukosekana watu wenye akili usalama wa taifa. Yaani unazidiwa mpaka na akina mange?

Mi huwa nakusoma sometme post zako na insta nakuona mweupe sana kwa hoja,uelewa na ufaham. Badilika chahali ndo maana unakosa hata kuwa na watu ambao ni credible kuku back up.


Makala ndefu iliyojaa pumba. Mkataba ulisainiwa na CCM, iwe Kikwete au Magufuli wote ni viongozi na wanachama wa chama chenu cha majambazi. Badala ya kukosoana wenyewe, mmepata pa kulaumu kwa kumnyooshea kidole Zitto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…