Kusoma na kuishi nje ya Afrika

Kusoma na kuishi nje ya Afrika

365

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2014
Posts
1,377
Reaction score
1,456
Heshima kwenu wote.
Napenda Uzi huu uwe maalum kwa watu walioko Tanzania na nje ya Tanzania, dhamira kuu ya Uzi huu ni kuwakutanisha watu wote wenye nia ya kwenda kusoma nje ya Africa na pengine kuishi huko sababu dunia ni Mali ya binadamu wrote.

Kwa maana hiyo mtanzania ulieko nje nchi hii au bara hili tunaomba utusaidie mawazo na mbinu ulizotumia kufika huko ughaibuni na Wewe mtanzania ulieko Tanzania useme una mikakati gani kwenda ughaibuni.

Kumbuka kila mtanzania anatakiwa akatafute elimu kila kona ya dunia ili upate maarifa na ujuzi mpya na wenye tija ili urudipo Tanzania usaidie nchi yako haiwezekani tuzidi kurudi nyuma wakati nchi nyingi zinaenda mbele karne hii ya 21.

Zingatia kuruani tukufu inasema mtafute elimu hata kama itakua UCHINA na Biblia takatifu inasema mshike sana elimu maana huo ndo uzima wako.

Mimi binafsi bado Niko Tanzania ila kila siku nafanya harakati za kwenda kutafuta elimu nje ya Tanzania.

Naomba kutoa hoja na karibuni kwa mawazo na mipango yenu.
 
Ikiwa walengwa ni walio na mpango wa kuishi nje ya Afrika huoni ungefungulia uzi huu huko huko nje ya Afrika?
 
Mleta uzi HAKUNA MAHALA POPOTE KATIKA QURAN palipoandikwa hivyo. Next time fanya research kabla hujaandika. Andika unachokijua TU.
 
Mwalimu qliyekufundisha hadi hapo ulipofika alisoma nchi gan tofauti na tz, dr anaekutibu hospital amesoma nchi ngqpi tofauti? Sidhani kama nje kuna kilicho bora zaidi ya ndani ila tu kule unasoma vitu vikubwa ambavyo ni lazima ufanye kazi na wao baada ya kumaliza cz huku kwetu havina application!! Ila samahani mimi sijawahi kusoma nje ya tz from nursery mpaka leo nafanya kazi
 
Xiexie ulizia vizuri
 
# Moe Junior Elimu tunayopata nchini haijatuletea mabadiliko chanya ndo mana nchi ni tajiri ila watu ni masikini,sasa lazima tukajifunze mbinu walizotumia wenzetu kuowanisha Mali za asili kama aridhi,misitu,mafuta,mito,maziwa,madini n.k na watu wake.zingatia mi nataka tukajifunze mbinu tukiwa katika mazingira yao tuone bayana wanavyofanya.
 
Wenje nia njema watatoa mawazo usijal mkuu...Achana na hizo kelele za hapo juu..Mimi binafsi natamani sana kusoma nje hata kuishi nje pia..Sijui pa kuanzia lakini itawezekana siku moja 365
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom