Kusoma Postgraduate (Master/PhD) UDSM majanga

Kusoma Postgraduate (Master/PhD) UDSM majanga

Hata Mimi nilikua na wazo la kufundishwa software nikiwa pale jalalani 😂. Lakini nilivyohitimu nikaja kushtuka aiseee, unaweza fundishwa software toka module ya kwanza mpaka unavaa joho maana software ni nyingi na zote za muhimu kwenye field Yako. Just imagine kwenye topic Moja Kuna kama software 5. Nadhan wanafunzi pana haja ya kujibidisha mbali na kile anachokupa mwalimu.
Na hapo ndio vijana hawataki kujiongeza kujifunza vitu vya ziada...utafundishwa ngapi Sasa na siku wa kukufundisha hayupo utafanyaje?
 
Na hapo ndio vijana hawataki kujiongeza kujifunza vitu vya ziada...utafundishwa ngapi Sasa na siku wa kukufundisha hayupo utafanyaje?
Mkuu vijana wa saivi tuna shida zetu nyingi sana japo hatuzijui wenyew. Siku zote kitu Cha kujifunza mwenyew kinaeleweka vizuri kuliko Cha kufundishwa, ndy kazi ya mwalimu ni kumfundisha mwanafunzi lakn sisi hatujibishi kujifunza.
 
Mkuu hiyo R unaweza kufundishwa lakini usije kutuma Maisha yako yote..mfano mtu wa molecular dynamics naye unataka atumie R kwenye kazi zake? Huoni Kama inategemea na field ya mtu?
R programming inatumika kwenye kila fani hata music watu wanaandika codes wanatengeneza different musical sounds na kuzimanipulate kwa namna ambayo hakuna software inafanya. Inatumika sana pia kwenye biochemistry na molecular biology, nanotechnology, etc.
 
R programming inatumika kwenye kila fani hata music watu wanaandika codes wanatengeneza different musical sounds na kuzimanipulate kwa namna ambayo hakuna software inafanya. Inatumika sana pia kwenye biochemistry na molecular biology, nanotechnology, etc.
Basi kama ni hivyo tusingeshuhudia software nyingine zinauzwa mpaka dollar elfu kumi kaam hiyo inafanya Kila kitu.
 
Basi kama ni hivyo tusingeshuhudia software nyingine zinauzwa mpaka dollar elfu kumi kaam hiyo inafanya Kila kitu.
R ni open platform inatumika sana kwenye research na ipo very robust na ina thousands of developers katika kila field kwani ni open platform. Kama wewe unfanya coding unaweza kuingia kwenye developers site ukaandika code za kufanya statistics za fani yoyote tu. It's very unique yet free!
 
Hahahaa nakumbuka kipindi Prof. Adolf Mkenda waziri wa elimu kipindi hicho akiwa mkuu wa idara ya uchumi kuna mdada mmoja alikuwa mwanafunzi Ph.D Economics kutoka Kenya aliangua kilio ofisini kwake baada kupewa stress za kutosha na supervisor wake nafikiri alikuwa Pro. Nehemia Osoro.
Osoro huyu aliyekula uteuzi enzi ya jiwe...?
 
Sir

e hakuna kitu nilichukia kama ufundishaji wa statistics pale Mlimani. Ni kama ulivyosema lecture anakomalia historia ya statistics na nadharia nyingi na kufanya statistics kuonekana ngumu mno.

Hakuna matumizi ya modern statistics softwares tena nashangaa kama bado watu hawafundishwi softwares kama R, Matlab, SPSS, nk! Ufundishaji wa hovyo sana huo na haunsaidii mwanafunzi.
Heeeee serious! Basi mnajitesa na mavyeti bure tu! Ukisoma online ukapata sehemu ya kupatia expirience, kwenye haya mashirika kazi unapata vizuri tu na hamna mwenye atakuomba cheti.

Labda kama focus ni kuwork for government.

Watu wamesoma BBA, ualimu, sociology, computer science, IT etc na wanapiga fresh tu statistical analysis.

Historia ya statistics ya kazi gani jamani ulimwengu wa leo??? 😅 Bora module iseme mkapitie historia ya statistics sio muisome muikariri na muijibie mtihani!!! Haina maana wala haina kazi!

Ndio maana people are going for short courses. Hakuna interview ya “maana” utaulizwa historia ya blah blah gani sijui!
 
Kwa hiyo inamhusu nini mhadhiri ambaye naye anawakuta tu wanafunzi darasani?...nimekupa kazi uniletee ratio hujaleta unaanza leta hoja nyingine...tuache ujanja ujanja watanzania tunawekeza kwenye siasa halafu tunataka kuvuna kwingineko...wewe baada ya kuhitimu MSc kwa nini hukubaki idarani kwako utatue hizo changamoto ukakimbia. Ungeongea na superior wako angekuambia yanayowasibu wanataaluma.
Kama mwajiri anaona mwajiriwa hafanyi kazi vizuri kwa nini hamfukuzi kazi? Iulize serikali yako hilo swali sio yule unayemtuhumu kutotenda kazi vyema.
Sasa wewe si umesema ratio ya hicho chuo Cha nje ungeleta hapa, hafu ka kazi ngumu si muache na mlalamike Kwa wahusika wanafunzi inawahusu nini.
Hafu nibaki huko kufanyaje nizeeke na ku cremisha madesa wanafunzi with zero impacts ya nini?
Naenda kwenye taasisi na international organization kule Kuna mazingira mazuri ya kazi na kupata exposure kubwa na ukifanyacho unaona real impacts.
Nyie wa vyuoni mnajionaga na akili na GPA za kubebana kikabila pambaneni na hali zenu bwana muendelee kutesa wanafunzi.
 
Sasa wewe si umesema ratio ya hicho chuo Cha nje ungeleta hapa, hafu ka kazi ngumu si muache na mlalamike Kwa wahusika wanafunzi inawahusu nini.
Hafu nibaki huko kufanyaje nizeeke na ku cremisha madesa wanafunzi with zero impacts ya nini?
Naenda kwenye taasisi na international organization kule Kuna mazingira mazuri ya kazi na kupata exposure kubwa na ukifanyacho unaona real impacts.
Nyie wa vyuoni mnajionaga na akili na GPA za kubebana kikabila pambaneni na hali zenu bwana muendelee kutesa wanafunzi.
Haya sawa kama hujui wanafunzi ndio wahusika wenyewe.
 
Tatizo ni mfumo wetu wa Elimu haujakaa sawa bado. Kwa postgraduate studies nikianza na Masters wanatakiwa wawe attached kwenye research projects za taasisi ama za department. Ni lazima taasisi kupitia idara zao wawe na projects zinazohusiana na degree programs wanazotoa. Hatuwezi kua na wanafunzi kila mmoja ana title yake bila hata kujali kama ina potential yoyote kwa taasisi husika, jamii na taifa kwa ujumla. Ina maana idara kupitia wataalamu wao Doctors & Professors wanatakiwa kua na miradi ambayo wata attach wanafunzi hiyo itarahisisha usimamizi na wanafunzi kumaliza haraka maana wakati mwingine mwanafunzi anakuja na title ambayo hata supervisor wake haielewi vizuri au hana interest nayo so inasababisha mvutano na mwanafunzi wake na kupelekea kuchelewa kumaliza kwa wakati. Lakini pia kupitia hizo projects wanafunzi wa PhD watawasaidia wa Masters na Bachelor degree kwasababu wanashare the same idea so itapunguza mzigo kwa supervisors. Sasa hapa tatizo ni wataalamu wetu ni wavivu wa kufikiria katika angle tofauti maana wanatakiwa waandike proposals kutoka kwenye funding organizations domestically and internationally ili kupata pesa za kuanzisha na kuendeleza miradi hii. Wao wamekalia kushindana kuandika papers ili wapande vyeo tu na kupata mishahara mikubwa wakati hizo papers hatuoni impact yake kwenye kutatua changamoto za jamii. Natamani nikutane na Rais pamoja na waziri wa Elimu nimshauri kitu kuhusu mfumo wa uendeshaji wa postgraduate studies kwa vyuo vyetu hasa kwa programs za science, engineering and technology. Hakuna muunganiko kati ya Elimu inayotolewa vyuoni na technology inayotumika viwandani. Huwezi kua na maendeleo ya technology kwenye viwanda kama hakuna hiyo connection. Research zinazofanyika vyuoni lazima ziliflect challenges kwenye sector ya viwanda ili tuweze kupiga hatua. Ni lazima kila chuo kiwe na industrial center ambayo itahusisha research, innovation na majaribio mbalimbali ya technology katika sector husika. Ina maana viwanda vitashirikiana moja kwa moja na vyuo kwenye hizo tafiti na zitatoa funds pia kusapot tafiti na majaribio hayo ya technology hapo itakua rahisi hata mwanafunzi kuajirika hata nje ya nchi baada ya masomo yake. Anyways niishie hapa kwa leo!!
Wazo zuri sana
 
Vipi wanaotaka managerial positions?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani elimu kubwa sana ina umuhimu kufika ngazi hizo? Taasisi au kampuni zote duniani zinazofanya vizuri vyeti vyako watu wataviangalia ngazi ya entry level ila kuanzia hapo hamna atayetaka kujua umesoma mpaka ngazi ipi. Kitu cha muhimu watu watataka waone kazi ulizowahi kufanya na sio elimu yako.

Unafikiri kampuni kama Benz au Apple wakitaka chief designer watataka kujua umesoma mpaka Master's /Ph.D? Wao kitu cha msingi ni kazi zipi umewahi kufanya. Hata hapa hapa bongo maeneo wanayojielewa elimu sio hoja. Vodacom waliwahi kuwa na CEO mwenye umri chini ya miaka 30 na alikuwa na shahada moja tu. Baada ya yeye kuondoka walikosa mtu hapa wakatafuta kutoka nje.
 
Back
Top Bottom