Nikiwa Ubungo Riverside, nimebaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya uondoaji wa taka ambapo huduma hiyo imekuwa ya kusuasua kwa muda sasa. Hali hii imesababisha taka kurundikwa kando ya barabara na katika maeneo ya makazi kwa siku nyingi bila kuondolewa.
Wakazi wa eneo hili wanasema taka hizo zinasababisha harufu mbaya, kuvutia nzi na wadudu wengine wanaoweza kusababisha magonjwa. Wameeleza hofu yao kwamba endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, eneo hilo linaweza kukumbwa na mlipuko wa magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na kuhara.
Mbali na athari za kiafya, taka hizo zimeendelea kuharibu mazingira na kuathiri shughuli za kila siku za wananchi. Wakazi sasa wanatoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha huduma ya ukusanyaji na uondoaji wa taka inaboreshwa ili kuzuia madhara zaidi.
Pia soma
~ Rais Samia: Dar es Salaam ni kuchafu, ni aibu
~ DC Mpogolo: Atakaye tupa taka Ganda la Ndizi na Pipi faini Milioni 1, Dar