Kusudio langu la kupata suluhisho la kudumu la mgogoro wa wapalestina na wayahudi

Kusudio langu la kupata suluhisho la kudumu la mgogoro wa wapalestina na wayahudi

Umeshindwa kushauri CCM ikakusikiliza ndio Netanyahu akusikilize 😅 😅

Kwanza itakuwa humjui waziri wa Ulinzi wa Israel alivo na roho ngumu
 
Unaweza ukawashuruhisha watu waliomuua mwana wa mungu wa pekee? Jiulize Yesu alikuwa na tatizo gani mpaka akasulubiwa na kuuwawa?
Si wote waliohusika kumuua. Walikuwepo Wayahudi wengi tu waliomwamini na kumfuata, na hata sasa wapo.
 
Umeshindwa kushauri CCM ikakusikiliza ndio Netanyahu akusikilize 😅 😅

Kwanza itakuwa humjui waziri wa Ulinzi wa Israel alivo na roho ngumu
Namjua sana, Yoav Gallant. Sijawahi kushindwa kuwashauri, labda wao wameshindwa kunisikiliza na kunielewa. Nafanya vivyo hivyo kwa washindani (mnaita wapinzani).
 
Shida ni kuna watu hawataki mgogoro uishe ...
Kuna watu wanafaida sana na hivyo vita mfano Hamas viongozi wao matajiri haswa mfano yule aliuwawa alikuwa bilionea na alikuwa anaishi maisha ya kifahari mno...
 
Uko sahihi sana. Unamwongelea Ismail Haniyeh aliyeuwawa Teheran nchini Iran. Aliyechukua nafasi yake sasa ni Yahya Sinwar
 
Mara kadhaa nimewahi kushiriki na naendelea kushiriki kutoa maoni ya kusuluhisha mgogoro mkongwe na mgumu mno wa Wayahudi na Wapalestina.

Kwa ujasiri mkubwa kabisa, nisisitize kuwa nakusudia na niko tayari kabisa kusuluhisha mgogoro huu kwa niaba ya Afrika na Waafrika wote, hata kama sina cheo chochote. Ilmradi tu nina "Suluhisho la Kudumu" ambalo ni kuwa na nchi moja ya Wapalestina na Wayahudi, wakiishi kama majirani na ndugu wa asili moja ya Ibrahimu (kinasaba na kieneo).

Jina la nchi liwe Middle East au Ibrahimu au lingine lolote litakalokubalika na kuwafaa wote.

Hakuna mpalestina au mmyahudi hata mmoja mwenye asili ya Afrika, Asia, Ulaya au Amerika - wote ni wa Mashariki ya Kati kutoka mtoni (Jordani) hadi baharini (Mediterranean) - ni ndugu hawa.

Tuanze sasa, leo hii; kupanda mbegu ya kupendana wao kwa wao, na kwa watoto, na watoto wa watoto wao; si kuchukiana pasina mwisho.

Adha, tuelewe kuwa dunia nzima kwa sasa tumechanganya sana damu kwa watu wengi, na tunaishi kila mahali kwa amani, japo bado kuna ubaguzi tunaoendelea kupambana nao. Kuna Wayahudi wenye asili ya Afrika na Waafrika wenye asili ya Kiyahudi (wengi wao wako Ethiopia).

Kwa wasiojua, kuna Wayahudi waliooa Wapalestina, na Wapalestina waliooa Wayahudi akiwemo hayati Yasser Arafat! Nina mdogo wangu wa karibu mno ambaye ana damu ya Uafrika (Nigeria na Afrika Mashariki), Uarabu na Uyahudi; lakini anaishi Ujerumani. Haungi mkono vita yoyote, uonevu wowote au dhuluma yoyote, isipokuwa haki na maridhiano.

Afterall, everyone is a rightful citizen anywhere in this world. And the reality is that, we don't own this world, but it owns us - it swallows all of us! We are just passersby.

Tupendane, tuheshimiane, tujaliane na tuishi popote duniani pasina kubaguana. Tofauti zetu za rangi, imani za kidini, uasili au hali ya maisha si kitu, bali utu wetu ndiyo utuunganishe.

Pia soma:Suluhisho la vita ya Mashariki ya kati ni kwa Wapalestina kutulia au kuhama kabisa pale Gaza
Mkuu huwa nakusikiliza sana DW kuna watu hawakujui watakujibu kwa kejeli na dharau usife moyo endelea hivohivo
 
Labda unaongelea Watu wa Palestina ya Sinza/Nzese.
Sio Wapalestina tu ila ata Waisaeli hawawezi kukubali kuwa na Taifa moja maana Wapalestina wengi ni wakimbizi huko nje kitendo cha kuwa Taifa moja manaake watarudi kwao na wale wanazaliana sana hivo population yao itawameza wayahudi kitu ambacho kinatafanya wayahudi wakose nafasi za uongozi.

Kama kuwa mataifa mawili tu yaani Palestina ipate uhuru wake Israel haitaki sembuse kuwa Taifa moja?
 
Hilo nalo neno!
 
Back
Top Bottom