Kusugua au kusigina meno wakati mtu yupo usingizini

Pole sana Lupituko. Huu sio ugonjwa kama magonjwa mengine. Unahitaji kumuona daktari wa meno kwa ushauri zaidi.
inawezekana kuwa utahitaji kifaa kinachoitwa "occlusal/mouth guard".

Ukisahau kukivua hicho kifaa watu watatoka mbio ofisini wakidhani unabadilika kuwa Zombi.
 

Huku ni kulika kwa meno kwenye sehemu ambapo meno ya juu na chini hukutana (occlusal surfaces). Katika hali ya kawaida meno hulika sehemu hizi kutokana na kadri yanavyoendelea

kutumika kusaga vyakula. Hali hii huendelea polepole kadri mtu anavyoendelea kuishi (umri), kitaalamu inajulikana kama physiological attrition. Si rahisi kuhisi dalili zake kwani mwili

hujaribu kuziba vitundu vya mifereji midogo inayotoka kwenye kiini cha jino kwenda kwenye sehemu ngumu ya kati (dentine). Ni vitundu hivi ambavyo vikiwa wazi husababisha msisimko

(sensitivity). Kulika kwa meno sehemu ya kusaga huwa ugonjwa pale tu unapotokana na mambo mengine zaidi ya kule kwa kawaida kwa kuongeza umri.


Sababu za kusagika kwa meno (attrition)

Baadhi ya mambo yanayosabisha hali hii ni

Kusaga meno (bruxism):
- hii ni hali ambayo mtu husaga meno yake wakati hatafuni kitu

chochote na mara nyingi mtu huwa hajitambui kama ana tatizo hili. Hali hii mara nyingi

hujitokeza wakati wa usiku mtu akiwa amelala (nocturnal bruxism) japo kwa wachache

wanaweza saga mchana pia. Si rahisi mtu wa namna hii kujitambua mpaka pale

atakapoambiwa na mtu wanayelala pamoja au atakapo kwenda kwa mtaalamu wa meno na

kuelezwa.

Nini husababisha hali hii?

Yapo baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha tatizo hili ingawa zaidi linahusishwa na mabadiliko ya kisaikolojia. Watu wenye mawazo mengi wanaonekana kuwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili.

Tatizo hili pia linaweza kutokana na jino lililozibwa na kujazwa zaidi ya kawaida. Mwili hufanya harakati za kupungua sehemu iliyozidi kwa kuisaga na hatimaye kujikuta umejenga mazoea, kiasi kwamba hata jino likisha kuwa kiasi sawa bado mwili utaendelea kusaga tu.

Pia wale wanaokaa kwenye meza kwa muda mrefu wakisoma au vyovyote huku wameshikiria kidevu kwa nguvu, nao ni waathirika wa ugonjwa huu. Katika hali ya kawaida mtu ukiwa

umefunga mdomo umetulia meno ya juu na ya chini huwa hayakutani bali huacha nafasi kama milimita mbili hivi (resting space). Sasa ukiyabana pamoja kwa muda mrefu kwa kushikilia

kidevu, utayafanya yajenge mazoea ya kushikana hata pale ambapo hujashika kidevu na mwishowe kuanza kusagana

Dalili zake na viashiria vyake

Mgonjwa mwenyewe kuhisi msisimko wakati wa kunywa vitu vya baridi, maumivu kama kiwango cha uharibifu ni kikubwa kiasi cha kuacha kiini jino wazi (dental pulp exposure).

Ukiangalia meno utakuta yamelika sehemu ya kutafunia kwenye magego na visaidizi vyake (molars and premolars), sehemu za kukatia na kuchoma kwa meno ya mbele (canines and

incisors). Kusagika huanzia sehemu za meno zilizoinuka (cusps) ambazo hatimaye huondoka kabisa na kuwa bapa au flati. Meno huweza kusagika mpaka wakati mwingine kufikia kwenye

usawa wa fizi. Watu wenye tatizo hili huonekana kuwa na uso wa mraba kutokana na msuli

mkubwa wa kuvuta taya (masseter muscle) kunenepa kutokana na kutumika zaidi. Mgonjwa pia huweza kuchoka kirahisi misuli wakati wa kutafuna katika hali ya kawaida.

Tatizo linaweza kuathiri hata sehemu ya muunganiko wa taya la chini na fuvu

(temporomandibular joint - TMJ). Mgonjwa huweza kusikia maumivu kwenye kiungo (joint) hiki

na wakati mwingine kufyatuka fyatuka (TMJ dislocation) au kutoa sauti wakati wa kufungua na

kufunga kinywa (popping or cricking sound in TMJ).








picha ya juu-kinachoonekana kama kuvimba shavu ni msuli wa kuvuta taya (masseter muscle) ulioongezeka ukubwa

kutokana na kusaga meno. Picha ya chini mwezi mmoja baada ya kupata matibabu ya uhakika, msuli unarudi katika hali

ya kawaida.


Matibabu

Ni vizuri kujua chanzo cha tatizo hili na kukishughulikia kwanza kabla ya kufanya matibabu

zaidi ya meno kurekebisha uharibifu uliotaka na msagiko. Utafiti unaonesha wengi wenye

matatizo haya ni wenye mawazo yaliyozidi kiwango (stress). Lazima ujue kwanini mtu

anawaza sana ili ummpatie ushauri nasaha au hata kumpeleka kwa wataamu wa mambo ya

saikolojia ili waweze kumsaidia.

Wakati hayo yakiendelea inabidi kumfundisha mgonjwa kulegeza taya (relaxation exercise) na

kuachanisha meno kila anapohisi meno ya juu na ya chini yamekutana. Akifanya mazoezi haya

kwa muda mrefu mwili huweza kujenga mazoea kuwa kila meno yakikutana yaachanishwe

(conditioned reflex action). Mgonjwa akiacha kusaga basi matibabu ya kurekebisha madhara

yanaweza kufanyika kwa mafanikio makubwa, iwe kuziba, kuua mzizi wa jino na kuyavalisha

meno kofia ngumu hasa metal reinforced porcelain crown.

Kwa wale ambao ni vigumu kuacha tabia ya kusaga wanaweza kutengenezewa kifaa maalumu

cha kulinda meno wakati wa usiku (night guards), ambacho huvaliwa na mgonjwa usiku wakati

wa kulala kuzuia meno kugusana na baada ya muda atazoea pia na kuacha kusaga. Kifaa hiki

husaidia pia kuondoa matatizo yaliyokwisha jitokeza kwenye jointi.




kifaa cha kukinga meno yasisagane (night guard) mgonjwa akiwa amevaa kifaa

Ni vizuri kumuuliza mwenzako kama amewahi kukusikia ukisaga meno usiku ili uweze kuchukua hatua za kuwaona

wataamu mapema. Kumbuka kujua tatizo mapema na kulitibu ni sehemu ya hatua za kinga.

Niishie hapa kwa leo, siku nyingine nitaongelea aina nyingine za kulika kwa kwa meno kama kuyeyuka kwa meno (tooth

erosion
), abrasion na abfraction wakati huo nitakuwa nimejaribu kupata maelezo ya “abfraction na abrasion”
 

Ushauri mzuri kabisa..
 
Kuna hili tatizo la mtoto mara nyingine kumsikia kama anatafuna meno kwa sauti kubwa kama vile mtu anayekula mahindi magumu yaliyokaangwa.

Ninaomba kuuliza nini hasa chanzo cha tatizo hili?
Na ni kwa nini iwe ni usiku tena akiwa kwenye usingizi?
Je,tatizo hili linaweza kuishaje?

cc.
MziziMkavu na wengineo naombeni ufafanuzi wa kitaalam kutokana na ujuzi mlio nao
 
Hali hiyo humtokea mwanangu pia, hasa pale anapoumwa. Ngoja tuwasubirie wataalamu watujuze
 
Mwezi wa tatu mwishoni nilimpa dawa ya minyoo.

Basi mkuu jaribu kumpeleka hospital akachekiwe zaidi maana katoto change kalishawah kuwa na hali kama hii tukashauriwa tumpe doz ya minyoo mbona aliacha kabisa kutafuna meno.
 
Basi mkuu jaribu kumpeleka hospital akachekiwe zaidi maana katoto change kalishawah kuwa na hali kama hii tukashauriwa tumpe doz ya minyoo mbona aliacha kabisa kutafuna meno.


Nashukuru sana kwa ushauri wako .Hata hilo la minyoo nitalifanyia kazi.
 
jamani na mim nimeona nichukue furusa hii kuwauliza swala la mtoto kuota MENO mwanangu ana miezi minane lkn hajaota meno nifanye nin
 
Mungu akubariki sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…