KUTAFUTA CHUMBA CHA KUPANGA SI KAZI NDOGO KAMA WENGI WANAVYOFIKIRI.

Joined
Mar 7, 2020
Posts
43
Reaction score
81
Kuna kipindi nilikuwa nasoma UDOM, na kama umewahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, utakuwa unaelewa vizuri kabisa maana ya kutafuta sehemu ya kuishi.

Unaweza ukafika eneo fulani ukiwa na matumaini kwamba leo lazima upate chumba. Unakutana na mtu unamuuliza;

"Samahani, huku kuna vyumba vya kupanga?"

Anaweza kukuambia, "Ndiyo vipo, lakini mwenye nyumba hayupo."

Unaendelea kutembea.

Unauliza mwingine, anakuelekeza upande mwingine.

Ukifika kule unaambiwa chumba kimechukuliwa jana.

Kesho yake unaanza tena.

Wakati mwingine unatembea umbali mrefu, unatumia nauli, muda unaenda, jua linawaka, lakini mwisho wa siku unarudi bila kupata chumba.

Na kwa mwanafunzi wa chuo, hali hii inaweza kuwa ngumu zaidi.

Mwanafunzi mpya akifika mjini, mara nyingi hajui maeneo vizuri. Hajui nyumba zipi zinapangishwa, bei zake ni kiasi gani, wala nani ana vyumba vilivyo wazi.

Anaweza kuishia kuzunguka mtaa mzima akiwauliza watu.

Na si wanafunzi pekee.

Hata mtu anayehama kutoka mtaa mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya kazi, biashara, familia au sababu nyingine anaweza kupitia changamoto kama hizi.

Tatizo jingine ni kwamba taarifa nyingi za vyumba huwa zinatembea kwa njia za kawaida sana, mtu anamwambia rafiki yake, rafiki anamwambia mwingine, au unaona karatasi imebandikwa kwenye nguzo.

Na wakati mwingine unakuta taarifa uliyoipata ni ya zamani, kumbe chumba kilishapangishwa siku kadhaa zilizopita.

Nimepitia maisha haya kama mwanafunzi wa UDOM, na sasa mimi mwenyewe nimepanga mtaani. Kwa hiyo najua kabisa kwamba kutafuta sehemu nzuri ya kuishi kunaweza kuwa mchakato unaochosha.

Ndiyo maana nikajiuliza:

Kwa nini mtu anayetafuta chumba asipate sehemu moja ambayo anaweza kwenda na kuona vyumba vinavyotangazwa badala ya kuzunguka mtaa mzima kuulizia?

Hapo ndipo nilipoanza kujenga PataChumba.

PataChumba inalenga kuwa daraja kati ya watu wanaotafuta vyumba/nyumba za kupanga na watu wanaotangaza vyumba/nyumba hizo.

Badala ya kuanza na kutembea bila kujua utakutana na nini, unaweza kuanza kwa kutafuta matangazo ya vyumba na nyumba kupitia PataChumba.

Na kwa mwenye chumba au nyumba inayopangishwa, unaweza pia kutangaza nafasi yako ili kuwafikia watu wanaotafuta sehemu ya kuishi.

Kwa kifupi;

Unatafuta chumba? PataChumba.

Una chumba au nyumba ya kupanga? Tangaza PataChumba.

Hii ni moja ya hatua ninazochukua kuhakikisha wazo nililokuwa nalo kichwani halibaki kuwa wazo tu, bali linakuwa huduma inayoweza kusaidia watu kwenye maisha yao ya kila siku.

Nafurahi kwa kuwa kwa sasa PataChumba ni daraja kati ya wanaotafuta sehemu ya kuishi na wamiliki wa vyumba.
https://patachumba-8fd9leim.manus.space
 
Attachments

  • 1000041253.jpeg
    1000041253.jpeg
    42.4 KB · Views: 10
Ungeenda moja kwa moja kutangaza biashara yako uache stori za uongo. Kuna wengine kama mimi unanikwaza hata hiyo biashara inakuwa sina hamu ya kuifahamu. - "Nimepata suluhisho na nimetengeneza App ya kusaidia kupata vyumba au chumba cha kupanga kirahisi baada ya kuona watu wanahangaika kutafuta kwa muda mrefu nyumba au chumba cha kupanga huku wengine wanalazimika kuwatumia madalali ili wapate chumba. Naombeni ........"
 
Ungeenda moja kwa moja kutangaza biashara yako uache stori za uongo. Kuna wengine kama mimi unanikwaza hata hiyo biashara inakuwa sina hamu ya kuifahamu. - "Nimepata suluhisho na nimetengeneza App ya kusaidia kupata vyumba au chumba cha kupanga kirahisi baada ya kuona watu wanahangaika kutafuta kwa muda mrefu nyumba au chumba cha kupanga huku wengine wanalazimika kuwatumia madalali ili wapate chumba"

Sawa, ni vile tu mimi ni mgeni huku, nilifikiri nimeweka uzi kumbe nimeweka kwenye jamvi la watu! Ngoja nifanye niondoe.
 
Kuna kipindi nilikuwa nasoma UDOM, na kama umewahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, utakuwa unaelewa vizuri kabisa maana ya kutafuta sehemu ya kuishi.

Unaweza ukafika eneo fulani ukiwa na matumaini kwamba leo lazima upate chumba. Unakutana na mtu unamuuliza;

"Samahani, huku kuna vyumba vya kupanga?"

Anaweza kukuambia, "Ndiyo vipo, lakini mwenye nyumba hayupo."

Unaendelea kutembea.

Unauliza mwingine, anakuelekeza upande mwingine.

Ukifika kule unaambiwa chumba kimechukuliwa jana.

Kesho yake unaanza tena.

Wakati mwingine unatembea umbali mrefu, unatumia nauli, muda unaenda, jua linawaka, lakini mwisho wa siku unarudi bila kupata chumba.

Na kwa mwanafunzi wa chuo, hali hii inaweza kuwa ngumu zaidi.

Mwanafunzi mpya akifika mjini, mara nyingi hajui maeneo vizuri. Hajui nyumba zipi zinapangishwa, bei zake ni kiasi gani, wala nani ana vyumba vilivyo wazi.

Anaweza kuishia kuzunguka mtaa mzima akiwauliza watu.

Na si wanafunzi pekee.

Hata mtu anayehama kutoka mtaa mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya kazi, biashara, familia au sababu nyingine anaweza kupitia changamoto kama hizi.

Tatizo jingine ni kwamba taarifa nyingi za vyumba huwa zinatembea kwa njia za kawaida sana, mtu anamwambia rafiki yake, rafiki anamwambia mwingine, au unaona karatasi imebandikwa kwenye nguzo.

Na wakati mwingine unakuta taarifa uliyoipata ni ya zamani, kumbe chumba kilishapangishwa siku kadhaa zilizopita.

Nimepitia maisha haya kama mwanafunzi wa UDOM, na sasa mimi mwenyewe nimepanga mtaani. Kwa hiyo najua kabisa kwamba kutafuta sehemu nzuri ya kuishi kunaweza kuwa mchakato unaochosha.

Ndiyo maana nikajiuliza:

Kwa nini mtu anayetafuta chumba asipate sehemu moja ambayo anaweza kwenda na kuona vyumba vinavyotangazwa badala ya kuzunguka mtaa mzima kuulizia?

Hapo ndipo nilipoanza kujenga PataChumba.

PataChumba inalenga kuwa daraja kati ya watu wanaotafuta vyumba/nyumba za kupanga na watu wanaotangaza vyumba/nyumba hizo.

Badala ya kuanza na kutembea bila kujua utakutana na nini, unaweza kuanza kwa kutafuta matangazo ya vyumba na nyumba kupitia PataChumba.

Na kwa mwenye chumba au nyumba inayopangishwa, unaweza pia kutangaza nafasi yako ili kuwafikia watu wanaotafuta sehemu ya kuishi.

Kwa kifupi;

Unatafuta chumba? PataChumba.

Una chumba au nyumba ya kupanga? Tangaza PataChumba.

Hii ni moja ya hatua ninazochukua kuhakikisha wazo nililokuwa nalo kichwani halibaki kuwa wazo tu, bali linakuwa huduma inayoweza kusaidia watu kwenye maisha yao ya kila siku.

Nafurahi kwa kuwa kwa sasa PataChumba ni daraja kati ya wanaotafuta sehemu ya kuishi na wamiliki wa vyumba.
https://patachumba-8fd9leim.manus.space
Idea nzuri sana.

Lakini kwenye Item karibu kuongeza description kwenye location, naendelea utie na land marks za item inapopatikana.

Mfano umbali kutoka barabara Kuu au property maarufu ya umma
 
Nyumba wanaweka za Kishua tu za bei juuz hakuna za wanafunzi hapo
Mm nimechagua option ya nyumba za 50k kwa mwezi uswahilini, kumbe ndo mana sijaziona hizo nyumba, nikadhani mtandao mbovu 😂
 
Back
Top Bottom