Nimewahi kufahamu njia inayokuwezesha kupata mtoto jinsia uitakayo. Kama kuna asiyefahamu basi nitaeleza. Mwanamke ana chromosomes XX, na mwanaume ana chromosomes XY.
MTOTO WA KIUME:
Mtoto wa kiume hupatikana kwa kuunganisha mbegu za kiume Y kukutana na ya kike X. Mbegu za kiume Y zina sifa ya kuwa na kasi sana kuliko X. Pamoja na kasi hizo sio stahimivu, zinakufa mapema sana. Ili upate mtoto wa kiume hakikisha unakutana na mwenza wako katika kipindi ambacho anatoa ute mwepesi, kwa kuwa mbegu Y zitakuwa na uwezo wa kusafiri kwa kasi bila kipingamizi. Ute ukiwa mzito basi zinachoka na kufa njiani.
MTOTO WA KIKE:
Huyu anapatikana kwa muunganiko wa X ya kiume na X ya kike. Mbegu za X hazina kasi na ni stahimivu. Kupata mtoto wa kike ni rahisi kuliko wa kiume. Hizi X zina uwezo wa kuishi masaa 72..sawa na siku 3. Hivyo basi unaweza kukutana na mke wako siku tatu kabla ya yai halijapevuka. Pia ute ute ukiwa mzito mtoto wa kike utampata kwa kuwa mbegu X zina ongelea kwa muda mrefu, hazichoki na kufa kwake ni masaa 72.
Baada ya hayo, naomba kujulishwa nani anafahamu mbinu za kupata watoto mapacha.?