Kutaka kila mtu akuongelee vizuri ni kutafuta msongo wa mawazo kuwa mwema ila usijali watakavyokuongelea

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
KUTAKA KILA MTU AKUONGELEE VIZURI NI KUTAFUTA MSONGO WA MAWAZO KUWA MWEMA ILA USIJALI WATAVYOKUONGELEA

Zama zinaenda kasi na vifo vitokanavyo na matokeo ya msongo wa mawazo vikiongezeka ikiwemo kujiua au shinikizo la juu la damu hata magonjwa ya moyo.

Msongo wa mawazo hautoki mbinguni bali ni kwenye maisha yetu ya kila siku ama kwa matendo yetu au kusababishiwa na watu na kukuta uwezo wako mdogo wa kuzikabili hizo changamoto.


Moja wapo ya sababu inayofanya watu wapate msongo ni kulipwa tofauti matendo yao yaani mtu anakua mwema halafu baadaye anasikia akiongelewa kwa ubaya hii inaumiza sana tena ukute anayekuongelea ni mtu wako wa karibu na umewahi kuwa msaada mkubwa kwake.

Hakuna namna unaweza kumfanya kila mtu akuseme vizuri hata hao wanaokusema mazuri tu kuna wengine ni chawa wanaogopa KUKUSEMEA mabaya kwa kuhofia kupoteza ugali ila kwa hulka zetu binaadamu tupo kuongea chochote bila hata ushahidi au kumchukia yoyote bila hata sababu za msingi.

Leo ukivaa ukipendeza KUNA WATU WATACHUKIA

Ukisaidia watu misaada kwa lengo jema kabisa KUNA WATU WATACHUKIA TENA IKIWEMO ULIOWASAIDIA

Ukipata kazi kuna WATU WATACHUKIA

HATA UNAYEMPA KILA SIKU IKITOKEA SIKU MOJA UKISEMA HUNA ATAONA UNAMNYIMA MAKUSUDI NA UNA ROHO MBAYA , ATASAHAU SIKU ZOTE ULIPOKUWA MWEMA

Ifike muda uikubali Dunia ilivyo usisumbuke na maneno la sivyo yawe ya kweli ndio fuatilia ili ujirekibishe ila tofauti na hivyo USIFUATILIE KUJUA WALE ULIOWASAIDIA WANAKUONGELEAJE, WATAKUPA MSONGO BURE

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Mitandaoni Fikia Ndoto Zako
 
Unaanza vipi kujali kuhusu watu wanaongea nn!?
Anyway mi nimeshawahi kushiriki kikao Cha kunipiga majungu na nikawa naongezea ongezea na point
 
Be you, dont care watu wanakupnaje. Utaishi maisha ya amani sana
 
👿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…