Kutaka vilabu wenyeji kuleta ambulance ni uonevu

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Bodi ya ligi ikiongozwa na Boniface Wambura imeweka kanuni inayotaka timu mwenyeji kwenye ligi kuu Bara ihakikishe kunakua na gari la wagonjwa (ambulance) likiwa na wataalamu na vifaa tiba

Timu mwenyeji itakayoshindwa kufanya hivyo itanyang'anywa point tatu na magoli matatu kwasababu kwanza mchezo wenyewe hautachezwa

Kwa maoni yangu kanuni hiyo ya kutaka kuwepo gari la wagonjwa kwenye mechi zote ni nzuri na hakika imechelewa kuja. Kitu ambacho hakiko sawa hapo ni kuvibebesha vilabu jukumu hilo

Nadhani hilo ni jukumu lisilo kwepeka la TFF kupitia Bodi ya ligi hasa ukizingatia hali za kiuchumi na mapato kwa timu zetu ambazo kwanza tayari zina mzigo mzito wa kuhakikisha zinajiendesha ikiwamo kulipa mishahara kwa wachezaji na wafanyakazi wengine

TFF na Bodi ya ligi wanachukua makato yatokanayo na viingilio lakini pia inapopata mdhamini kunakua na fungu la uendeshaji ambalo ni lazima wajibane ili washughulikie mambo kama hayo

TFF kwa udhaifu wao na makosa yao wenyewe walisababisha kusiwe na mdhamini kwenye msimu wa ligi uliopita na msimu huu hata kama wamempata lakini kachelewe na hivyo kupelekea vilabu kuanza kubeba mzigo wa ushiriki wa ligi

Najiuliza vyama vya mpira vya wilaya na mikoa ambavyo pia ni wanachama wa TFF wanajukumu gani kama kila kitu kuhusiana na gharama za mechi zinaachiwa vilabu wakati vyama hivyo vinapata migao ya pesa kwenye gate collections?

Natoa wito kwa kina Karia na mwenzake Wambura waache ubabe na wawe wadau wa kweli wa mpira na kuacha kuvibebesha mzigo vilabu. Ninavyoelewa kila timu ina daktari wake ambae analipwa na klabu
 
Hii kanuni haitendi haki kwa Timu mwenyeji. Kwa kuwa kwenye mapato ya uwanjani kuna kipengele cha kukata gharama za uwanja, ingefaa malipo ya Ambulance na watu wa huduma ya kwanza yatokane na mapato ya uwanjani na sio Club mwenyeji kugharamia hiyo huduma wakati tayari vilabu vinakuwa na Daktari wa timu.
 
Sawa kabisa mkuu. Kuna mechi zimeripotiwa kuingiza hela kidogo sana yaani hata laki haifiki. Halafu bado vilabu vinabebeshwa mzigo wa kutakiwa kuleta sio tu ambulance bali pia iwe na wataalamu wa afya wenye sifa na wanaotambulika na mamlaka husika na iwe vifaa tiba

Kwanini jukumu hilo lisiachiwe mashirikisho ya soka ya wilaya au mikoa inayotoka timu mwenyeji? Au wale kazi yao ni kukinga tu pesa kwenye migao ya gate collection?
 
Kwa hili bodi ya ligi wamekosea tena sana...
Na nitashangaa kama vilabu havitaungana kulipinga hili ili na sisi wadau tupaze sauti kuwasaidia.
Hovyo kabisa.
 
Kweli kabisa mkuu. Tena maranyingi kwenye utungaji wa kanuni za mashindano hasa za ligi wadau wote hasa vilabu huwa wanashirikishwa, sasa nashangaa hili limepitishwaje kimya kimya!!!?

Inajulikana ambulance ikiwepo uwanjani hutumiwa na wote wenye dharura ya kimatibabu ikiwemo na mashabiki waliohudhuria mechi. Kwa maana hiyo hili si jukumu la vilabu ni jukumu la moja kwa moja la uongozi wa soka wa ama wilaya, mkoa au taifa
 
Hii kanuni haitendi haki kwa Timu mwenyeji. Kwa kuwa kwenye mapato ya uwanjani kuna kipengele cha kukata gharama za uwanja, ingefaa malipo ya Ambulance na watu wa huduma ya kwanza yatokane na mapato ya uwanjani na sio Club mwenyeji kugharamia hiyo huduma wakati tayari vilabu vinakuwa na Daktari wa timu.

Kuna mechi ya ligi kuu msimu uliopita kati ya Prisons na nani sijui vile iliyofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya, waliingia mashabiki watatu na hivyo kupata kiingilio cha tsh 9000! Kwa hali hiyo hao jamaa wenye ambulance, wanaweza kukuchoma hata sindano ya sumu wewe uliyewaita kwa hasira.

Kama vilabu havitaridhika, ni bora vikaa na hiyo bodi yao ya ligi kuangalia namna ya kutatua hilo tatizo bila shaka.
 
Sawa kabisa mkuu. Kuna mechi zimeripotiwa kuingiza hela kidogo sana yaani hata laki haifiki. Halafu bado vilabu vinabebeshwa mzigo wa kutakiwa kuleta sio tu ambulance bali pia iwe na wataalamu wa afya wenye sifa na wanaotambulika na mamlaka husika na iwe vifaa tiba
Kwanini jukumu hilo lisiachiwe mashirikisho ya soka ya wilaya au mikoa inayotoka timu mwenyeji? Au wale kazi yao ni kukinga tu pesa kwenye migao ya gate collection?
Hii ishu ya afya inafanyiwa mzaha sana mkuu..
Kama viongozi wa vilabu walikubaliana hili ngoja tuone ukekelezaji wake utakuwaje.
 
Nahisi kwenye hii kanuni vilabu havikushirikishwa vinginevyo kama vilishirikishwa na vikapitisha hili basi vinashangaza sana

Na kanuni inavyobana ni kwamba kama timu mwenyeji haijaleta ambulance basi mechi haichezwi na inapoteza point tatu na magoli matatu!

Vilabu vitatekeleza hilo kwa vile ni amri/kanuni ya kibabe tu ya wanojiita wenye mpira wao(TFF) lakini vitakua vinaziumiza hasa timu ndogo zinazobangaiza kama kina Biashara, Ndanda n.k
 
Hizi AMBULANCE wawe wanazimiliki au za kukodi?.. Kama hata za kukodi wanakodi kwa nani?
Huko wanapokodi hazina kazi?.. Au ratiba yake itaendana na ratiba ya mechi..?
Sioni kama timu zote zitaweza sheria hii, tofauti na hapo ni hatari kwa afya za wachezaji na mashabiki.
 
Hoja yako ni nzuri sana mkuu
 
TFF hapa mumechemka na kupogoma kabisa kabisa,kwa nn mnakimbia majukumu yenu?!?!,mtaendelea kuziumiza hizi tim milele na milele kwa mwendo huu.
 
Bodi ya ligi ikiongozwa na Boniface Wambura imeweka kanuni inayotaka timu mwenyeji kwenye ligi kuu Bara ihakikishe kunakua na gari la wagonjwa (ambulance) likiwa na wataalamu na vifaa tiba

Timu mwenyeji itakayoshindwa kufanya hivyo itanyang'anywa point tatu na magoli matatu kwasababu kwanza mchezo wenyewe hautachezwa

Kwa maoni yangu kanuni hiyo ya kutaka kuwepo gari la wagonjwa kwenye mechi zote ni nzuri na hakika imechelewa kuja. Kitu ambacho hakiko sawa hapo ni kuvibebesha vilabu jukumu hilo

Nadhani hilo ni jukumu lisilo kwepeka la TFF kupitia Bodi ya ligi hasa ukizingatia hali za kiuchumi na mapato kwa timu zetu ambazo kwanza tayari zina mzigo mzito wa kuhakikisha zinajiendesha ikiwamo kulipa mishahara kwa wachezaji na wafanyakazi wengine

TFF na Bodi ya ligi wanachukua makato yatokanayo na viingilio lakini pia inapopata mdhamini kunakua na fungu la uendeshaji ambalo ni lazima wajibane ili washughulikie mambo kama hayo

TFF kwa udhaifu wao na makosa yao wenyewe walisababisha kusiwe na mdhamini kwenye msimu wa ligi uliopita na msimu huu hata kama wamempata lakini kachelewe na hivyo kupelekea vilabu kuanza kubeba mzigo wa ushiriki wa ligi

Najiuliza vyama vya mpira vya wilaya na mikoa ambavyo pia ni wanachama wa TFF wanajukumu gani kama kila kitu kuhusiana na gharama za mechi zinaachiwa vilabu wakati vyama hivyo vinapata migao ya pesa kwenye gate collections?

Natoa wito kwa kina Karia na mwenzake Wambura waache ubabe na wawe wadau wa kweli wa mpira na kuacha kuvibebesha mzigo vilabu. Ninavyoelewa kila timu ina daktari wake ambae analipwa na klabu
Wambura, Kidao,mguto,nyamlani na KARIA NI WEZI WAKUBWA! !
 
Hii TFF ya wambura na Karia imekosa weledi kabisa.Ntashangaa kama atapita tena huyu mbumbumbu.
 
Back
Top Bottom