Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Bodi ya ligi ikiongozwa na Boniface Wambura imeweka kanuni inayotaka timu mwenyeji kwenye ligi kuu Bara ihakikishe kunakua na gari la wagonjwa (ambulance) likiwa na wataalamu na vifaa tiba
Timu mwenyeji itakayoshindwa kufanya hivyo itanyang'anywa point tatu na magoli matatu kwasababu kwanza mchezo wenyewe hautachezwa
Kwa maoni yangu kanuni hiyo ya kutaka kuwepo gari la wagonjwa kwenye mechi zote ni nzuri na hakika imechelewa kuja. Kitu ambacho hakiko sawa hapo ni kuvibebesha vilabu jukumu hilo
Nadhani hilo ni jukumu lisilo kwepeka la TFF kupitia Bodi ya ligi hasa ukizingatia hali za kiuchumi na mapato kwa timu zetu ambazo kwanza tayari zina mzigo mzito wa kuhakikisha zinajiendesha ikiwamo kulipa mishahara kwa wachezaji na wafanyakazi wengine
TFF na Bodi ya ligi wanachukua makato yatokanayo na viingilio lakini pia inapopata mdhamini kunakua na fungu la uendeshaji ambalo ni lazima wajibane ili washughulikie mambo kama hayo
TFF kwa udhaifu wao na makosa yao wenyewe walisababisha kusiwe na mdhamini kwenye msimu wa ligi uliopita na msimu huu hata kama wamempata lakini kachelewe na hivyo kupelekea vilabu kuanza kubeba mzigo wa ushiriki wa ligi
Najiuliza vyama vya mpira vya wilaya na mikoa ambavyo pia ni wanachama wa TFF wanajukumu gani kama kila kitu kuhusiana na gharama za mechi zinaachiwa vilabu wakati vyama hivyo vinapata migao ya pesa kwenye gate collections?
Natoa wito kwa kina Karia na mwenzake Wambura waache ubabe na wawe wadau wa kweli wa mpira na kuacha kuvibebesha mzigo vilabu. Ninavyoelewa kila timu ina daktari wake ambae analipwa na klabu