Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Shikamoo MzeeMwanakijiji...naona mnaanza kuamka!...Geukeni tu Wala hamtabadilika kuwa Barafu la Chumvi!
Huu NI ujumbe katumiwa Mtakatifu wenu John!
Kwa sisi tusio na elimu ,tumeelewa kuwa Mkuu wa Kaya kapelekewa ujumbe kupitia kwa Mwanawe Mpendwa....
Mfano mdogo tu ...like tukio la kikatili la Tundu Lissu ,Been Saanane halitawaacha wao ,watoto wao ,...mpaka vilembwe!
Hata waliokataa kusimama na haki!
Na kwa jina la MUNGU ALIYE HAI WANA DESERVE' ........Pumbabu!
 
Mpaka wewe Mzee Mwanakijiji umeanza kugeuka

Passport yako ime expire nini Halafu bado upo Tanzania

Kaka kama una makazi huko Marekani anza kurudi home mapema

Kifuatacho kwa hasira serikali itazuia Raia wote wa Tanzania wasiende huko
hahahaha kizee kimeminywa maslahi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona suala la Makonda kudhulumu haki ya kuishi kwa baadhi ya watu kama ilivyosemwa katika sababu nne za yeye kuzuiwa kuingia US..Hili haulisemi.

Kwamba Makonda anatuhumiwa kuuwa baadhi ya watu hili HAULISEMI KABISA..

Tuhuma kubwa na mbaya kama hii ya kumwaga damu kwako sio kitu.Na tayari kuna tuhuma huyu ndie alishiriki mwanzo mpaka mwisho kwenye kuutoa uhai wa Ben Saanane..

Umesimamia tu hapo haki za binadamu nk.

Ni wewe huko nyuma mambo yakiwa yanaenda mrama ulikuwa unaandika kwa namna ya kusifia tu..
Leo suala zito kama hili unaandika kwa namna ile ile..kama vile ni jambo rahisi-rahisi tu..

Kuwa muwazi..Makonda amedhulumu HAKI YA KUISHI ya baadhi ya watu na jpm anapaswa amuondoe sheria zichukue mkondo wake.

US hawawezi kulisema hili bila kuwa na ushahidi.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Serikali ya Marekani ingeweza kuchukua hatua kali zaidi kuliko ambazo imechukua kwa nchi rafiki kama ya Tanzania. Tangu wakati wa Kikwete Tanzania imejisogeza zaidi na Serikali ya Marekani kiasi kwamba ni sawa kabisa kuamini kuwa tuna uhusiano wa karibu na wa kirafiki na Taifa hili lenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi duniani. Uamuzi wa kumzuia Paul Makonda na Mkewe kuingia Marekani na kuzuia Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani (Green Card Lotto) kwa wengine unaweza kuonekana ni mkali lakini kiuhalisia ni uamuzi mwepesi, na siyo mkali kwa kipimo chochote kile lakini ujumbe wake ni Dhahiri kabisa. Rafiki ameona kuna tatizo kwa rafiki yake.

Marekani kama ingetaka ingeweza kuchukua hatua kali zaidi ukiangalia sababu ilizotoa juu ya hatua ilizochukua. Kwenye tuhuma za uvunjaji wa haki za binadamu (kutishia maisha na usalama wa watu), kuminywa kwa uhuru wa habari, uhuru wa kukusanyika na kuwatenga watu kutoka makundi yanayotengwa mengi wangeweza kufanya. Kama Serikali ya Marekani inao ushahidi mzito dhidi ya viongozi wa serikali katika tuhuma hizo bila ya shaka wangeweza kuwaweka watu wengine kwenye zuio hilo la Marekani. Wangeweza kumzuia Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Upelelezi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) n.k.

Kitendo cha zuio lao kuliweka dhidi ya Paul Makonda na mke wake peke yao ni lazima liwekwe kwenye muktadha wake sahihi. Nje ya hapo tutakosa kukielewa kwa kinagaubaga kile ambacho Marekani imekifanya na matokeo yake kila mtu ataweka tafsiri isiyo sahihi. Kuna mambo kadhaa ya kuyaangalia.

US Wanajua Yote Wanayotaka Kujua Kuhusu Makonda

Kwanza, Marekani ina taarifa za kiinteligensia za nini Makonda amekifanya, na wapi amekifanya na namna gani amekifanya. Itakuwa ni makosa makubwa ya kudhania kuwa Zitto Kabwe, Maria Sarungi, Tundu Lissu na wanaharakati ndio wamesababisha Makonda afungiwe. Marekani haimhitaji Zitto, Sarungi au Lissu kujua kinachotokea. Kama kuna lolote wamefanya hawa inawezekana ni kidogo sana kulinganisha na Marekani ilivyopata taarifa zake. Fikiria tu kuwa Marekani iliweza kumpata Osama bin Laden katika maficho yake, Walimpata Abubakri Al-Baghdad na hivi majuzi wamemuua Gen. Kassam Suleimani wa Iran.

Ujumbe wa Kwanza

Katika matukio hayo matatu (Osama, Al-Baghdad, na Suleimani) Wamarekani wameendelea kuonesha dunia uwezo wao wa kiinteligensia iliyopitiliza. Mtandao wa CIA unavyofanya kazi kwa wanaolewa wanajua kabisa ni mzito na wa kina sana. Naomba kudokeza tu kuwa taarifa za kinachoendelea kwenye nchi yeyote CIA wanaweza kupata kwa mbinu nyingi sana na hazihitaji viongozi wa upinzani au wanaharakati. Hivyo basi, hadi Marekani iamue kumtaja na kumtenga Mkuu wa Mkoa Makonda na siyo RPC, RIO, DCI, au DPP wana maana yao. Wanasema “tunajua anachofanya Makonda na hakitufurahishi na kinatishia uhusiano kati ya Tanzania na Marekani”. Huu ndio ujumbe wao wa kwanza.

Ujumbe wa Pili

Hata hivyo Wamarekani kutokana na uwezo wao wa kiinteligensia wameonesha kuwa hadi hivi sasa taarifa walizo nazo hazijafikia kiwango cha kuinyoshea nchi na viongozi wa juu ya nchi kuwatuhumu uvunjaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia na haki mbalimbali za kiraia. Hawakuwa tayari kumtaja Rais Magufuli, Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa. Hawakuwa tayari kumtaja Kapilimba au Diwani, hawakuwa tayari kumtaja Sirro au Mabeyo au Afisa yeyote wa usalama wa ngazi yoyote ile. Hili si jambo dogo; Wamarekani hawaiogopi Tanzania (hatuna cha kuwafanya) na hivyo kama wangetaka kumtaja yeyote kati yao kuwa anahusika na utekaji, uuaji au idara yake inahusika na mambo hayo wangemtaja na katazo lao lingekuwa pana zaidi. Ni wazi kwa kuliweka katazo lao juu ya afisa wa ngazi ya chini wa serikali wanataka kutuambia na kuwaambia viongozi wetu wa juu wafikirie kinachofanywa na huyu bwana kwani kinaweza kuleta matatizo makubwa ya kidemokrasia.

Ujumbe wa Tatu

Katika maamuzi yao Wamarekani hawakumpa katazo kali zaidi Makonda. Kwa kweli ukiangalia utaona kuwa ni katazo jepesi sana. Wamarekani wangetaka siyo tu wangempiga yeye marufuku lakini wangefunga akaunti zake (kama anazo), uwekezaji wake wowote unaofanywa na Makonda au watu wake wa karibu wanaoweza kuwa wanahusika na yale ambayo Wamarekani wanamtuhumu. Kwa maneno mengine, wamempa Makonda nafasi ya kujionesha kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi na hazina ushahidi wowote ule. Hivyo, ujumbe wa tatu ni kwa Makonda mwenyewe. Ni wazi kuwa, kama Makonda alikuwa na mpango wowote wa kuja Marekani mpango huo sasa umekufa. Kama kuna jambo lolote ambalo alihitaji kuja kulifanya hapa (binafsi au kwa niaba ya Mkoa wake) jambo hilo kwa sasa limekufa. Ajitafakari na Mamlaka iliyomteua itafakari kama inataka mtu anayeongoza Mkoa wenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa Tanzania asiwe na uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri na Marekani. Je, inastahili kuvuruga uhusiano na Marekani kwa sababu ya Makonda?

Ujumbe wa Nne

Kwenye maamuzi yao Wamarekani wamepiga marufuku Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani ambayo hatimaye humpa mtu nafasi ya kupata uraia wa Marekani. Visa hii hutolewa kwa njia ya bahati nasibu kwa nafasi 55,000 kila mwaka na kwa Bara la Afrika tunapata nafasi karibu nusu ya hizo. Nchi ambazo hazijatoa washindi wengi hupewa zaidi na zile ambazo zimetoa wengi huko nyuma hupunguziwa. Miaka ya karibuni Watanzania wameanza kushinda na kupata nafasi hizo. Ikumbukwe kuwa aina hii ya Visa tayari inapigwa vita na Rais Donald Trump ambaye anataka kuifuta kwani inawapa nafasi siyo tu wale walioshinda kuingia Marekani bali hata familia zao na ndugu wa karibu.

Hivyo kuzuia nafasi hiyo kumeondoa nafasi kwa Watanzania ambao wangependa kujaribu maisha huko Marekani. Hata hivyo, kiukweli kabisa uamuzi huu ni mdogo sana kuliko ambao watu walihofia. Marekani ikitaka watu wa nchi fulani wasiingie inaweka zuio kali zaidi. Hata hivyo, kwa Tanzania haikufanya hivyo; badala yake imeweka zuio kwenye program ambayo labda watu wachache sana inawahusu. Na hapa kuna ujumbe; Marekani haikutaka kuvuruga uhusiano na Tanzania na badala yake imetuma ujumbe wa kirafiki. Watanzania bado wanaweza kwenda Marekani kwa shughuli zao mbalimbali. Kwamba, kama itakuja kulazimu basi hatua kali zaidi za uhamiaji zitachukuliwa. Huo nao ni ujumbe wa kidiplomasia; wenye onyo na ushauri ndani yake. Wamarekani wangetaka kupiga marufuku Watanzania wote wasiingie Marekani wangeweza ila hawakufanya hivyo.

Serikali Ijibu Vipi Marekani?

Swali kubwa ni je Serikali ijibu vipi Marekani kutokana na hatua hizi mbili? Serikali ya Tanzania kama nchi huru na yenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali inatakiwa kupima mwitikio wake. Lakini ili itoe mwitikio sahihi ni lazima ijioneshe imeelewa kwa muktadha sahihi hatua zilizochukuliwa na Marekani. Ukweli ni kuwa Marekani haijachukua hatua kali sana za kidiplomasia; imechukua hatua za chini zaidi kulinganisha na hatua zilizochukuliwa kwa nchi kama Venezuela, Iran, Cuba, na Korea ya Kaskazini. Kutokana na ukweli huu basi kuna mambo au hatua kadhaa serikali inaweza kuchukua.

  • Serikali Inaweza Kupuuzia Tuhuma na Hatua za Marekani
  • Serikali ya Tanzania inaweza ikapuuzia na kuona kuwa hoja za Marekani hazina msingi, tuhuma zake hazina ushahidi na hatua zilizochukuliwa hazina ulazima wowote. Kwa maneno mengine, serikali inaweza kusema “Marekani inasema uongo”. Lakini ili iweze kusema hivi na kufanya hivi ni lazima iwe na ushahidi kinyume. Na hivyo, kwa vile Makonda na Mkewe hawana mpango wa kwenda Marekani siku yoyote ya karibuni na kuwa Serikali haijali hizo Visa za bahati nasibu basi serikali inaweza kusema “tunaheshimu uamuzi wa Marekani japo hatukubaliani nao” halafi ikaendelea na mambo yake.

  • Serikali Inaweza Kuhoji na Kupinga Hatua za Marekani
  • Ikionesha kuwa imechukizwa Serikali inaweza kubeza, kupinga na kukataa hatua za Marekani. Inaweza ikasema “tuhuma hazina msingi na zina lengo la kuichafua Tanzania”. Na ikipenda inaweza kumuita Balozi wa Marekani (Naibu Balozi) na kutoa pingamizi la kidiplomasia (diplomatic protest). Lakini inaweza ikataka maelezo ya ushahidi ambao Serikali ya Marekani inayo ya kuhusika kwa Makonda katika uvunjaji wa haki za binadamu, kuvuruga haki za watu kuishi na uminyaji wa demokrasia na haki za kiraia zilizoanishwa Kikatiba na kulindwa na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania imeridhia. Ikifanya hivi Serikali itakuwa imeamua kufuata njia ya kuchochea (elevate) mgogoro kutoka wa afisa wa chini wa Serikali na kuiingiza Serikali nzima na hivyo kutoa nafasi kwa Marekani kuongeza kibano zaidi kwa watu zaidi – nje ya Makonda. Binafsi ningependa kuwajua hao watu ni kina nani maana Makonda (kama kweli anavyodaiwa kufanya) hayupo peke yake.

  • Na katika kupinga kwake Serikali inaweza ikaamua na yenyewe kujibu mashambulizi kiaina. Sijui tunaweza kumpiga nani marufuku kuingia Marekani kwa tuhuma gani! Na sijui ni Visa za aina gani tunaweza kuwakataza Wamarekani kuja Tanzania. Lakini pia itakuwa ni ku-escalate (kufanya jambo dogo kuwa kubwa zaidi). Itakuwa njia sahihi?

  • Eritrea ambao nao wamewekewa vizuizi na Marekani inaonekana wamechagua aina ya jibu hili na kutoa kauli kali ya kupinga katazo au marufuku hiyo ya Marekani.

  • Serikali Inaweza Kuzingatia Tuhuma na Kuzipa Uzito Unaostahili
  • Kama nilivyosema hapo juu kwa namna moja Marekani imeinyoshea kidole Serikali na kinamna imemnyoshea kidole Rais Magufuli bila kupiga kelele sana. Kwa vile Makonda ni mteuliwa wa Rais ni wazi kuwa wanataka kumwambia Magufuli kuwa kama kuna jambo halijui basi mteuliwa wake anahusishwa na mambo mabaya (yanayoweza kupakana na uhalifu au uhalifu dhidi ya ubinadamu – crimes against humanity). Wamarekani wanataka kuona ni nani kweli anamlinda Makonda na kama mambo yanafanywa na Makonda yana baraka na viongozi wa juu wa serikali. Jinsi gani Serikali itaitikia ndio mtego ulipo; je itajitokeza na kumlinda Makonda kwa nguvu zote au itatulia na kumuita Makonda na kuhoji (labda baada ya kuwasiliana na Marekani).

  • Je, Serikali itakuwa tayari kuona Watanzania wengine wanaadhibiwa (kwa kunyimwa Visa) kwa sababu ya mtu mmoja? Je, kuna vitu ambavyo inawezekana vinahitaji kuangaliwa kwa uzito unaostahili na kuonesha dunia na Watanzania kuwa Serikali kweli inaamini katika haki za binadamu na uhuru wa kidemokrasia?

  • Kwa mfano, suala la kuhakikisha kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki lina mtego. Uchaguzi hauwi huru na wa haki siku ya uchaguzi tu bali mazingira yote yanayohusiana na uchaguzi yako vipi? Hili Marekani wanafuatilia vinginevyo tunaweza kujikuta kwenye mgogoro mkubwa sana kama wa Zimbabwe kati ya Mugabe na Morgan Tsvangirai. Kweli uchaguzi unaweza kufanyika Oktoba lakini hawa hawa wakasema toka Januari tuliona kuna matatizo Tanzania na hawakusikia na hivyo uchaguzi huu haukuwa huru (hata kama sisi tutauita hivyo). Hili lilitokea kwa Maduro wa Venezuela. Binafsi siamini kama tutafika huko lakini sioni kwanini watu wapewe sababu ya kudhania kuwa tunaweza kufika huko!

  • Kama Serikali (Rais Magufuli) mwenyewe ataona kuwa jambo hili ni zito kweli basi suala la Makonda linaweza kuwa ni jambo lilotegwa kwake. Maana baada ya Marekani kufanya walivyofanya sitoshangaa siku chache zijazo washirika wake nchi za EU na Uingereza zinaweza nazo kutoa matamko ya aina hiyo na hivyo kulikuza jambo hili.

  • Nigeria ambao nao wamepigwa marufuku kali zaidi kuliko ile ya Tanzania wameamua kuchukua kwa uzito wake katazo hili hasa ukizingatia ukaribu wao na Marekani na wameamua kuunda Kamati Maalum ya kuchunguzi madai yaliyosababisha Marekani ipige marufuku wananchi wake kuingia Marekani.
Hekima Itatamalaki?

Ndugu zangu, kati ya hatua hizo tatu Serikali ina mambo ya kupima kabla ya kufanya. Inaweza ikaamua kupimana nguvu na Marekani kidiplomasia au inaweza ikatafakari na kuona ni njia ipi itapunguza na kulifanya jambo hili lisiwe kubwa zaidi. Ni hatua gani itachukua kuonesha kweli inaheshimu haki za binadamu na haki za kidemokrasia; itajionesha ni kwa namna gani Makonda si mtu ambaye anaweza kutishia haki za kidemokrasia kwa mtu yeyote yule. Ni kwa sababu hiyo swali kubwa linalohitaji kujibiwa baada ya tafakari hii ni je hekima inaweza vipi kutamalaki?

Muda utatupa majibu.

Niandikie: [email protected]
miiforums.com
Mkuu naona Hatimaye umepata nguvu za kuja Jukwaani...

Naona ulipigwa ganzi kali tangu mambo ya mkopo wa World Bank na hili la kupigwa ban Bashite na kunyemelewa Magufuli hujajitokeza kabisa kujadili
 
Naona suala la Makonda kudhulumu haki ya kuishi kwa baadhi ya watu kama ilivyosemwa katika sababu nne za yeye kuzuiwa kuingia US..Hili haulisemi.

Kwamba Makonda anatuhumiwa kuuwa baadhi ya watu hili HAULISEMI KABISA..

Tuhuma kubwa na mbaya kama hii ya kumwaga damu kwako sio kitu.Na tayari kuna tuhuma huyu ndie alishiriki mwanzo mpaka mwisho kwenye kuutoa uhai wa Ben Saanane..

Umesimamia tu hapo haki za binadamu nk.

Ni wewe huko nyuma mambo yakiwa yanaenda mrama ulikuwa unaandika kwa namna ya kusifia tu..
Leo suala zito kama hili unaandika kwa namna ile ile..kama vile ni jambo rahisi-rahisi tu..

Kuwa muwazi..Makonda amedhulumu HAKI YA KUISHI ya baadhi ya watu na jpm anapaswa amuondoe sheria zichukue mkondo wake.

US hawawezi kulisema hili bila kuwa na ushahidi.
Mzee mpuuzi huyu!
 
Umeandika vizuri, umeshauri vizuri. Nina imani Profesa Kabudi na Dr. Magufuli watazingatia ushauri huu.

Binafsi nisingependa mivutano na Marekani. Nashauri tume huru ya kijaji iundwe na ichunguze tuhuma hizi.

Tunawahitaji marafiki zetu na majirani zetu kuliko wao wanavyotuhitaji sisi. Let us be humble and active. Ninaamini hiyo tume itamsafisha RC kama tuhuma ni za uongo au itapelekea kuwajibishwa kwake na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kama tuhuma zina chembe ya ukweli.



Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la Tanzania ya sasa hakuna mwenye uwezo wa kufanya maamuzi against Jiwe.

Hiyo tume ya kijaji lazima itagundua uozo wote na ikamshauri jiwe na akakataa ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ukosefu wa hekima kwa baadhi ya viongozi wa juu wa nchi ndilo linatutafuna.Hekima itatawala milele sawa,lakin je,wataipataje hiyo hekima?Mungu amesema waombe.

Hili jambo ni baya na linaweza kugeuza sura ya Tanzania milele kwa sababu ushahidi ni wa wazi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ni rahisi sana hapo,kama Mh.Rais anampenda mteule wake amtoe kwenye nafasi hiyo ampe nyingine ambayo ni ya kiutendaji zaid kuliko hizi za kisiasa zinazomkutanisa na wananchi.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si mlikuwa mkisifia kwa kauli mbiu ya "Go Magufuli go" wewe na Slaa wako! Sasa kwa taarifa yako ni kuwa main target ni Dr. John Pombe Magufuli.

Serikali wajibu, wasijibu, waongee, wasiongee, wapuuze, wasipuuze it's too late. Makonda alituhumiwa kwa mauaji wazi wazi na hadi huku JF tukamuita Malyamungu bado mkaona tunaona wivu eti mchapakazi. Serikali ya Rais Magufuli imeshakosa credibility nje na ndani ya nchi haifai tena.

Sasa hizo blah blah zako ulizoorodhesha hapo ngoja nikupe hitimisho la nini kifanyike ili mambo yarudi.

1. Rais John Magufuli akae pembeni kwakuwa ameshaonekana hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwaunganisha watanzania wao kwa wao na kiiunganisha Tanzania na nchi zilizostaharabika.

2. Tuhuma zinazotolewa kila uchwao ziwekwe wazi na watu wapelekwe mbele ya sheria. Full stop

Hivi unakuaje na kiongozi wa nchi ambaye kila uchwao nchi inaenda kombo na bado hamuoni mnaishia kuandika andika uozo?

Hivi wewe mtu mpuuzi unaona kupotea kwa watu, kunyanyaswa na wengine kushambuliwa hadharani bila hatua zozote kuchukuliwa ni sawa? Nakuuliza ni sawa?

Acheni upumbavu bwana!
Acha kuvuruga uzi mzuri kwa tamaa yenu ya kuingia Ikulu kwa Mlango wa nyuma. Mwanakijiji ameongea vizuri kiukomavu, wewe ati Magufuli atoke! Huo ni utoto na ndoto za Abunuasi.
 
Diplomasia inasemaje kuhusu kuwasilisha ujumbe?
Tusitishwe na intelijensia
 
Bila hata ya Marekani, Watanzania wengi, kwa minong'ono na uwazi, tena si mara chache, wameonesha kwa uwazi kuwa huyu mtu ni mwovu.

Lakini kuna ukweli mdogo sana, kama upo, kuwa amekuwa akiyafanya anayoyafanya, kwa maamuzi yake, kwa nguvu zake na kwa hiari yake.

Kwenye mambo ya usalama huwa tunasema kuwa karibia ajali zote kubwa na zenye madhara makubwa sana, kwanza hutanguliwa na ajali (accidents) au matukio ya kiusalama (incidents), ambayo yalipuuzwa. Kwa ujinga tukilipuuza hili, tusubirie yale ambayo hata tukitaka kuyapuuza, hatutakuwa na uwezo wa kuyapuuza.

Uovu hata siku moja hauwezi kuwa wa kudumu.

Huu ni wakati wa kumhoji kwa nguvu aliyemteua Makonda kuliko Makonda mwenyewe. Wananchi tuendelee kuhoji. Bunge na wabunge wahoji - iwe ni hoja inayojitegemea na ijadiliwe. Wanaharakati wahoji. Taasisi za ndani na nje zihoji. Maana sote tunajua hakuna mwenye haki ya kuwaondolea watu haki ya kuishi zaidi ya Mungu pekee yake. Kwa nini Makonda amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi? Huyu siyo tu wa kumwondoa kwenye uongozi lakini kuundwe tume ya ndani itakayoshirikiana na hao Wamarekani, wamchunguze na ashtakiwe.
 
Kenge nyie hamjifunzi hadi mtoke damu... Mlikuwa mnaambiwa na kupewa tahadhari masikio mliweka pamba ... Leo Greencard lottery imezuiliwa kwa watanzania ndio mmeamka ... Stupid


Dawa yenu inachemshwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom