Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Kwani serikali haijui anayoyafanya Makonda? Wakichukua ushauri wako, tegemea mabaya zaidi. Ni sawa, nakuona wazi kabisa unaiba, halafu unaniambia, nikuoe ushahidi.
Hamna suluhu ambayo ni rafiki kwa taifa hili katika mtego huu zaidi ya wahusika kuwajibishwa
Bams umesema ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ningekuwa Kiongozi wa chama chochote Cha upinzani kuanzia kesho jtatu mpaka siku ya ijumaa tungekuwa na press conference kila siku kuzungumzia na kuhoji;

1. Aliko Azory Gwanda

2. Kupigwa risasi tundu lisu na case ipo inaelea tu.

3. Kutekwa kwa Mo dewj

4. Kuuawa kwal alphonce mawazo

5. Kubambikiwa kesi watu ... Mtu kaiba flash anapewa money laundering

6. Kuteswa kwa wanaharakati.

8. Kuvamiwa kwa clouds tv



Yaani ningehakikisha makaburi yote yanafukuliwa na vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimatifa wanapewa nakala ... Yaani wiki nzima ni coverage kuhusu hayo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona suala la Makonda kudhulumu haki ya kuishi kwa baadhi ya watu kama ilivyosemwa katika sababu nne za yeye kuzuiwa kuingia US..Hili haulisemi.

Kwamba Makonda anatuhumiwa kuuwa baadhi ya watu hili HAULISEMI KABISA..

Tuhuma kubwa na mbaya kama hii ya kumwaga damu kwako sio kitu.Na tayari kuna tuhuma huyu ndie alishiriki mwanzo mpaka mwisho kwenye kuutoa uhai wa Ben Saanane..

Umesimamia tu hapo haki za binadamu nk.

Ni wewe huko nyuma mambo yakiwa yanaenda mrama ulikuwa unaandika kwa namna ya kusifia tu..
Leo suala zito kama hili unaandika kwa namna ile ile..kama vile ni jambo rahisi-rahisi tu..

Kuwa muwazi..Makonda amedhulumu HAKI YA KUISHI ya baadhi ya watu na jpm anapaswa amuondoe sheria zichukue mkondo wake.

US hawawezi kulisema hili bila kuwa na ushahidi.
Nimemshangaa sana Mwanakijiji, kujikita kwenye hoja dhaifu na kuacha tuhuma mbaya kabisa dhidi ya Makonda, tuhuma ya kuwaondolea watu uhai. Mwanakijiji anaona hili ni dogo. Anaongelea tu kuwanyima watu haki za binadamu!!

Kwangu mimi, kiwango cha juu kabisa cha ushetani, ni uuaji. Muuaji hata angemgawia kila mtu ndege, kamwe siwezi hawezi kuwa kiongozi. Muuaji hana jina jingine zaidi ya hilo. Hastahili kuitwa kiongozi. Muuaji ni jambazi.
 
..... denial of the right to life, liberty, or the security of persons."

Mzee Mwanakijiji, hilo neno."denial" umelipooza kweli..Umeliita 'kutishia'' na siyo" kunyima". Wamarekani wamekua direct kabisa. Ushauri wako ungejikita kuwa mamlaka zijuzwe ni vipi RC amenyima watu hali za kua hai
 
Waungwana , tujiulize swala moja tu Kuhusu kushambuliwa kwa risasi kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Ndugu Tundu Lisu, kwenye makazi ya watumishi wa Serikali.
Na yaliyofuata baada ya hapo kuanzia upelelezi, matibabu,posho zake, ubunge wake na stahiki zake zote, je! Serikali ilimtendea haki?

Ukuta una masikio.
Mwenye macho haambiwi tazama.
Unapokaanga ujue na kufukuta.
 
Dawa ni rahisi sana hapo,kama Mh.Rais anampenda mteule wake amtoe kwenye nafasi hiyo ampe nyingine ambayo ni ya kiutendaji zaid kuliko hizi za kisiasa zinazomkutanisa na wananchi.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Muuaji apewe nafasi nyingine badala ya kupelekwa mbele ya vyombo vya kisheria? Are we serious? Hao walionyimwa haki yao ya kuishi, wana ndugu, wana familia, wana wazazi - sisi tunasema aliyewaondolea haki ya kuishi apewe nafasi nyingine. Hivi tumerogwa?
 
Marekani haikutaka kuvuruga uhusiano na Tanzania na badala yake imetuma ujumbe wa kirafiki. Watanzania bado wanaweza kwenda Marekani kwa shughuli zao mbalimbali. Kwamba, kama itakuja kulazimu basi hatua kali zaidi za uhamiaji zitachukuliwa. Huo nao ni ujumbe wa kidiplomasia; wenye onyo na ushauri ndani yake. Wamarekani wangetaka kupiga marufuku Watanzania wote wasiingie Marekani wangeweza ila hawakufanya hivyo.
Jibu liko hapa.. Na huu ni ujumbe kwa Magu ..
Wanadhani ataumia kwa Watanzania kuikosa hii nafasi..Lakini hana roho hiyo..

Amtume Musiba kuporomosha matusi tena kwa USA.
 
Kama makonda ana malengo ya kuendelea kisiasa basi hili zuio kwake litakua na athari katika safari yake ya kisiasa.....magu najua atakaa tu kimya
 
..... denial of the right to life, liberty, or the security of persons."

Mzee Mwanakijiji, hilo neno."denial" umelipooza kweli..Umeliita 'kutishia'' na siyo" kunyima". Wamarekani wamekua direct kabisa. Ushauri wako ungejikita kuwa mamlaka zijuzwe ni vipi RC amenyima watu hali za kua hai
DENIAL OF RIGHT TO LIFE- tafsiri ya moja kwa moja ni kumnyima mtu haki ya kuishi.
 
Kwa style ya awamu ya tano', Kuna mtu Kama sio Waziri,DC au RC ataibuka na kujibu majibu yasiyo na staha na kesho yake atapandisha cheo.

Ujumbe kwa JPM toka USA ni wazi kuwa "tunaelewa uhalifu unaofanya" Katika kiwango kama hiki labda tungehitaji mwanadiplomasi kiwango Cha Jakaya, lakini matendo na mwenendo wa awamu hii sio reliable
 
Yaani ningekuwa Kiongozi wa chama chochote Cha upinzani kuanzia kesho jtatu mpaka siku ya ijumaa tungekuwa na press conference kila siku kuzungumzia na kuhoji;

1. Aliko Azory Gwanda

2. Kupigwa risasi tundu lisu na case ipo inaelea tu.

3. Kutekwa kwa Mo dewj

4. Kuuawa kwal alphonce mawazo

5. Kubambikiwa kesi watu ... Mtu kaiba flash anapewa money laundering

6. Kuteswa kwa wanaharakati.

8. Kuvamiwa kwa clouds tv



Yaani ningehakikisha makaburi yote yanafukuliwa na vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimatifa wanapewa nakala ... Yaani wiki nzima ni coverage kuhusu hayo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya yote & zaidi ya haya wanayajua vizuri kwa hiyo ondoa hofu kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko hivi black and white apigwe chini kazi yake, akamatwe aliyetuhumiwa awekwe ndani wakati upelelezi unaendelea Kama wengine wote wanavyo tendwa! Kama hatuna ushahidi tuombe USA watupe ushahidi mda huo huo wazir wa mambo ya nje tumbadili maana anapwaya sana and all of those should have happened 24 hrs ago!

Lkn ntakwambia kitachotokea hawa washashupaza shingo hata uwashauri vipi ktk kumtoa mwana wa pekee hatomtoa kafara, ataendelea Kama alivyo wahi kutuambia pale ubungo kuwa yeye hashauriki! Kwa hiyo we are going all the way maana mwana anapendwa kuliko maslahi ya wengine wote!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Serikali ya Marekani ingeweza kuchukua hatua kali zaidi kuliko ambazo imechukua kwa nchi rafiki kama ya Tanzania. Tangu wakati wa Kikwete Tanzania imejisogeza zaidi na Serikali ya Marekani kiasi kwamba ni sawa kabisa kuamini kuwa tuna uhusiano wa karibu na wa kirafiki na Taifa hili lenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi duniani. Uamuzi wa kumzuia Paul Makonda na Mkewe kuingia Marekani na kuzuia Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani (Green Card Lotto) kwa wengine unaweza kuonekana ni mkali lakini kiuhalisia ni uamuzi mwepesi, na siyo mkali kwa kipimo chochote kile lakini ujumbe wake ni Dhahiri kabisa. Rafiki ameona kuna tatizo kwa rafiki yake.

Marekani kama ingetaka ingeweza kuchukua hatua kali zaidi ukiangalia sababu ilizotoa juu ya hatua ilizochukua. Kwenye tuhuma za uvunjaji wa haki za binadamu (kutishia maisha na usalama wa watu), kuminywa kwa uhuru wa habari, uhuru wa kukusanyika na kuwatenga watu kutoka makundi yanayotengwa mengi wangeweza kufanya. Kama Serikali ya Marekani inao ushahidi mzito dhidi ya viongozi wa serikali katika tuhuma hizo bila ya shaka wangeweza kuwaweka watu wengine kwenye zuio hilo la Marekani. Wangeweza kumzuia Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Upelelezi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) n.k.

Kitendo cha zuio lao kuliweka dhidi ya Paul Makonda na mke wake peke yao ni lazima liwekwe kwenye muktadha wake sahihi. Nje ya hapo tutakosa kukielewa kwa kinagaubaga kile ambacho Marekani imekifanya na matokeo yake kila mtu ataweka tafsiri isiyo sahihi. Kuna mambo kadhaa ya kuyaangalia.

US Wanajua Yote Wanayotaka Kujua Kuhusu Makonda

Kwanza, Marekani ina taarifa za kiinteligensia za nini Makonda amekifanya, na wapi amekifanya na namna gani amekifanya. Itakuwa ni makosa makubwa ya kudhania kuwa Zitto Kabwe, Maria Sarungi, Tundu Lissu na wanaharakati ndio wamesababisha Makonda afungiwe. Marekani haimhitaji Zitto, Sarungi au Lissu kujua kinachotokea. Kama kuna lolote wamefanya hawa inawezekana ni kidogo sana kulinganisha na Marekani ilivyopata taarifa zake. Fikiria tu kuwa Marekani iliweza kumpata Osama bin Laden katika maficho yake, Walimpata Abubakri Al-Baghdad na hivi majuzi wamemuua Gen. Kassam Suleimani wa Iran.

Ujumbe wa Kwanza

Katika matukio hayo matatu (Osama, Al-Baghdad, na Suleimani) Wamarekani wameendelea kuonesha dunia uwezo wao wa kiinteligensia iliyopitiliza. Mtandao wa CIA unavyofanya kazi kwa wanaolewa wanajua kabisa ni mzito na wa kina sana. Naomba kudokeza tu kuwa taarifa za kinachoendelea kwenye nchi yeyote CIA wanaweza kupata kwa mbinu nyingi sana na hazihitaji viongozi wa upinzani au wanaharakati. Hivyo basi, hadi Marekani iamue kumtaja na kumtenga Mkuu wa Mkoa Makonda na siyo RPC, RIO, DCI, au DPP wana maana yao. Wanasema “tunajua anachofanya Makonda na hakitufurahishi na kinatishia uhusiano kati ya Tanzania na Marekani”. Huu ndio ujumbe wao wa kwanza.

Ujumbe wa Pili

Hata hivyo Wamarekani kutokana na uwezo wao wa kiinteligensia wameonesha kuwa hadi hivi sasa taarifa walizo nazo hazijafikia kiwango cha kuinyoshea nchi na viongozi wa juu ya nchi kuwatuhumu uvunjaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia na haki mbalimbali za kiraia. Hawakuwa tayari kumtaja Rais Magufuli, Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa. Hawakuwa tayari kumtaja Kapilimba au Diwani, hawakuwa tayari kumtaja Sirro au Mabeyo au Afisa yeyote wa usalama wa ngazi yoyote ile. Hili si jambo dogo; Wamarekani hawaiogopi Tanzania (hatuna cha kuwafanya) na hivyo kama wangetaka kumtaja yeyote kati yao kuwa anahusika na utekaji, uuaji au idara yake inahusika na mambo hayo wangemtaja na katazo lao lingekuwa pana zaidi. Ni wazi kwa kuliweka katazo lao juu ya afisa wa ngazi ya chini wa serikali wanataka kutuambia na kuwaambia viongozi wetu wa juu wafikirie kinachofanywa na huyu bwana kwani kinaweza kuleta matatizo makubwa ya kidemokrasia.

Ujumbe wa Tatu

Katika maamuzi yao Wamarekani hawakumpa katazo kali zaidi Makonda. Kwa kweli ukiangalia utaona kuwa ni katazo jepesi sana. Wamarekani wangetaka siyo tu wangempiga yeye marufuku lakini wangefunga akaunti zake (kama anazo), uwekezaji wake wowote unaofanywa na Makonda au watu wake wa karibu wanaoweza kuwa wanahusika na yale ambayo Wamarekani wanamtuhumu. Kwa maneno mengine, wamempa Makonda nafasi ya kujionesha kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi na hazina ushahidi wowote ule. Hivyo, ujumbe wa tatu ni kwa Makonda mwenyewe. Ni wazi kuwa, kama Makonda alikuwa na mpango wowote wa kuja Marekani mpango huo sasa umekufa. Kama kuna jambo lolote ambalo alihitaji kuja kulifanya hapa (binafsi au kwa niaba ya Mkoa wake) jambo hilo kwa sasa limekufa. Ajitafakari na Mamlaka iliyomteua itafakari kama inataka mtu anayeongoza Mkoa wenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa Tanzania asiwe na uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri na Marekani. Je, inastahili kuvuruga uhusiano na Marekani kwa sababu ya Makonda?

Ujumbe wa Nne

Kwenye maamuzi yao Wamarekani wamepiga marufuku Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani ambayo hatimaye humpa mtu nafasi ya kupata uraia wa Marekani. Visa hii hutolewa kwa njia ya bahati nasibu kwa nafasi 55,000 kila mwaka na kwa Bara la Afrika tunapata nafasi karibu nusu ya hizo. Nchi ambazo hazijatoa washindi wengi hupewa zaidi na zile ambazo zimetoa wengi huko nyuma hupunguziwa. Miaka ya karibuni Watanzania wameanza kushinda na kupata nafasi hizo. Ikumbukwe kuwa aina hii ya Visa tayari inapigwa vita na Rais Donald Trump ambaye anataka kuifuta kwani inawapa nafasi siyo tu wale walioshinda kuingia Marekani bali hata familia zao na ndugu wa karibu.

Hivyo kuzuia nafasi hiyo kumeondoa nafasi kwa Watanzania ambao wangependa kujaribu maisha huko Marekani. Hata hivyo, kiukweli kabisa uamuzi huu ni mdogo sana kuliko ambao watu walihofia. Marekani ikitaka watu wa nchi fulani wasiingie inaweka zuio kali zaidi. Hata hivyo, kwa Tanzania haikufanya hivyo; badala yake imeweka zuio kwenye program ambayo labda watu wachache sana inawahusu. Na hapa kuna ujumbe; Marekani haikutaka kuvuruga uhusiano na Tanzania na badala yake imetuma ujumbe wa kirafiki. Watanzania bado wanaweza kwenda Marekani kwa shughuli zao mbalimbali. Kwamba, kama itakuja kulazimu basi hatua kali zaidi za uhamiaji zitachukuliwa. Huo nao ni ujumbe wa kidiplomasia; wenye onyo na ushauri ndani yake. Wamarekani wangetaka kupiga marufuku Watanzania wote wasiingie Marekani wangeweza ila hawakufanya hivyo.

Serikali Ijibu Vipi Marekani?

Swali kubwa ni je Serikali ijibu vipi Marekani kutokana na hatua hizi mbili? Serikali ya Tanzania kama nchi huru na yenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali inatakiwa kupima mwitikio wake. Lakini ili itoe mwitikio sahihi ni lazima ijioneshe imeelewa kwa muktadha sahihi hatua zilizochukuliwa na Marekani. Ukweli ni kuwa Marekani haijachukua hatua kali sana za kidiplomasia; imechukua hatua za chini zaidi kulinganisha na hatua zilizochukuliwa kwa nchi kama Venezuela, Iran, Cuba, na Korea ya Kaskazini. Kutokana na ukweli huu basi kuna mambo au hatua kadhaa serikali inaweza kuchukua.

  • Serikali Inaweza Kupuuzia Tuhuma na Hatua za Marekani
  • Serikali ya Tanzania inaweza ikapuuzia na kuona kuwa hoja za Marekani hazina msingi, tuhuma zake hazina ushahidi na hatua zilizochukuliwa hazina ulazima wowote. Kwa maneno mengine, serikali inaweza kusema “Marekani inasema uongo”. Lakini ili iweze kusema hivi na kufanya hivi ni lazima iwe na ushahidi kinyume. Na hivyo, kwa vile Makonda na Mkewe hawana mpango wa kwenda Marekani siku yoyote ya karibuni na kuwa Serikali haijali hizo Visa za bahati nasibu basi serikali inaweza kusema “tunaheshimu uamuzi wa Marekani japo hatukubaliani nao” halafi ikaendelea na mambo yake.

  • Serikali Inaweza Kuhoji na Kupinga Hatua za Marekani
  • Ikionesha kuwa imechukizwa Serikali inaweza kubeza, kupinga na kukataa hatua za Marekani. Inaweza ikasema “tuhuma hazina msingi na zina lengo la kuichafua Tanzania”. Na ikipenda inaweza kumuita Balozi wa Marekani (Naibu Balozi) na kutoa pingamizi la kidiplomasia (diplomatic protest). Lakini inaweza ikataka maelezo ya ushahidi ambao Serikali ya Marekani inayo ya kuhusika kwa Makonda katika uvunjaji wa haki za binadamu, kuvuruga haki za watu kuishi na uminyaji wa demokrasia na haki za kiraia zilizoanishwa Kikatiba na kulindwa na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania imeridhia. Ikifanya hivi Serikali itakuwa imeamua kufuata njia ya kuchochea (elevate) mgogoro kutoka wa afisa wa chini wa Serikali na kuiingiza Serikali nzima na hivyo kutoa nafasi kwa Marekani kuongeza kibano zaidi kwa watu zaidi – nje ya Makonda. Binafsi ningependa kuwajua hao watu ni kina nani maana Makonda (kama kweli anavyodaiwa kufanya) hayupo peke yake.

  • Na katika kupinga kwake Serikali inaweza ikaamua na yenyewe kujibu mashambulizi kiaina. Sijui tunaweza kumpiga nani marufuku kuingia Marekani kwa tuhuma gani! Na sijui ni Visa za aina gani tunaweza kuwakataza Wamarekani kuja Tanzania. Lakini pia itakuwa ni ku-escalate (kufanya jambo dogo kuwa kubwa zaidi). Itakuwa njia sahihi?

  • Eritrea ambao nao wamewekewa vizuizi na Marekani inaonekana wamechagua aina ya jibu hili na kutoa kauli kali ya kupinga katazo au marufuku hiyo ya Marekani.

  • Serikali Inaweza Kuzingatia Tuhuma na Kuzipa Uzito Unaostahili
  • Kama nilivyosema hapo juu kwa namna moja Marekani imeinyoshea kidole Serikali na kinamna imemnyoshea kidole Rais Magufuli bila kupiga kelele sana. Kwa vile Makonda ni mteuliwa wa Rais ni wazi kuwa wanataka kumwambia Magufuli kuwa kama kuna jambo halijui basi mteuliwa wake anahusishwa na mambo mabaya (yanayoweza kupakana na uhalifu au uhalifu dhidi ya ubinadamu – crimes against humanity). Wamarekani wanataka kuona ni nani kweli anamlinda Makonda na kama mambo yanafanywa na Makonda yana baraka na viongozi wa juu wa serikali. Jinsi gani Serikali itaitikia ndio mtego ulipo; je itajitokeza na kumlinda Makonda kwa nguvu zote au itatulia na kumuita Makonda na kuhoji (labda baada ya kuwasiliana na Marekani).

  • Je, Serikali itakuwa tayari kuona Watanzania wengine wanaadhibiwa (kwa kunyimwa Visa) kwa sababu ya mtu mmoja? Je, kuna vitu ambavyo inawezekana vinahitaji kuangaliwa kwa uzito unaostahili na kuonesha dunia na Watanzania kuwa Serikali kweli inaamini katika haki za binadamu na uhuru wa kidemokrasia?

  • Kwa mfano, suala la kuhakikisha kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki lina mtego. Uchaguzi hauwi huru na wa haki siku ya uchaguzi tu bali mazingira yote yanayohusiana na uchaguzi yako vipi? Hili Marekani wanafuatilia vinginevyo tunaweza kujikuta kwenye mgogoro mkubwa sana kama wa Zimbabwe kati ya Mugabe na Morgan Tsvangirai. Kweli uchaguzi unaweza kufanyika Oktoba lakini hawa hawa wakasema toka Januari tuliona kuna matatizo Tanzania na hawakusikia na hivyo uchaguzi huu haukuwa huru (hata kama sisi tutauita hivyo). Hili lilitokea kwa Maduro wa Venezuela. Binafsi siamini kama tutafika huko lakini sioni kwanini watu wapewe sababu ya kudhania kuwa tunaweza kufika huko!

  • Kama Serikali (Rais Magufuli) mwenyewe ataona kuwa jambo hili ni zito kweli basi suala la Makonda linaweza kuwa ni jambo lilotegwa kwake. Maana baada ya Marekani kufanya walivyofanya sitoshangaa siku chache zijazo washirika wake nchi za EU na Uingereza zinaweza nazo kutoa matamko ya aina hiyo na hivyo kulikuza jambo hili.

  • Nigeria ambao nao wamepigwa marufuku kali zaidi kuliko ile ya Tanzania wameamua kuchukua kwa uzito wake katazo hili hasa ukizingatia ukaribu wao na Marekani na wameamua kuunda Kamati Maalum ya kuchunguzi madai yaliyosababisha Marekani ipige marufuku wananchi wake kuingia Marekani.
Hekima Itatamalaki?

Ndugu zangu, kati ya hatua hizo tatu Serikali ina mambo ya kupima kabla ya kufanya. Inaweza ikaamua kupimana nguvu na Marekani kidiplomasia au inaweza ikatafakari na kuona ni njia ipi itapunguza na kulifanya jambo hili lisiwe kubwa zaidi. Ni hatua gani itachukua kuonesha kweli inaheshimu haki za binadamu na haki za kidemokrasia; itajionesha ni kwa namna gani Makonda si mtu ambaye anaweza kutishia haki za kidemokrasia kwa mtu yeyote yule. Ni kwa sababu hiyo swali kubwa linalohitaji kujibiwa baada ya tafakari hii ni je hekima inaweza vipi kutamalaki?

Muda utatupa majibu.

Niandikie: [email protected]
miiforums.com
Mara nyingi watu wenye matendo ya kishetani wanapenda sana kumtaja Mungu hadharani,Makonda ni moja ya watu hatari kutokea Tanzania
 
Back
Top Bottom