Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Kutamalaki kwa Hekima: Serikali ijibu vipi Marekani na kwanini? Mtego wa Ikulu

Na. M. M. Mwanakijiji

Serikali ya Marekani ingeweza kuchukua hatua kali zaidi kuliko ambazo imechukua kwa nchi rafiki kama ya Tanzania. Tangu wakati wa Kikwete Tanzania imejisogeza zaidi na Serikali ya Marekani kiasi kwamba ni sawa kabisa kuamini kuwa tuna uhusiano wa karibu na wa kirafiki na Taifa hili lenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi duniani. Uamuzi wa kumzuia Paul Makonda na Mkewe kuingia Marekani na kuzuia Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani (Green Card Lotto) kwa wengine unaweza kuonekana ni mkali lakini kiuhalisia ni uamuzi mwepesi, na siyo mkali kwa kipimo chochote kile lakini ujumbe wake ni Dhahiri kabisa. Rafiki ameona kuna tatizo kwa rafiki yake.

Marekani kama ingetaka ingeweza kuchukua hatua kali zaidi ukiangalia sababu ilizotoa juu ya hatua ilizochukua. Kwenye tuhuma za uvunjaji wa haki za binadamu (kutishia maisha na usalama wa watu), kuminywa kwa uhuru wa habari, uhuru wa kukusanyika na kuwatenga watu kutoka makundi yanayotengwa mengi wangeweza kufanya. Kama Serikali ya Marekani inao ushahidi mzito dhidi ya viongozi wa serikali katika tuhuma hizo bila ya shaka wangeweza kuwaweka watu wengine kwenye zuio hilo la Marekani. Wangeweza kumzuia Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Upelelezi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) n.k.

Kitendo cha zuio lao kuliweka dhidi ya Paul Makonda na mke wake peke yao ni lazima liwekwe kwenye muktadha wake sahihi. Nje ya hapo tutakosa kukielewa kwa kinagaubaga kile ambacho Marekani imekifanya na matokeo yake kila mtu ataweka tafsiri isiyo sahihi. Kuna mambo kadhaa ya kuyaangalia.

US Wanajua Yote Wanayotaka Kujua Kuhusu Makonda

Kwanza, Marekani ina taarifa za kiinteligensia za nini Makonda amekifanya, na wapi amekifanya na namna gani amekifanya. Itakuwa ni makosa makubwa ya kudhania kuwa Zitto Kabwe, Maria Sarungi, Tundu Lissu na wanaharakati ndio wamesababisha Makonda afungiwe. Marekani haimhitaji Zitto, Sarungi au Lissu kujua kinachotokea. Kama kuna lolote wamefanya hawa inawezekana ni kidogo sana kulinganisha na Marekani ilivyopata taarifa zake. Fikiria tu kuwa Marekani iliweza kumpata Osama bin Laden katika maficho yake, Walimpata Abubakri Al-Baghdad na hivi majuzi wamemuua Gen. Kassam Suleimani wa Iran.

Ujumbe wa Kwanza

Katika matukio hayo matatu (Osama, Al-Baghdad, na Suleimani) Wamarekani wameendelea kuonesha dunia uwezo wao wa kiinteligensia iliyopitiliza. Mtandao wa CIA unavyofanya kazi kwa wanaolewa wanajua kabisa ni mzito na wa kina sana. Naomba kudokeza tu kuwa taarifa za kinachoendelea kwenye nchi yeyote CIA wanaweza kupata kwa mbinu nyingi sana na hazihitaji viongozi wa upinzani au wanaharakati. Hivyo basi, hadi Marekani iamue kumtaja na kumtenga Mkuu wa Mkoa Makonda na siyo RPC, RIO, DCI, au DPP wana maana yao. Wanasema “tunajua anachofanya Makonda na hakitufurahishi na kinatishia uhusiano kati ya Tanzania na Marekani”. Huu ndio ujumbe wao wa kwanza.

Ujumbe wa Pili

Hata hivyo Wamarekani kutokana na uwezo wao wa kiinteligensia wameonesha kuwa hadi hivi sasa taarifa walizo nazo hazijafikia kiwango cha kuinyoshea nchi na viongozi wa juu ya nchi kuwatuhumu uvunjaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia na haki mbalimbali za kiraia. Hawakuwa tayari kumtaja Rais Magufuli, Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa. Hawakuwa tayari kumtaja Kapilimba au Diwani, hawakuwa tayari kumtaja Sirro au Mabeyo au Afisa yeyote wa usalama wa ngazi yoyote ile. Hili si jambo dogo; Wamarekani hawaiogopi Tanzania (hatuna cha kuwafanya) na hivyo kama wangetaka kumtaja yeyote kati yao kuwa anahusika na utekaji, uuaji au idara yake inahusika na mambo hayo wangemtaja na katazo lao lingekuwa pana zaidi. Ni wazi kwa kuliweka katazo lao juu ya afisa wa ngazi ya chini wa serikali wanataka kutuambia na kuwaambia viongozi wetu wa juu wafikirie kinachofanywa na huyu bwana kwani kinaweza kuleta matatizo makubwa ya kidemokrasia.

Ujumbe wa Tatu

Katika maamuzi yao Wamarekani hawakumpa katazo kali zaidi Makonda. Kwa kweli ukiangalia utaona kuwa ni katazo jepesi sana. Wamarekani wangetaka siyo tu wangempiga yeye marufuku lakini wangefunga akaunti zake (kama anazo), uwekezaji wake wowote unaofanywa na Makonda au watu wake wa karibu wanaoweza kuwa wanahusika na yale ambayo Wamarekani wanamtuhumu. Kwa maneno mengine, wamempa Makonda nafasi ya kujionesha kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi na hazina ushahidi wowote ule. Hivyo, ujumbe wa tatu ni kwa Makonda mwenyewe. Ni wazi kuwa, kama Makonda alikuwa na mpango wowote wa kuja Marekani mpango huo sasa umekufa. Kama kuna jambo lolote ambalo alihitaji kuja kulifanya hapa (binafsi au kwa niaba ya Mkoa wake) jambo hilo kwa sasa limekufa. Ajitafakari na Mamlaka iliyomteua itafakari kama inataka mtu anayeongoza Mkoa wenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa Tanzania asiwe na uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri na Marekani. Je, inastahili kuvuruga uhusiano na Marekani kwa sababu ya Makonda?

Ujumbe wa Nne

Kwenye maamuzi yao Wamarekani wamepiga marufuku Watanzania kushiriki bahati nasibu ya Visa ya kuishi na kufanya kazi Marekani ambayo hatimaye humpa mtu nafasi ya kupata uraia wa Marekani. Visa hii hutolewa kwa njia ya bahati nasibu kwa nafasi 55,000 kila mwaka na kwa Bara la Afrika tunapata nafasi karibu nusu ya hizo. Nchi ambazo hazijatoa washindi wengi hupewa zaidi na zile ambazo zimetoa wengi huko nyuma hupunguziwa. Miaka ya karibuni Watanzania wameanza kushinda na kupata nafasi hizo. Ikumbukwe kuwa aina hii ya Visa tayari inapigwa vita na Rais Donald Trump ambaye anataka kuifuta kwani inawapa nafasi siyo tu wale walioshinda kuingia Marekani bali hata familia zao na ndugu wa karibu.

Hivyo kuzuia nafasi hiyo kumeondoa nafasi kwa Watanzania ambao wangependa kujaribu maisha huko Marekani. Hata hivyo, kiukweli kabisa uamuzi huu ni mdogo sana kuliko ambao watu walihofia. Marekani ikitaka watu wa nchi fulani wasiingie inaweka zuio kali zaidi. Hata hivyo, kwa Tanzania haikufanya hivyo; badala yake imeweka zuio kwenye program ambayo labda watu wachache sana inawahusu. Na hapa kuna ujumbe; Marekani haikutaka kuvuruga uhusiano na Tanzania na badala yake imetuma ujumbe wa kirafiki. Watanzania bado wanaweza kwenda Marekani kwa shughuli zao mbalimbali. Kwamba, kama itakuja kulazimu basi hatua kali zaidi za uhamiaji zitachukuliwa. Huo nao ni ujumbe wa kidiplomasia; wenye onyo na ushauri ndani yake. Wamarekani wangetaka kupiga marufuku Watanzania wote wasiingie Marekani wangeweza ila hawakufanya hivyo.

Serikali Ijibu Vipi Marekani?

Swali kubwa ni je Serikali ijibu vipi Marekani kutokana na hatua hizi mbili? Serikali ya Tanzania kama nchi huru na yenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali inatakiwa kupima mwitikio wake. Lakini ili itoe mwitikio sahihi ni lazima ijioneshe imeelewa kwa muktadha sahihi hatua zilizochukuliwa na Marekani. Ukweli ni kuwa Marekani haijachukua hatua kali sana za kidiplomasia; imechukua hatua za chini zaidi kulinganisha na hatua zilizochukuliwa kwa nchi kama Venezuela, Iran, Cuba, na Korea ya Kaskazini. Kutokana na ukweli huu basi kuna mambo au hatua kadhaa serikali inaweza kuchukua.

  • Serikali Inaweza Kupuuzia Tuhuma na Hatua za Marekani
  • Serikali ya Tanzania inaweza ikapuuzia na kuona kuwa hoja za Marekani hazina msingi, tuhuma zake hazina ushahidi na hatua zilizochukuliwa hazina ulazima wowote. Kwa maneno mengine, serikali inaweza kusema “Marekani inasema uongo”. Lakini ili iweze kusema hivi na kufanya hivi ni lazima iwe na ushahidi kinyume. Na hivyo, kwa vile Makonda na Mkewe hawana mpango wa kwenda Marekani siku yoyote ya karibuni na kuwa Serikali haijali hizo Visa za bahati nasibu basi serikali inaweza kusema “tunaheshimu uamuzi wa Marekani japo hatukubaliani nao” halafi ikaendelea na mambo yake.

  • Serikali Inaweza Kuhoji na Kupinga Hatua za Marekani
  • Ikionesha kuwa imechukizwa Serikali inaweza kubeza, kupinga na kukataa hatua za Marekani. Inaweza ikasema “tuhuma hazina msingi na zina lengo la kuichafua Tanzania”. Na ikipenda inaweza kumuita Balozi wa Marekani (Naibu Balozi) na kutoa pingamizi la kidiplomasia (diplomatic protest). Lakini inaweza ikataka maelezo ya ushahidi ambao Serikali ya Marekani inayo ya kuhusika kwa Makonda katika uvunjaji wa haki za binadamu, kuvuruga haki za watu kuishi na uminyaji wa demokrasia na haki za kiraia zilizoanishwa Kikatiba na kulindwa na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania imeridhia. Ikifanya hivi Serikali itakuwa imeamua kufuata njia ya kuchochea (elevate) mgogoro kutoka wa afisa wa chini wa Serikali na kuiingiza Serikali nzima na hivyo kutoa nafasi kwa Marekani kuongeza kibano zaidi kwa watu zaidi – nje ya Makonda. Binafsi ningependa kuwajua hao watu ni kina nani maana Makonda (kama kweli anavyodaiwa kufanya) hayupo peke yake.

  • Na katika kupinga kwake Serikali inaweza ikaamua na yenyewe kujibu mashambulizi kiaina. Sijui tunaweza kumpiga nani marufuku kuingia Marekani kwa tuhuma gani! Na sijui ni Visa za aina gani tunaweza kuwakataza Wamarekani kuja Tanzania. Lakini pia itakuwa ni ku-escalate (kufanya jambo dogo kuwa kubwa zaidi). Itakuwa njia sahihi?

  • Eritrea ambao nao wamewekewa vizuizi na Marekani inaonekana wamechagua aina ya jibu hili na kutoa kauli kali ya kupinga katazo au marufuku hiyo ya Marekani.

  • Serikali Inaweza Kuzingatia Tuhuma na Kuzipa Uzito Unaostahili
  • Kama nilivyosema hapo juu kwa namna moja Marekani imeinyoshea kidole Serikali na kinamna imemnyoshea kidole Rais Magufuli bila kupiga kelele sana. Kwa vile Makonda ni mteuliwa wa Rais ni wazi kuwa wanataka kumwambia Magufuli kuwa kama kuna jambo halijui basi mteuliwa wake anahusishwa na mambo mabaya (yanayoweza kupakana na uhalifu au uhalifu dhidi ya ubinadamu – crimes against humanity). Wamarekani wanataka kuona ni nani kweli anamlinda Makonda na kama mambo yanafanywa na Makonda yana baraka na viongozi wa juu wa serikali. Jinsi gani Serikali itaitikia ndio mtego ulipo; je itajitokeza na kumlinda Makonda kwa nguvu zote au itatulia na kumuita Makonda na kuhoji (labda baada ya kuwasiliana na Marekani).

  • Je, Serikali itakuwa tayari kuona Watanzania wengine wanaadhibiwa (kwa kunyimwa Visa) kwa sababu ya mtu mmoja? Je, kuna vitu ambavyo inawezekana vinahitaji kuangaliwa kwa uzito unaostahili na kuonesha dunia na Watanzania kuwa Serikali kweli inaamini katika haki za binadamu na uhuru wa kidemokrasia?

  • Kwa mfano, suala la kuhakikisha kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki lina mtego. Uchaguzi hauwi huru na wa haki siku ya uchaguzi tu bali mazingira yote yanayohusiana na uchaguzi yako vipi? Hili Marekani wanafuatilia vinginevyo tunaweza kujikuta kwenye mgogoro mkubwa sana kama wa Zimbabwe kati ya Mugabe na Morgan Tsvangirai. Kweli uchaguzi unaweza kufanyika Oktoba lakini hawa hawa wakasema toka Januari tuliona kuna matatizo Tanzania na hawakusikia na hivyo uchaguzi huu haukuwa huru (hata kama sisi tutauita hivyo). Hili lilitokea kwa Maduro wa Venezuela. Binafsi siamini kama tutafika huko lakini sioni kwanini watu wapewe sababu ya kudhania kuwa tunaweza kufika huko!

  • Kama Serikali (Rais Magufuli) mwenyewe ataona kuwa jambo hili ni zito kweli basi suala la Makonda linaweza kuwa ni jambo lilotegwa kwake. Maana baada ya Marekani kufanya walivyofanya sitoshangaa siku chache zijazo washirika wake nchi za EU na Uingereza zinaweza nazo kutoa matamko ya aina hiyo na hivyo kulikuza jambo hili.

  • Nigeria ambao nao wamepigwa marufuku kali zaidi kuliko ile ya Tanzania wameamua kuchukua kwa uzito wake katazo hili hasa ukizingatia ukaribu wao na Marekani na wameamua kuunda Kamati Maalum ya kuchunguzi madai yaliyosababisha Marekani ipige marufuku wananchi wake kuingia Marekani.
Hekima Itatamalaki?

Ndugu zangu, kati ya hatua hizo tatu Serikali ina mambo ya kupima kabla ya kufanya. Inaweza ikaamua kupimana nguvu na Marekani kidiplomasia au inaweza ikatafakari na kuona ni njia ipi itapunguza na kulifanya jambo hili lisiwe kubwa zaidi. Ni hatua gani itachukua kuonesha kweli inaheshimu haki za binadamu na haki za kidemokrasia; itajionesha ni kwa namna gani Makonda si mtu ambaye anaweza kutishia haki za kidemokrasia kwa mtu yeyote yule. Ni kwa sababu hiyo swali kubwa linalohitaji kujibiwa baada ya tafakari hii ni je hekima inaweza vipi kutamalaki?

Muda utatupa majibu.

Niandikie: [email protected]
miiforums.com
Eboooh.! Huyu kenge hana uwezo wa kuwekeza marekani.. [emoji23] [emoji23]

Kingine utambue kuwa USA wanajua fika bashite anafanya haya kwa kutumwa na nani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mwanakijiji

Hili swala kwa muktadha wake wala sio kubwa sana na wala Tanzania sio nchi ya kwanza kuwekewa vikwazo vya namna hiyo, ishu kubwa ni kwamba hili swala limekaa kimtego.

Rais wetu wote tunamfahamu kwenye maswala ya kufanya maamuzi huwa hakubali kupangiwa, hili swala kwakwe na kwetu litakuwa rahisi sana kama team leader atakubali kurudi nyuma na kuamua kujiuliza wapi alipokosea na kujirekebisha, tofauti na hapo akikaza shingo atalikuza hili jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
lini alikubali kirahisi kuwa kakosea
 
Nandio tageti hao.
-Hao akina Pempeo hamna kitu wanatafuta kura mwezi nov mwaka huu. Walijaribu kutafuta kura kwa Soleiman wa Iran, Iran wakawatuliza mara moja, hawaku score points yoyote.
-Hao akina Pempeo wameona Magufuli kumbe wanaweza negotiate naye ktk interests zao, na ili aende ktk negotiating table lazima wa mpush na ku trigger kama hivyo. Hapo wanamtaka Magufuli akae nao chini kuwahakikishia masilahi yao, kama tukitaka kuipiga Iran utatoa wanajeshi kutuunga something like that.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si mlikuwa mkisifia kwa kauli mbiu ya "Go Magufuli go" wewe na Slaa wako! Sasa kwa taarifa yako ni kuwa main target ni Dr. John Pombe Magufuli.

Serikali wajibu, wasijibu, waongee, wasiongee, wapuuze, wasipuuze it's too late. Makonda alituhumiwa kwa mauaji wazi wazi na hadi huku JF tukamuita Malyamungu bado mkaona tunaona wivu eti mchapakazi. Serikali ya Rais Magufuli imeshakosa credibility nje na ndani ya nchi haifai tena.

Sasa hizo blah blah zako ulizoorodhesha hapo ngoja nikupe hitimisho la nini kifanyike ili mambo yarudi.

1. Rais John Magufuli akae pembeni kwakuwa ameshaonekana hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwaunganisha watanzania wao kwa wao na kiiunganisha Tanzania na nchi zilizostaharabika.

2. Tuhuma zinazotolewa kila uchwao ziwekwe wazi na watu wapelekwe mbele ya sheria. Full stop

Hivi unakuaje na kiongozi wa nchi ambaye kila uchwao nchi inaenda kombo na bado hamuoni mnaishia kuandika andika uozo?

Hivi wewe mtu mpuuzi unaona kupotea kwa watu, kunyanyaswa na wengine kushambuliwa hadharani bila hatua zozote kuchukuliwa ni sawa? Nakuuliza ni sawa?

Acheni upumbavu bwana!
Acha hasira,, pigania tume huru ili oktoba usije tena kulia lia humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe alivo hana akili hatojibu!ataishia kutumbua tu kama anavotumbuaga!!!naona mzee mwanakijiji umekuja ku Neutralize situation!!!!
 
Jiwe alivo hana akili hatojibu!ataishia kutumbua tu kama anavotumbuaga!!!naona mzee mwanakijiji umekuja ku Neutralize situation!!!!
 
Niambie ni nchi gani waliyowahi kuingilia masuala yake ya ndani iko salama kwa sasa ,toa mfano,
Hao huwa wako kimaslahi zaidi,Jamal Kashog kanyongwa kinyama umeona wametia neno kwa mtoto wa mfalme?,akili ya kuambiwa changanya na zako ,mbwiga wewe
Bora kuongozwa na hao mababylon maana hawa washamba wenzetu hawajitambui. Huu sio muda wa kiongozi kutuongoza kwa utashi wake, maana sisi sio familia yake. Aheshimu chaguzi, na afahamu kwenye mfumo wa vyama vingi kukosolewa ndio kanuni namba moja ya uongozi. Hawezi akae pembeni, maana tuna akili timamu na tunaona hao wazungu wanachohoji kiko wazi maana ni kilio chetu cha muda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee MwanaKisosora, kudos to you, hii ni bonge ya uchambuzi na ushauri, Infact Washauri wa Raisi au Waziri Kabudi, wange fanya jitahada ya COPY PASTE na kumkabidhi Raisi period.

Choices , zote zipo hapa ni kufumba macho na patakapo angukia kidole ndio uwe uchaguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Kesi za watu wote waliopotea zifunguliwe na wahusika wapelekwe mahakamani
2.Uhuru wa kutoa maoni uheshimiwe..sheria kandamizi zote pamaja na matamko ya wanasiasa au polisi yanayochochea ukundamizaji wa haki za watu yachunguzwe na wahusika wote wachukuliwe hatua
3.Serikali itoe semina kwa viongozi wake hasa wa ngazi za juu...speaker etc....waangalie kauli wanazozitumia...wajifunze kuwa na vifua vya kuongea machache yanayohitajika kuongeleka mbele ya watu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niambie ni nchi gani waliyowahi kuingilia masuala yake ya ndani iko salama kwa sasa ,toa mfano,
Hao huwa wako kimaslahi zaidi,Jamal Kashog kanyongwa kinyama umeona wametia neno kwa mtoto wa mfalme?,akili ya kuambiwa changanya na zako ,mbwiga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app

Hatujali walipoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine nini kiliendelea, ila tunachojua hapa nchini kwetu kuna uonevu kwa wapinzani na hawana la kufanya zaidi ya kunyanyaswa, hivyo acha waingilie ili tuheshimiane. Sio juu yao wakiingilia kuwe na amani, bali ni juu yetu kuacha kuoneana, na kama hilo halitendeki tutakuwa jeuri yetu. Naomba waje hata kesho, ili nyie mnao faidika na huu ukatili tuwe sawa.
 
Haya Sasa, Pompeo amjibu kabudi
 

Attachments

  • IMG-20200202-WA0085.jpg
    IMG-20200202-WA0085.jpg
    25.2 KB · Views: 16
Si mlikuwa mkisifia kwa kauli mbiu ya "Go Magufuli go" wewe na Slaa wako! Sasa kwa taarifa yako ni kuwa main target ni Dr. John Pombe Magufuli.

Serikali wajibu, wasijibu, waongee, wasiongee, wapuuze, wasipuuze it's too late. Makonda alituhumiwa kwa mauaji wazi wazi na hadi huku JF tukamuita Malyamungu bado mkaona tunaona wivu eti mchapakazi. Serikali ya Rais Magufuli imeshakosa credibility nje na ndani ya nchi haifai tena.

Sasa hizo blah blah zako ulizoorodhesha hapo ngoja nikupe hitimisho la nini kifanyike ili mambo yarudi.

1. Rais John Magufuli akae pembeni kwakuwa ameshaonekana hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwaunganisha watanzania wao kwa wao na kiiunganisha Tanzania na nchi zilizostaharabika.

2. Tuhuma zinazotolewa kila uchwao ziwekwe wazi na watu wapelekwe mbele ya sheria. Full stop

Hivi unakuaje na kiongozi wa nchi ambaye kila uchwao nchi inaenda kombo na bado hamuoni mnaishia kuandika andika uozo?

Hivi wewe mtu mpuuzi unaona kupotea kwa watu, kunyanyaswa na wengine kushambuliwa hadharani bila hatua zozote kuchukuliwa ni sawa? Nakuuliza ni sawa?

Acheni upumbavu bwana!
Aisee asante Kwa hii comment yako.
Ukitaka kujua serikali ya magufuli imekalia kidole cha Kati Kwenye ishu hii ya MAKONDA ni namna walivyokuwa wapole hakuna kiongozi yeyote anayetaja jina la beberu maana wanajua Tanzania ipo hatarini na kadiri watakavyokuwa wanajibu ndipo wanapozidi kuangamia zaidi
 
Back
Top Bottom