Kutana na akili kubwa ya Rais Kagame, one of the best President, the dream of Africa

Hamia Rwanda
 
Crap… 💩
 
Hakuna mahali popote alipo mswahili tena mbaya kabisa awe kiongozi pamewahi kufanikiwa..culture ya kiarabu ni mafanikio kupitia ushirikina..na wivu mwingi kwa anayefanikiwa, angalia comments za waswahili hapa utakubali ninachosema..lakini Rais Kagame ameibadilisha Rwanda, tafuta Nchi Africa hii iliyopitia disaster km ya Rwanda km hata tu wana shirika la ndege linalomilikiwa na serikali..! watanzania tuvae makobazi tu na kaunda suti lkn, maendeleo tusahau..nchi inatambikiwa wananchi wawe km mazombie, miezi zaidi ya 7 sasa mgao wa umeme halafu watu wako km majuha wanakashifu nchi zingine wanasahau matatizo waliyo nayo ya kujitakia..kuna maendeleo hapo? SAHAU!
 
Tukiwa vijana, Mwalimu Nyerere aliwahi sema, mtu mbaya usipoweza kumfanya lolote, mzomeeni tu!
Mtu kama huyu bado anaota kauli za miaka 50 iliyopita na kuzifanya reference ya zama hizi..na ukute huyu labda ni mwenyekiti wa mtaa au balozi.., hao wengine si ni majanga!
 
Hamia Rwanda.
 
Huyo DIKTETA mchukue akatawale familia yako. Hatutaki MADIKTETA Tanzania na ndiyo maana hata Magufuli amekufa.

Unachoita maendeleo ni upuuzi mtupu wakati wananchi hawana uhuru wa kujieleza.
 
Mkuu

Kuna ukweli fulani kwenye hicho ulichoandika!

Mimi nitalia na DOLA (the state)siku zote!

Waliruhusuje chama tawala kikaanza kupambana wapinzani wake badala ya kupambana na maendelao ya UZALISHAJI na technolojia!!?

NGUVU iliyotumia ccm kupambana na vyama vya UPINZANI ni KUBWA Sana KULIKO iliyowekeza kupambania maendeleo!

Leo Umeme,maji,viwanda,elimu na vinginevyo BADO kizungumkuti WAKATI wamekaa madarakani muda mrefu!!

Kuna tatizo KUBWA Sana la kidola linalotusumbua KULIKO hata maendeleo yenyewe!!!

DOLA ISINGEWAACHIA WANASIASA HATMA YA MAENDELEO YA NCHI INGESHIKA SEKTA ZOTE NA WANASIASA WAKABAKI KUWA WATEKELEZAJI TU WA SERA HIZI KULIKO KUWAACHIA WAO WAWE WATUNGA SERA NA WASIMAMIZI WA SERA HUSIKA!!!!

TATIZO DOLA NDIO IMEFELI KUWASIMAMIA WANASIASA KWA MGONGO WA KATIBA WAKATI KATIBA NI KARATASI TU AMBAYO IPO CHINI YA UWEZO WETU KUIREKEBISHA NA KUTEKELEZA KWA MBINYO WAKIUTENDAJI!!!

TUMECHELEWA SANA SANA SANA KWA WANASIASA KUWAACHIA HATMA YA NCHI YETU!
 
Kuna kitu kimoja mnapaswa kuelewa. Pamoja na kwamba Kagame yuko very strict, huwezi kulinganisha Rwanda na Tanzania. Udogo wa Rwanda unafanya iwe rahisi sana kuiendeleza na kuifanya iwe hiyo world class unayoisema.

Magufuli, pamoja na ubaya wake, alitaka kuifanya Dar es Salaam iwe kama ulaya, lakini asingeweza kuifanya Tanzania yote iwe kama ulaya.

Ndio maana hata Singapore, kwa infrastructure na usafi na uzuri hata ulaya hawaifikii, kwa sababu ni ka nchi kadogo sana, imeendelea kwa kutumia bandari tu. Hata Norway ni hiyo hivyo. Sasa utamlaumuje mtu mwenye eka 20 kuwa shamba lake sio safi kama yule mwenye eka moja?

Nenda South Africa, pamoja na uchumi wao mkubwa, ukitoka nje ya jiji kilometa 50 tu utaona maisha ya rural areas Tanzania tunawaacha kwa mbali sana.

Hata China, wanapendeza mijini tu. Kuna sehemu za vijijini China wako hoi sana.

Kwa hiyo usimsifie sana Kagame kuwa ameifanya Rwanda kuwa nchi ya kuigwa, wakati ka-nchi kadogo. Ukitaka kumsifia Kagame basi mlinganishe na Zanzibar, sio Tanzania bara
 
Kwa bahati mbaya sana dola ndio ccm na ccm ndio dola.

Hakuna maendeleo hapa mpaka Yesu anarudi
 
Mbona hulinganishi wingi wa raslimali? Kwa kifupi ni kwamba ukiweza kutumia kidogo ulichonacho basi kikubwa utakitumia vizuri zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…