Kutana na fundi rangi, kuna mengi ya kujifunza

Mkuu naomba ufafanuzi kipi ni bora zaidi katika ku skim kati wallputt, white cement au gypsum powder. Pia katika kupambana na chumvi zinazoharibu ukuta umetaja anti~chumvi, hili ndio jina rasmi la hii bidhaa?
 
White cement ni komesha ya chumvi na magadi
 
Hivi kati ya zile rangi za vipele na za kawaida unamshauri mteja apake rangi ipi?
 
Hivi kati ya zile rangi za vipele na za kawaida unamshauri mteja apake rangi ipi?
Ndg hii ni stone paint, kwasababu imetokana na mawe yaliyosagwa. Hapa kwetu tunaita Drewa ndo jina lililozoeka na wengi. Hii ni nzuri kwa mwonekano lakini kwa ushauri wangu inapendeza ukiipaka eneo dogo kama vile nguzo na vibaraza, kwani ikiwa utaipaka eneo kubwa baada ya miaka 3 na kuendelea ukiichoka huwezi kupaka rangi juu yake.
 
Hivi kati ya zile rangi za vipele na za kawaida unamshauri mteja apake rangi ipi?
Hii pia ni stone paint, 90% ni mawe yaliyosagwa, hapa kwetu inamajina tofauti kama vile Conmix,Wallmaster, Terast, Decor plaster, Rough Plaster, na mengine mengi kwani kila mtengenazi na jina lake. Mimi napendekeza hii, kwani hata ikiwa imepauka unaweza kupaka rangi ya kawaida juu tofauti na ile ya upele. Zote ni rafiki na unyevunyevu na mwonekano wake nimzuri na wa kuvutia tofauti na rangi ya kawaida.
 
Samahani hizo picha zilitakiwa zisimame.
 
Safi sana mkuu kazi nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…