Kutana na mtanzania aliyeacha kazi Bank ya Dunia ili ashone nguo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Jeffrey Jessey ni kijana wa Kitanzania ambaye baada ya kumaliza masomo yake aliajiriwa na Benki ya Dunia nchini Tanzania lakini aliacha kazi na kuanza kushona nguo akisema alipenda kushona nguo kwa sababu ni kitu alichokipenda.

Tangu aache kazi hiyo, sasa anamiliki kampuni inayoitwa Speshoz na ameajiri watu wengine ambao anafanya nao kazi.

Unaweza kuitazama hii kwenye hii Full interview


Kwa hisani ya Millard Ayo
 
Yuko vzr japo yupo katika industry yenye kashfa nyingi
 
Zuckerberg aliacha CHUO havard for facebook alikataa mapesa kibao look where he is

watu wanajitambua hawaishi Kwa kushinikizwa
 
Babangu baada ya kustaafu kazi alizawadiwa vyerehani 6 vya kisasa na mzungu, Lakini Kakangu mmoja hivi baada ya kufeli shule alikataa kwenda kusoma kupekecha chereheni kisa aliona mzee kama anamdharau kumbe Baba alikua na lengo zuri nae.
matokeo yake mpaka hii Leo yupo tu anasubiri nyasi zikue achukue slasher azikate,anasubiri mtembelee nyumbani awasindikize awapige vibomu. Dunia hii inahitaji wanaume wenye akili
 
Duh,ana umri gani???
 
Nampongeza sana kwa kuwa na ujasir wa kujiajir,kwa sasa anaingiza pesa zaidi ya hiyo 160 kwa siku,kingine yupo huru na anachokifanya,kwa hiyo siyo tegemez tena kwa sasa bal anategemewa,atafika mbali kwan alionesha nia na sasa ameanza kujenga pia jina,kujenga jina si jambo jepes na uzuri anajishughilisha na jez na mavaz mengine,hivyo nijuavyo wadau wa jez ni weng sana pia biashara ya jez inalipa hatar
 
Sure ni jefrey Jessey ex-seminarian mwezangu pale URU SEMINARY.. sie wenzake tuko tunatumikishwa ila always hukiniinspire sana
 
Ana determination, ila nimeshindwa kumuelewa amesema amemaliza 2011 na ameajiliwa kuanzia 2008 au hapo benk ya dunia aliajiriwa akiwa na diploma au form 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…